Tukumbushane kuhusu itikadi ya CCM

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,422
7,208
Tulikubaliana ujamaa ni utu ni usawa na haki kwenye uchumi.

Tulipogundua hatuwezi kujenga ujamaa kwa uwekezaji wa umma kwenye viwanda na biashara tukaamua kutumia sekta binafsi kwa uwekezaji wa ndani na wa nje.

Kwa msingi huo mpango wa CCM ukawa ni kuendeleza umma kupata maendeleo ya kiuchumi na sio kuendeleza na kujenga tabaka la wachache kumiliki uchumi wa nchi peke yao.

Ili kujenga ujamaa kutumia sekta binafsi inahitajika udhibiti mkubwa toka serikali ya ccm. Kwa hivyo ndio maana utaona mashirika ya umma ya udhibiti yapo na yamepewa kisheria madaraka makubwa.

Tatizo kubwa linalotuchanganya nchini toka mfumo huu wa kujenga ujamaa kwa sekta binafsi ni viongozi kwenye Serikali na chama kuwa na maslahi binafsi yanayopingana na yale ya umma.

Viongozi kama wabunge mawaziri hata rais ambao ni sekta binafsi.

Ili sekta binafsi kuendelezwa ili kujenga ujamaa inahitaji kudhibitiwa na uongozi wa serikali ya chama tawala CCM.

Hawa viongozi mabwanyenye kwa utajiri wengi utajiri wao umetokana na kula rushwa kutoka sekta binafsi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka, hawawezi kudhibiti sekta binafsi kwa faida ya umma.

Ili CCM iweze kuendelea kukubaliba lazima wabakie kwenye reli ya kuendeleza maslahi ya umma. Hakuna mbadala. Vinginevyo ule uongo wa wapinzani kwamba wanategemea wizi wa kura itakua kweli na hapo ndio amani itatoweka.

Ili kuendelea kupigiwa kura CCM inahitaji uongozi wa kimagufuli. Huu ni ukweli na mama akikaza shingo 2025 mtaona matokeo.

Wasalaam.
 
CCM ni chama cha wafanyabiashara na matajiri. Si vibaya lakini wafanyabiashara matajiri hawafiki 1% ya raia nchi hii. Hao ndiyo wanaamua mustakabali wa wengine wote.
 
Tulikubaliana ujamaa ni utu ni usawa na haki kwenye uchumi.

Tulipogundua hatuwezi kujenga ujamaa kwa uwekezaji wa umma kwenye viwanda na biashara tukaamua kutumia sekta binafsi kwa uwekezaji wa ndani na wa nje.

Kwa msingi huo mpango wa CCM ukawa ni kuendeleza umma kupata maendeleo ya kiuchumi na sio kuendeleza na kujenga tabaka la wachache kumiliki uchumi wa nchi peke yao.

Ili kujenga ujamaa kutumia sekta binafsi inahitajika udhibiti mkubwa toka serikali ya ccm. Kwa hivyo ndio maana utaona mashirika ya umma ya udhibiti yapo na yamepewa kisheria madaraka makubwa.

Tatizo kubwa linalotuchanganya nchini toka mfumo huu wa kujenga ujamaa kwa sekta binafsi ni viongozi kwenye Serikali na chama kuwa na maslahi binafsi yanayopingana na yale ya umma.

Viongozi kama wabunge mawaziri hata rais ambao ni sekta binafsi.

Ili sekta binafsi kuendelezwa ili kujenga ujamaa inahitaji kudhibitiwa na uongozi wa serikali ya chama tawala CCM.

Hawa viongozi mabwanyenye kwa utajiri wengi utajiri wao umetokana na kula rushwa kutoka sekta binafsi na ubafhilifu hawawezi kudhibiti sekta binafsi kwa faida ya umma.

Ili CCM iweze kuendelea kukubaliba lazima wabakie kwenye reli ya kuendeleza maslahi ya umma. Hakuna mbadala. Vinginevyo ule uongo wa wapinzani kwamba wanategemea wizi wa kura itakua kweli na hapo ndio amani itatoweka.

Ili kuendelea kupigiwa kura CCM inahitaji uongozi wa kimagufuli. Huu ni ukweli na mama akikaza shingo 2025 mtaona matokeo.

Wasalaam.
CCM haina itikadi kama chama kwa sasa CCM ni Chama Cha Magaidi wenye Nia ya kufilisi uchumii na maendeleo ya Tanzania na kudumaza fikra za wananchi wake.
 
Kunge kuwa na mijadala ya kusuka vyama vya upinzani ili viweze kuondoa huu mzizi mkuu (ccm) ulio beba matawi (vyama pinzani) ninge waelewa

Lakini kila siku kuishia kuisema ccm na kura hampigi, wanao piga kura na kuchagua ccm ni bibi zenu na vijana watiifu...

Tengenezeni mikakati, ondoeni chama mfukoni mwa mtu mmoja na familia/ukoo wake... chama kiondokane na ukanda, ukabila, udini nk...

Wakina Duni haji hawapo tena...
 
Back
Top Bottom