Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 274
- 781
Mbunge wa Nzenga Vijijini Dr. Hamisi Kigwangalla kupitia mtandao wa twitter amehoji kwanini Serikali imenunua mabehewa “used”
Amesema “Hili behewa moja (tena used) limenunuliwa kwa sh ngapi? Tumeambiwa yapo haya mabehewa 54, yamenunuliwa kwa us$ 59mn. Kwa hiyo behewa moja ni us$ 1,092,592 ambayo ni sawa na 2.57bn! Hivi hizi ni taarifa za kweli ama? Yamekuja 14 ya awali, bado 45. Kwa nini wametununulia used?”
Dk Hamisi Andrea Kigwangalla alizaliwa Agosti 7, 1975 mkoani Kigoma. Baba yake mzazi Nasser Kigwangalla alikuwa mfanyakazi wa benki na baadaye mwandishi wa habari, huku mama yake mzazi, Bagaile Lumola akiwa mwalimu na baadaye akaingia katika siasa ndani ya CCM.
Baba na mama wa kijana huyu ni “Wanyamwezi” wa Tabora kwa asili, na kuzaliwa kwa ‘Kigwa’ mkoani Kigoma kulitokea kwa vile wazazi wake wote walikuwa waajiriwa huko.
Kigwangalla alitumia sehemu ya maisha yake ya utotoni katika maeneo ya Goweko na Mlimani yanayopatikana Wilaya ya Uyui mkoani Tabora na alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Kigoma kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Baadaye alijiunga kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Shinyanga (Shy Bush) akichukua mchepuo wa PCB (Physics, Chemistry, Biology). Mwaka 1999 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alichukua masomo ya udaktari wa binadamu na alihitimu shahada yake mwaka 2004.
Watu waliosoma na Kigwangalla pale ‘Shybush’ na hata chuo kikuu, wanamtazama kama kijana wa Kitanzania mwenye juhudi, anayependa kujisomea, anayependa uongozi wa kujitolea na mwanamichezo mahiri.
Kwa sasa ni Mbunge wa Nzega Vijijini kupitia chama cha mapinduzi (CCM)

Picha aliyo ambatanisha
Akijibu swali la mdau mmoja aliyesema kuwa mabehewa hayo ni mapya, Dr. kigwangalla amesema “Ulipata Bahati ya kwenda kuyaona Kwa karibu? Kwa taarifa rasmi nilizonazo, walichelewa kuweka order ya mabehewa, hivyo wakalazimika kuchukua hayo ya zamani sema yamefanyiwa refurbishment/ pimping /facelift kidogo”
Kigwangalla amesema "Mama hahusiki kwenye ununuzi wa mabehewa, hao ni watu wetu wa TRC tu. Na Ndiyo maana tunahoji kwa Uhuru kabisa! Watoe majibu. Najua mama yuko na sisi, tunachofanya ni kumsaidia kazi ya kuwawajibisha watu wajanja wajanja! Peke yake hawezi kufanya yote haya!"Kigwangalla said:We certainly need more transparency in procurement!