ccm

Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama tawala nchini Tanzania na chama cha pili kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya Chama cha True Whig cha Liberia. Kilianzishwa mwaka 1977, baada ya kuunganishwa kwa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar.
  1. JamiiForums Tanzania CCM na RPF ni vyama ndugu tangu lini?

    Nijuavyo mimi RPF kimepindua kuingia madarakani, CCM ilishiriki vipi kwenye mapinduzi ya Kagame hadi CCM kuvialika RPF na CNDD-FDD? Chama cha mambuzi bhana!!!!
  2. L

    JamiiForums Tanzania Demokrasia iliyopo ndani ya CCM ni mfano wa kuigwa kwa vyama vyote Barani Afrika, hakuna wa kukiondoa madarakani

    Ndugu zangu CCM Ni Kama Maji usipoyanywa utayaoga Tu,Huwezi ukazikwepa kuzisikia habari za CCM,huwezi ukajipa upofu wa kutokuona ukubwa na mizizi ya cccm hapa nchini,huwezi ukazuia habari za CCM na ukafanikiwa,huwezi ukaishinda CCM katika medani za kisiasa,huwezi ukaibomoa CCM hata kwa...
  3. JamiiForums Tanzania Sengerema: Diwani wa Buzilasoga (CCM), David Shilinde afikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji

    Diwani wa Buzilasoga (CCM), David Shilinde na watu wengine 13 wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Getruda Dotto. Mbali na diwani huyo, yumo pia Mwenyekiti wa CCM Kijiji cha Ikoni B, William Nengo...
  4. T

    JamiiForums Tanzania Naamini lengo la CCM ni zuri lakini hili la kuteua wagombea siku moja kabla ya uchaguzi linafikirisha

    Kidumu Chama cha mapinduzi, Pongezi na hongera kwa kila mmoja aliyefanikisha uchaguzi wa Chama na jumuiya kwa ngazi zote. Mmefanikisha kuitekeleza demokrasia kwa vitendo. Kesho tarehe 07/12/2022 Chama kinakwenda kuhitimisha uchaguzi kwa kuchagua viongozi wakuu wa chama na wajumbe wa NEC Taifa...
  5. K

    JamiiForums Tanzania Rais Samia ateuliwa kuwa mgombea wa Uenyekiti wa CCM

    Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imempitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa mwaka 2022 hadi 2027 na jina lake litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu December 07 kwa ajili ya kupigiwa kura. Katika mkutano huo pia...
  6. JamiiForums Tanzania Nawatakia heri CCM katika Mkutano wao Dodoma

    Hapa nataka kuandika something like an imaginary speech kuwaalika wajumbe. Kama anavyofanya Xi Jin Ping. Wengine labda watataka kuiendeleza. Karibuni Dodoma wajumbe wote. Tunakutana katika hali ambapo changamoto nyingi zinatukabili, kwa mfano vita ya Ukraine ambayo inayumbisha uchumi wa...
  7. JamiiForums Tanzania Uchaguzi ndani ya CCM: Je, January na Nape watakatiza mbele ya Wajumbe wenye hasira?

    Hakika kuna za chini ya kapeti kuwa wajumbe wengi wanakasirishwa na utendaji na tabia za hawa vijana wa Samia wanaowania nafasi zile 15 za kapu ndani ya Halmashauri Kuu na wameahidi kuwafundisha adabu ya utumishi ni kuheshimu walio chini. Kuna habari pia kuwa Mama Mwenyekiti anawataka hao...
  8. JamiiForums Tanzania Shaffi Dauda ni kijani tupu

    Mimi nilidhani yuko Qatar kumbe karudi ili kuhudhuria mkutano mkuu mkubwa wa CCM utakaofanyika tareh7-8/12/2022 mjini Dodoma. Pia na mimi najiandaa kuanza safari usiku huu kutokea Chunya, Mbeya kupitia Tabora ili kuweza kuudhuria mkutano mkuu huo. Nawasilisha kwa sasa safarini kutokea Chunya...
  9. JamiiForums Tanzania CCM wanaleta siasa za kijima. Wanapanga wenyewe sherehe baadaye anatokea kiongozi wao anaghairisha ili wapate sifa

    Huu mchezo nilikuwa naukemea tangu enzi za Magufuli. Hii leo ni zaidi ya mara 4 sherehe za kitaifa kughairishwa na viongozi kisha fedha kuamuru zipelekwe kwingineko. Rais hupatiwa kitabu chote cha bajeti kabla haijasomwa naye hutoa mapendekezo au amri zake. Kisha hurudi kwa wahusika. Sasa huu...
  10. JamiiForums Tanzania Kigwangalla: Kwanini Serikali imenunua mabehewa ya SGR yaliyotumika (used)?

    Mbunge wa Nzenga Vijijini Dr. Hamisi Kigwangalla kupitia mtandao wa twitter amehoji kwanini Serikali imenunua mabehewa “used” Amesema “Hili behewa moja (tena used) limenunuliwa kwa sh ngapi? Tumeambiwa yapo haya mabehewa 54, yamenunuliwa kwa us$ 59mn. Kwa hiyo behewa moja ni us$ 1,092,592...
  11. S

    JamiiForums Tanzania Ni kweli kuwa Shaka ni mpwa wa Rais Samia? Na kama ni kweli CCM mmebariki nepotism hii ndani ya chama?

