Muziki wa Tanzania ni jina la kutaja muziki wenye asili ya Tanzania ya leo. Kama ilivyokuwa kwa binadamu wengine, wakazi wa eneo ambalo hatimaye limekuwa nchi ya Tanzania, walikuwa na utamaduni wao. Utamaduni huu ulikuwa ukitofautiana kati ya kabila na kabila. Moja ya vipengele ilikuwa muziki...