Inahitaji kuwa mjinga na kichaa kilichokubuhu kuendelea kuamini eti CCM italeta maendeleo!

embechanga

Member
Dec 22, 2022
10
16
Miaka zaidi ya sitini, nchi bado hata haieleweki ni lini itaondokana na uchumi tegemezi licha ya kuwa na kila kitu.

Kitabu cha mwanzo kwa wasomaji wa Biblia, nyoka alitambulika kama nyoka tuu, lakini kitabu cha ufunuo, nyoka anatambulika kama JOKA kwa sababu moja tu, nyoka, hakushughurikiwa mapema, na hatimaye akajidhatiti na kuwa JOKA litishalo

Kadiri tatizo linapozidi kuachwa, linazidi kuwa kubwa zaidi. Inawezekana kabisa, ccm Kwa sasa, inataka kufikia kwenye kiwango cha kuitwa JOKA, ni wakati wa kushughurikiwa na kila mtu mwenye akili timamu.

Miaka michache iliyopita, nchi yetu haikuwa na madeni, hii ni baada ya Rais aliyekuwepo kipindi hiko kuomba misamaha ya madeni.

Miaka michache tokea hapo hadi Leo, nchi yetu inadaiwa zaidi ya trillion 90 kiwango ambacho kinatishia ustawi wa maendeleo na radilimali zetu pamoja na nchi yetu Kwa ujumla.

Tumesikia nchi nyingi za Afrika zikifilisiwa na ama kunyanganywa bandari zao na ama viwanja vya ndege, ukisikia mwenzako kanyolewa, na wewe tia maji!

Ccm haiwezi tena kufanya chochote cha ajabu zaidi ya kuipeleka nchi kwenye kufilisiwa kutokana mikopo mingi isiyo na tija!

Nasema haina tija kwa sababu, hakuna uwekezaji wa maana unaofanywa kutokana na mikopo hiyo.

Kwa sasa deni la taifa, inahitaji serikali ikusanye kodi na isifanye chochote ndani ya miaka 3 ili kukamiliasha kulipa deni hilo! Bado unaiamini CCM kwamba inaweza kuleta maendeleo?

Kwa sasa CCM ni sawa na lile JOKA la kwenye Biblia, inahitaji Kwa pamoja tupambane nalo Kwa kufa na kupona, la sivyo, 90℅ ya watanzania, mjiandae kuishi kama digidigi polini ktk aridhi yenu yenye utajiri Mkubwa wa kupindukia!
 
Sasa kama mlimkataa Magu aliekuja na mikakati ya kizalendo mkaona ni Dikteta ,mkaona bora muwe na uhuru wa kuchart na kutukana kwenye mitandao kuliko Maendeleo .Mnataka mletewe mtu wa aina gani ?
 
Miaka zaidi ya sitini, nchi bado hata haieleweki ni lini itaondokana na uchumi tegemezi licha ya kuwa na kila kitu,

Kitabu cha mwanzo kwa wasomaji wa Biblia, nyoka alitambulika kama nyoka tuu,

Lakini kitabu cha ufunuo, nyoka anatambulika kama JOKA!

Kwa sababu moja tu, nyoka, hakushughurikiwa mapema, na hatimaye akajidhatiti na kuwa JOKA litishalo

Kadiri tatizo linapozidi kuachwa, linazidi kuwa kubwa zaidi,

Inawezekana kabisa, ccm Kwa sasa, inataka kufikia kwenye kiwango cha kuitwa JOKA, ni wakati wa kushughurikiwa na kila mtu mwenye akili timamu

Miaka michache iliyopita, nchi yetu haikuwa na madeni, hii ni baada ya Rais aliyekuwepo kipindi hiko kuomba misamaha ya madeni

Miaka michache tokea hapo hadi Leo, nchi yetu inadaiwa zaidi ya trillion 90 kiwango ambacho kinatishia ustawi wa maendeleo na radilimali zetu pamoja na nchi yetu Kwa ujumla,

Tumesikia nchi nyingi za Afrika zikifilisiwa na ama kunyanganywa bandari zao na ama viwanja vya ndege,

Ukisikia mwenzako kanyolewa, na wewe tia maji!

Ccm haiwezi tena kufanya chochote cha ajabu zaidi ya kuipeleka nchi kwenye kufilisiwa kutokana mikopo mingi isiyo na tija!

Nasema haina tija Kwa sababu, Hakuna uwekezaji wa maana unaofanywa kutokana na mikopo hiyo,

Kwa sasa deni la taifa, inahitaji serikali ikusanye kodi na isifanye chochote ndani ya miaka 3 ili kukamiliasha kulipa deni hilo! Bado unaiamini CCM kwamba inaweza kuleta maendeleo?

