Baada ya kuona kuwa nyumbani kunanichosha jioni ile, nikaamua niende katika baa iliyokuwa mtaa wa nne kutoka katika nyumba niliyokuwa naishi.
Pindi nilipowasili katika lango kuu la baa nililakiwa na sauti ya muziki wa ngwasuma ya Kikongo iliyokuwa ikirindima kutoka katika jukebox. Nilisimama...