MWISHONI mwa wiki, Tanzania ilipokea heshima ya aina yake kwa watanzania watano waliotunukiwa udaktari wa heshima ya Chuo Kikuu cha Read Impact kilichopo Colorado nchini Marekani.
Tukio hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Tanganyika 2 ulioko kwenye Hoteli ya Land Mark, Ubungo jijini Dar es Salaam...