Kwa sasa CCM ni sawa na lile JOKA la kwenye Biblia, inahitaji Kwa pamoja tupambane nalo Kwa kufa na kupona, la sivyo, 90℅ ya watanzania, mjiandae kuishi kama digidigi polini ktk aridhi yenu yenye utajiri Mkubwa wa kupindukia!
CCM ndiyo chama pekee cha kuweza kuleta maendeleo. Wapinzani huo ni mkusanyiko wa EATERS, yaani ni ‘ASSOCIATION OF EATERS’ ‘AOE’. Tunaamini siku rais Samia akitoka madarakani na kuja rais mwingine wa kuchaguliwa na aliyeandaliwa mwenye uchungu na uzalendo wa Nchi yake Tanzania kila kitu kitakuwa vizuri. Rais Samia kazidiwa na genge la wezi
 
baada ya kuwaza kwa muda mrefu na kujiuliza sana ni kwa nini mwalimu hakutaka tupigane kudai Uhuru na badala akaudai kwa njia za amani? Nimeanza kupata majibu, kudai Uhuru nje ya utaratibu wa mwalimu nchi ingechelewa sana kupata Uhuru.

Siku zote nasema na nitarudia kusema upinzani unatuchelewesha sana na hawaheshimu kanuni na misingi ya maendeleo na mmojawapo ni maendeleo ni mchakato.

Mchakato wa maendeleo unatokana na sera na mipango na tuna sera za muda mrefu hususani ukamilishaji wa malengo ya MDG. Ahadi na ilani sio sera ila zinasaidia ukamilikaji wa sera kwa hiyo kipimo Cha muda mfupi Cha utekelezaji wa sera kwa CCM ni ilani. Swali, je ilani haitekelezwi?

Kingine ,sio vema kufanya comparison ya maendeleo yetu na ya nchi zilizoendelea. Ila kutwa kucha wapinzani wanakuja na agenda zile zile za upotoshaji kwamba tumechelewa sana kwa sababu ya CCM na hapo hapo bila aibu Wana compare na Marekani, Uingereza au ufaransa n.k

Kiasili watanzania ni wavivu sana na wanajisikia mno leo mtu akimaliza shahada ukimwambia kalime hakuelewi hata kidogo ila hapo hapo yupo tayari kwenda kuwa car wash Marekani wakati wanajivunia kwa chochote wanachofanya. Hivi unadhani kwa aina hii ya watu mtaendelea?

Nchi zote duniani zimeendelezwa na wazawa bila kujalisha utajiri au umaskini wao. Na usione vyaelea vimeundwa ,hakuna maendeleo yaliyopo kwenye nchi bila wazawa kujitoa kwa nguvu zote. Watanzania Kodi hawalipi kwa usahihi, uzalishaji hawafanyi wa kutosha, udanganyifu mkubwa kutoka shulen,vyuoni mpaka makazini na kulalamika sana,kukaa vijiweni na vilabuni muda wote. Nakuambia hakuna nchi yenye watu kama hawa itaendelea kwa haraka kama mnavyotaka kupotosha CCM haijafanya kitu.

Cha kufanya ambacho upinzani hawataki kusema kwamba hata Marekani wanafanya ni vyama kushirikiana kujenga nchi yao. Huwezi kukuta vyama nchi Marekani vinazozana kwa maslahi ya taifa lakini njoo hapa Tanzania kuna watanzania wapo upande wa mtu mweupe siku zote
 
Hapo unaendesha gari kwenye lami, polisi wanakulinda barabarani, mwanao anasoma, uko kwenye mtandao wa intaneti, umemaliza kuoga maji ya Bomba, unaangalia tv Kwa umeme.......mama yako Kijijini ametoka dispensary.............. .kama umemaliza kuny-a, na uko Dsm, mfumo wa majitaka unabeba kimba zako zilizosheheni dagaa na tembele
 
Porojo nyingi tu, kama hutaki maendeleo ya nchi hii kulinganishwa na Ulaya au Marekani basi yalinganishe na Korea Kusini, Malaysia, Vietnam, Singapore ambazo tulikuwa nazo karibia sawa kwa umaskini miaka ya 1960.
baada ya kuwaza kwa muda mrefu na kujiuliza sana ni kwa nini mwalimu hakutaka tupigane kudai Uhuru na badala akaudai kwa njia za amani? Nimeanza kupata majibu, kudai Uhuru nje ya utaratibu wa mwalimu nchi ingechelewa sana kupata Uhuru.

Siku zote nasema na nitarudia kusema upinzani unatuchelewesha sana na hawaheshimu kanuni na misingi ya maendeleo na mmojawapo ni maendeleo ni mchakato.

