Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb) anapenda kuwafahamisha wananchi wote hasa wakulima kutumia mvua za vuli zilizoanza kunyesha katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani na Morogoro ambayo hupata mvua mara mbili (bimodal) kwa mwaka...