Huu ni wakati muhimu kwa vyama vya siasa kujipanga vyema, maana uchaguzi mkuu ni msimu wa mavuno—wakati wa kuuza sera kwa wananchi na kuona matokeo yake. Ukizubaa, umeliwa.
Changamoto ipo kwa CHADEMA na kampeni yao ya "Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi." Kaulimbiu hii ni tamu, inavutia kisiasa...