Mchakato wa maendeleo unatokana na sera na mipango na tuna sera za muda mrefu hususani ukamilishaji wa malengo ya MDG. Ahadi na ilani sio sera ila zinasaidia ukamilikaji wa sera kwa hiyo kipimo Cha muda mfupi Cha utekelezaji wa sera kwa CCM ni ilani. Swali, je ilani haitekelezwi?

Kingine ,sio vema kufanya comparison ya maendeleo yetu na ya nchi zilizoendelea. Ila kutwa kucha wapinzani wanakuja na agenda zile zile za upotoshaji kwamba tumechelewa sana kwa sababu ya CCM na hapo hapo bila aibu Wana compare na Marekani, Uingereza au ufaransa n.k

Kiasili watanzania ni wavivu sana na wanajisikia mno leo mtu akimaliza shahada ukimwambia kalime hakuelewi hata kidogo ila hapo hapo yupo tayari kwenda kuwa car wash Marekani wakati wanajivunia kwa chochote wanachofanya. Hivi unadhani kwa aina hii ya watu mtaendelea?

Nchi zote duniani zimeendelezwa na wazawa bila kujalisha utajiri au umaskini wao. Na usione vyaelea vimeundwa ,hakuna maendeleo yaliyopo kwenye nchi bila wazawa kujitoa kwa nguvu zote. Watanzania Kodi hawalipi kwa usahihi, uzalishaji hawafanyi wa kutosha, udanganyifu mkubwa kutoka shulen,vyuoni mpaka makazini na kulalamika sana,kukaa vijiweni na vilabuni muda wote. Nakuambia hakuna nchi yenye watu kama hawa itaendelea kwa haraka kama mnavyotaka kupotosha CCM haijafanya kitu.

Cha kufanya ambacho upinzani hawataki kusema kwamba hata Marekani wanafanya ni vyama kushirikiana kujenga nchi yao. Huwezi kukuta vyama nchi Marekani vinazozana kwa maslahi ya taifa lakini njoo hapa Tanzania kuna watanzania wapo upande wa mtu mweupe siku zote
 
Ujinga zaidi ni kuamini wale jamaa wanaoomba nauli ( chagadema) kwa rais Samia ili waende kula bata Marekani eti watakuletea maendeleo.
Kwan kasema CDM wataleta maendeleo? Hoja ipo very specific ambayo ww mwenyew unaweza tafakari kama ukitumia akili yako vzr. Miaka zaid ya 60 tunahangaika na maji saf, umeme, matundu ya choo mashulen? Na sahiv tuna survive kwa mikopo 😂😂😂
 
Sasa kama mlimkataa Magu aliekuja na mikakati ya kizalendo mkaona ni Dikteta ,mkaona bora muwe na uhuru wa kuchart naikujidhi kutukana kwenye mitandao kuliko Maendeleo .Mnataka mletewe mtu wa aina gani ?
Hatukuwai kuomba Mungu atupe rais chinja chinja! Tuelewane kwanza hapo!
Nakubaliana na wewe kwenye ujasiri na uthubutu wa jamaa lakin nia njema haikujidhihiri katika matendo na kweli! (Hakufanikiwa kuwa dikteta mzalendo..benevolent dictator)
Na kwa vile tunachohitaji hatujawai kukipata hasa kama taifa, binafs siwezi kulinganisha awam yoyote kwa mizania ya uzuri na ubaya kwa maana neno 'chanya' halipo ndan ya uhai wa ccm.
Ingawa kwa mizania ya ubovu dhidi ya ubovu, tuko afadhar leo maana walau kuna heshma na hofu ya Mungu dhidi ya uhai wa binadam, hata kama kimbari ya Taifa mama inaendelea!
(between two evils, we have a lesser evil currently)
 
Hujui historia kabisa, bora ungenyamaza tu.
Xi Jinping ni mpaka rangi tu kwenye historia ya China.
Wee bana weee, unadhan mpaka anaongezewa vipindi, ni Kwa sababu gan??

Xi Jinping ndie kaileta China hapa ,Jamaa kawaondolea wachina zaidi ya million 100 umasikin ,unajua umasikin wewe ??.

Sijui wazungumzia Historia gan aisee !!.

Yaan Xi Jinping ndo wakina JPM, wengine wanaser mipango, wao wanaitimiliza
 
Hata Museveni anaongezewa muda kwa miongo minne sasa.
Wee bana weee, unadhan mpaka anaongezewa vipindi, ni Kwa sababu gan??

Xi Jinping ndie kaileta China hapa ,Jamaa kawaondolea wachina zaidi ya million 100 umasikin ,unajua umasikin wewe ??.

Sijui wazungumzia Historia gan aisee !!.

Yaan Xi Jinping ndo wakina JPM, wengine wanaser mipango, wao wanaitimiliza
 
Ukiona unaamini tutapata maendeleo kwa mfumo huu jua tuu hujui maana ya maendeleo au huna akili timam
 
Back
Top Bottom