ccm

Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama tawala nchini Tanzania na chama cha pili kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya Chama cha True Whig cha Liberia. Kilianzishwa mwaka 1977, baada ya kuunganishwa kwa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar.
  1. chiembe

    JamiiForums Tanzania CDM hawataruhusu aina ya Magufuli waingie madarakani, bora waunge mkono timu SSH. Sawa kwa CCM asili pia, ni mchezo mgumu kucheza!

    Yaani Chadema Bora muwaue kuliko team Magu warudi madarakani, na Bora CCM asili muwaue kuliko wakubali team MAGU warudi madarakani. Hard cards to play
  2. Determinantor

    JamiiForums Tanzania Utabiri, 2023 utakuwa mwaka mgumu sana kwa CCM

    Ndio hivyo, 2023 Itakua ngumu sana kwa wanazi wa CCM! Kuna ambao watakubali kubadilika Ili waendelee kula, Kuna kundi litaibuka kimya kimya likijiandaa kuweka mizizi, Kuna Viongozi wa CCM watapandishwa Kwa Pilato. Utakua mwaka wenye machungu sana kwa CCM na mara nyingi watajitokeza hadharani...
  3. DELETED ACCOUNT

    JamiiForums Tanzania Sakata la Feisal Salum linahusiana vipi na siasa za ndani ya CCM?

    Ngoja leo niwape za ndani ndaniii kabisa. Kuna mwanasiasa mmoja ambaye kwa miaka ya hivi karibuni amejipenyeza katika mambo ya mpira ili kutafuta ushawishi wa kisiasa. Wote tunajua kuwa toka Mwendazake aondoke, kumekuwa na mtifuano wa chini chini ndani ya chama kati ya wale waliokuwa wamewekwa...
  4. Gaganiga

    JamiiForums Tanzania Lini CCM itatoka madarakani?

    Hivi ccm inaweza kutoka madarakani? na kama ikitoka ni lini? Nakili kusema ccm kuitoa kupitia Sanduku la maoni tusahau na tusifikiri hata kidogo yaani sio leo wala kesho kwa ccm hii kutoka madarakani. Kwanza itatokaje? Na kivipi yaani? Kama Rais pia ni mwenekiti wa Chama hapo kuna kutoka...
  5. kmbwembwe

    JamiiForums Tanzania Tukumbushane kuhusu itikadi ya CCM

    Tulikubaliana ujamaa ni utu ni usawa na haki kwenye uchumi. Tulipogundua hatuwezi kujenga ujamaa kwa uwekezaji wa umma kwenye viwanda na biashara tukaamua kutumia sekta binafsi kwa uwekezaji wa ndani na wa nje. Kwa msingi huo mpango wa CCM ukawa ni kuendeleza umma kupata maendeleo ya kiuchumi...
  6. C

    JamiiForums Tanzania Mzee Tanzania na Mama Mkubwa CCM

    Toka mzee wetu azaliwe na kubahatika kumpata mke wa kwanza wa kumtunza Februari 5, 1977 na kuwa mama wa Watanzania wote bara na visiwani kwa miaka mingi, hatimaye mwaka 1992, mzee kwa kushirikiana na mke mkubwa, aliweka wazi wazo lake la kuwa na wake wengi. Wakaibuka wengi kwa namna ambayo...
  7. Mystery

    JamiiForums Tanzania Je, Serikali "imevilazimisha" vyombo vya habari viripoti habari nzuri pekee za watawala wa CCM?

    Kwa nchi yoyote yenye utawala Bora, inavitumia vyombo vya habari kama mhimili wao wa 4, usio rasmi, baada ya mihimili rasmi ya Serikali, Mahakama na Bunge, katika kuendesha nchi. Huwa wanavitumia vyombo vya habari kama "watchdogs" vyao Kwa kuwa huwa wanakosoa, Ili serikali Ione mapungufu yake...
  8. britanicca

    JamiiForums Tanzania Sawa mmeichoka CCM, je mbadala wao mna waamini!?

    Daily na waambia hapa Muda ni mwalimu mzuri sana mpaka tunafika 2030 Mungu atuweke ndo watu wataanza kushangaa kwamba pamoja na baadhi ya CCM wenye misimamo mikali huwa hata Chama kiteteleke vipi hawakimbii kwingine ? Ni kwasababu huko kwingine ni mzaha hakuna nia ya dhati ya kumkomboa Mtanzania...
  9. peno hasegawa

    JamiiForums Tanzania Tetesi: Serikali ya CCM yashindwa kulipa Posho za Madaraka ya Walimu Wakuu, Wakuu wa shule, vyuo, na Maafisa Elimu kata pamoja na ruzuku za shule Dec 2022

    KUTOKANA na Hali mbaya ya uchumi, pamoja na serikali kumiliki deni la Taifa la Trilion 91, Serikali imemshinda kuwalipa Posho za madaraka ya walimu wakuu,wakuu washule,vyuo,na maafisa elimu kata pamoja na ruzuku za shule Kwa kipindi cha Mwezi Novemba na Decemba 2022. Hali hii imekwenda mbali...
  10. J

    JamiiForums Tanzania Kenya inaongoza uzalishaji Avocado Afrika. Tusipokuwa makini chini ya CCM kuna siku Kenya itailisha Tanzania

    ..Majirani wako makini kwelikweli ktk masuala ya kilimo, na wanazingatia viwango. ..angalia video hizi mbili kuna mengi ya kujifunza kuhusu namna ya kufanya kilimo.
  11. S

    JamiiForums Tanzania Wananchi tuwe makini tunapochagua viongozi. Huyu anayejipiga picha na taulo naye alikuwa Diwani?

