Fid Q aelezea sababu ya Muziki wa Gospel kuondolewa kwenye tuzo

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Akiwa katika Kofia ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Fid Q ametolea ufafanuzi suala la kutokuwepo Vipengele vya muziki wa Injini katika Tuzo za Muziki Tanzania TMA akieleza sababu kuu mbili!

1. Aina ya Wadhamini na bidhaa zao ambazo pengine hazifungamani na itikadi za kidini! Jambo ambalo lilileta mtafaruku kwenye Tuzo za KTMA.

2. Uwepo wa dini zaidi ya moja nchini hivyo kuepuka baadhi ya maneno yanayoweza kuibuka kwa kudai ubaguzi wa kidini na vitu kama hivyo!

fid-q_0.jpg
 
Fid aache woga ajifunze kwa Nikki mbishi the G.O.A.T Mwana hip pop haitakiwi uwe mwoga mwoga sio anafuata upepo tu.
 
Gospel inasikilizwa na watu wa dini zote kwa kufanya hivyo tayari ameingia kwenye mtego wa udini
By the way yeye ni dini gani
 
Hawaogopi hata kusema hukumu imekaribia/

Na waimbaji wa dini hata wao pia/

Wanatuzwa na wanaotengeneza bia/

wanachanganywa na wanaofagilia/

maovu na starehe za kupita hii dunia…..

~Hao - Joh Makini
 
Back
Top Bottom