Nilipohitimu shahada yangu ya kwanza ya elimu mwezi wa saba mwaka 2014 kule Mtwara kwenye chuo cha STAMUCO nikaamua kurejea nyumbani Dar-es-Salaam, nikaona nisibweteke na kungojea ajira za Serikali, nikaamua kujiunga na shughuli za hapa na pale angalau niwe napata hata fedha za kuweza kununua...