    Tuchague watu wenye maadili mema katika jamii. Huyu mtu anautafuta uzee lakini anafanya mambo ya mtoto wa darasa la 3. Vipi alipokuwa chini ya umri wa sasa akili yake ilikuwaje? Huyu jamaa aliwahi kuwa Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma. Najiuliza, wananchi waliona nini cha...
  12. Gaganiga

    JamiiForums Tanzania Kwa haya ninayoyasikia na kuyaona! Tusahau CCM kutoka madarakani kwa namna yoyote ile

    Ndiyo ukweli halisi huo kuitoa ccm kwenye Uongozi wa nchi msifikirie na wala msiwaze hata kidogo kama nyie wenyewe hata kujiongoza hamuwezi na tunajikuta wanaharakati wa mitandao kwahiyo ndugu zenu au bibi zenu wa bara wanaifahamu Twitter au jamiiforum? Nyie kutwa kazi ya kupiga kelele humu...
  13. M

    JamiiForums Tanzania Uraibu wa kamari za Kichina, mabonanza na pombe kali unazidi kumaliza watumishi wa umma. CCM ipo kimya

    Walimu, madaktari na watumishi wa kila kada wanajimaliza kwa pombe kali na kucheza kamali za kichina maarufu kama bonanza. Mishahara ikitoka ni kucheza makamali tu na kunywa pombe kali. Wanasahau familia zao na kutoa matumizi. CCM ipo kimya. Watumishi wanahitaji msaada wa kisaikolojia.
  14. GENTAMYCINE

    JamiiForums Tanzania Wajumbe wa MCC Kawe ina maana hata hapa 'JamiiForums' mpo pia na bado tu 'Mnanisagia Kunguni' Mwanenu?

    Wajumbe wa MCC Kawe kama mpo pia na hapa JamiiForums naomba nichukue nafasi hii kuwatakeni radhi kama kuna nilikowakosea ili mnisamehe na nyota yangu ya kukubalika irejee kwa Jamii. Kwani kama kuna sehemu ya kipekee ambayo mara kwa mara nimekuwa nikitamba kuwa nakubalika, ni maarufu na mimi...
  15. Idugunde

    JamiiForums Tanzania Bila kuikataa na kuipinga hii CCM maisha ya Watanzania yatakuwa magumu na itakuwa ni janga kubwa

    Watanzania ni watu wa kujishughulisha. Wanapambana maana wanalima, wanafuga na kufanya ujasiriamali wa kila namna. Ila ukweli ni kuwa CCM haina sera na mipango madhubuti ya kiuchumi kuwanyanyua Watanzania. Ufisadi na ubadhirifu usiokemewa na kudhibitiwa huruudisha nyuma maendeleo ya...
  16. Kabende Msakila

    JamiiForums Tanzania Toka 2000 CCM imebadili Wenyeviti mara 4, CDM na CUF hakuna

    WanaJf, Salaam za Krismas na Mwaka mpya 2023! Najiuliza tu iwapo taasisi za kivyama ni imara na wanavyama wana utimamu wa akili kwa nini CCM imebadili wenyeviti mara 4 tangu miaka ya 2000 wakati wanaojiita upinzani wakiwa na wenyeviti ving'ang'anizi wa madaraka. Hii kweli inatuonesha kwamba...
  17. L

    JamiiForums Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ndiye aliyenishawishi kujiunga CCM mwaka 2005

    Ndugu zangu, Rais mstaafu mh Jakaya Kikwete Ndiye Aliyenishawishi Kujiunga na CCM Mwaka 2005 Nikiwa mkoani Rukwa wilaya ya Sumbawanga vijijini, mji mdogo wa Laela Jimbo la Kwela lililokuwa linaongozwa na Marehemu Chrisant maji ya Tanga Mzindakaya. Nilikuwa huko kwa baba yangu mdogo ambako...
  18. Mystery

    JamiiForums Tanzania Je, kipaumbele cha CCM ni kuendelea kusalia madarakani au ni kuwaletea maendeleo Watanzania?

    Kutokana na mlolongo wa matukio yanayotokea nchini, nimekuwa nikijiuliza Sana, je kipaumbele Cha CCM, ni kuendelea kubaki madarakani au ni kuwaletea maendeleo watanzania? Kipaumbele Cha utawala wowote wa serikali ni kuwaletea maendeleo wananchi wake na kama wasipofanya hivyo, watajikuta...
  19. E

    JamiiForums Tanzania Inahitaji kuwa mjinga na kichaa kilichokubuhu kuendelea kuamini eti CCM italeta maendeleo!

    Miaka zaidi ya sitini, nchi bado hata haieleweki ni lini itaondokana na uchumi tegemezi licha ya kuwa na kila kitu. Kitabu cha mwanzo kwa wasomaji wa Biblia, nyoka alitambulika kama nyoka tuu, lakini kitabu cha ufunuo, nyoka anatambulika kama JOKA kwa sababu moja tu, nyoka, hakushughurikiwa...
  20. sammosses

    JamiiForums Tanzania CCM mtaogopa siasa za wazi hadi lini?

    CCM ni chama kikongwe kwa vyama vya ukombozi kusini mwa jangwa la sahara na Afrika kwa ujumla. Kilipaswa kuwa mfano bora kwa vyama vingine vya siasa kutokana na kuishi kwingi na kuona mengi. Ajabu ndicho chama kinacho ogopa siasa kuliko vyama vyote vya siasa nchini,kwa kulitambua hilo...
Back
Top Bottom