    Niko Zanzibar kutafuta namna ya kuufanya mkono uende kinywani. Katika stori mbili tatu mwenyeji wangu kagusia kuwa Shaka ni mpwa wa rais Samia. Nimestushwa sana na hiyo kitu ambayo mwenyeji wangu ananiambia kuwa kwa hapa Zanzibar inajulikwna na kila mtu. Hebu ndugu wadau nijuzeni. Habari hii...
  12. T

    JamiiForums Tanzania Kuelekea mkutano mkuu wa CCM Taifa, natamani kuona uongozi mpya wenye ushawishi

    Amani iwe nanyi, Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema, amani, upendo, umoja na mshikamano kwa taifa letu. Ni mengi makuu Mungu ametenda maishani mwetu kustahili shukrani kuu. Pia, nakipongeza CCM kwa kudumisha utamaduni wa kuandaa chaguzi za kidemokrasia...
  13. S

    JamiiForums Tanzania Wana CCM ambao kazi yetu ni kuipigania CCM mitaani na mitandaoni lakini hatuteuliwi tukutane hapa

    Kucha kutwa sisi kazi yetu ni kupambana na wananchi wanaoibeza CCM huko mitaani na mitandaoni. Lakini miaka inaenda, mvi zinaota kichwani, nyuso zinajikunja kwa kupigwa na maisha magumu na hatuteuliwi kugombea au kupewa nyadhifa. Ukifika wakati wa uchaguzi mkuu utasikia CCM ina wenyewe. Hapo...
  14. JamiiForums Tanzania Harufu ya Rushwa CCM Mkutano Mkuu

    Chama cha Mapinduzi kimetangaza Tarehe 7 na 8 Disemba ni Mkutano Mkuu wa Taifa wa ambao utakuwa na jukumu la kuwachagua viongozi wapya ngazi ya Taifa suala la rushwa limeonekana kuitia doa CCM. Tayari malalamiko yameanza kutolewa kwa baadhi ya wagombea kudaiwa kutoa hadi milioni 5 kwa kila...
  15. JamiiForums Tanzania CCM wanaongoza nchi kisanii, ngumu sana kwa Tanzania kusonga mbele bila mbadala

    Nitataja mambo kadhaa 1. Kwanini mchakato wa katiba mpya awamu ya pili ya Mh Jakaya utumie mabilioni ya pesa kisha uwe abandoned kirahisi tu hivi????. Hizo fedha zingesaidia kumaliza tatizo la maji mikoa kadhaa yenye shida ya maji. They don't care 2. Baada ya zoezi la sensa meseji zinazotumwa...
  16. J

    JamiiForums Tanzania Dodoma: CCM yaitisha viongozi wake wote nchi nzima kuanzia Dec 07

    TANZANIA CHAMA NI KIMOJA TU CCM
  17. T

    JamiiForums Tanzania Hayati Magufuli ndiye mtu pekee toka CCM kuwahi kisifiwa na uongozi wa CHADEMA akiwa Waziri wa Ujenzi

    Sikumbuki ni mwaka gani lakini nakumbuka kwenye moja ya bajeti zake aliitekeleza kwa ufanisi Kwa kiwango ambacho hata Mbowe na wenzie walikosa kabisa cha kukosoa wakaishia kusifia tu. Kwa jinsi hiyo hata CHADEMA wangekuwa na mtu kama Magufuli wasingeacha kumpa bendera agombee Urais kwa chama...
  18. P

    JamiiForums Tanzania CCM haiaminiki hata kidogo kwa sasa. Tuna uhakika gani ikiwa siyo wao wanaohusika na ukamatwaji wa ndege zetu?

    Siwachoshi! Mliorogwa na jina JPM muendelee kuamini kuwa hasara zote za nchi hii chanzo chake ni yeye hata kama miaka miwili yuko kaburini! Swali ni je, ndege yetu iliyokamatwa huko imefanya safari ngapi za kwenda na kurudi hata kabla ya JPM kuwepo? Tutaaminije kama siyo mikono michafu ya...
  19. JamiiForums Tanzania CCM tujifunze kutoka kwa CCP ya China

    Wenzangu wa CCM tujifunze kutoka kwa CCM mwenzetu wa China. Yeye yupo kwa maslahi ya China kwa 100% lakini sisi wengi wetu kwa 100% wapo kwa maslahi yao. Tukutane tukae tuunde mfumo wa kudhibiti rushwa ndani ya chama. Tupate viongozi waadilifu na wenye kuisimamia nchi isonge mbele. Tuache...
  20. K

    JamiiForums Tanzania CCM jikiteni: Kupunguza rushwa na Katiba

    Mimi nashauri CCM badala ya kupoteza muda kusifia kinafiki mngetumia muda kwenye vitu viwili 1. Rushwa ambayo inarudi kwa kasi 2. Muwe na mapendekezo yenu kwenye katiba badala ya kutumia muda na nguvu kuzuia mchakato. Kwenye katiba tumieni mijadala na ipinzani kujadili mambo ambayo...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…