Search results

  1. Hot Lady

    Kwa nini umaarufu wa Saed Kubenea umeshuka baada ya kuwa mbunge wa Ubungo?

    Kuna mambo yanashangaza sana. Saed Kubenea kabla hajawa mbunge, hakika nilikuwa namuadmire sana kutokana na hoja alizokuwa anajenga. Nadhani hiyo ndio sababu ya wana Ubungo kumwamini na kumpa kura za kutosha hadi akawa mbunge. Hata hivyo, najiuliza sana nini kimemkumba? Kwa nini kapwaya sana...
  2. Hot Lady

    Kwa nini utajiri uliosemwa wa Ridhiwani Kikwete umetoweka baada ya baba yake kuondoka madarakani?

    Wakati Kikwete akiwa Rais, Ridhiwani Kikwete alitajwa kumiliki mali nyingi sana. Makampuni mengi yakiwemo ya usafirishaji yalidaiwa kuwa ni ya Ridhiwani. Hata nyumba zilizokuwa zinajengwa maeneo muhimu ilisemekana ni ya Ridhiwani. Humu kwenye social media mada za Ridhiwani zilikuwa hazikauki...
  3. Hot Lady

    Yule Mfanyabiashara kinara wa kutakatisha Milioni 7 kwa dakika hatimaye afikishwa Mahakamani

    Mfanyabiashara Mohamed Mustapha (anayeongea na simu) na wenzake, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kukabiliana na tuhuma za kuibia Serikali kodi ya Sh milioni 7 kwa kila dakika kwa kipindi kirefu. ** Hatimaye mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa...
  4. Hot Lady

    Kuna haja ya kuwa na sheria ili kuruhusu wanasiasa kutolewa kwa mkopo

    Nimetafakari sana jinsi anavyoteseka Julius Mtatiro. Nimetafakari sana jinsi Lowasa na Juma Duni Haji wanavyopitia wakati mgumu. Natafakari sana jinsi Zitto Kabwe anavyotamani kuwa kwenye chama kikubwa cha siasa. Natafakari sana jinsi Dr Slaa anavyotamani kurejea CCM. Natafakari sana jinsi David...
  5. Hot Lady

    Ni lini Frederick Sumaye amehamia CHADEMA?

    Ijumaa kareem ndugu zangu. Wakati Sumaye anatangaza kujivua uanachama wa CCM, alisema kuwa anaenda UKAWA lakini hakubainisha anaenda chama gani. Taarifa za ndani zilisema kuwa Sumaye anahamia NCCR na kwamba ndiye anayeandaliwa kugombea Urais ikiwa Lowasa ataishia njiani. Hata hivyo, akiwa...
  6. Hot Lady

    Dr Slaa aibuka shujaa mpya baada ya Nyerere nchini Tanzania. Wengi wapongeza msimamo wake

    HOTUBA ya kwanza tangu ‘atoweke' kwenye anga za siasa ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dokta Wilbroad Slaa, aliyoitoa juzi Jumanne juu ya kujiweka pembeni, imepokelewa kwa hisia tofauti huku wengi wakimuita kuwa ni shujaa wa taifa kutokana na ujasiri...
  7. Hot Lady

    Said Nkumba abadili gia angani. Soon kutangaza kurudisha kadi ya CHADEMA, kurejea CCM

    Kaka zangu habari za Jumamosi. Taarifa za kuaminika nilizopata kutoka chanzo cha kuaminika ni kwamba, aliyekuwa Mbunge wa Sikonge kwa tiketi ya CCM na ambaye ni mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Said Nkumba, yupo mbioni kujivua uanachama wa chama hicho, kuachia nafasi ya mgombea Ubunge na...
  8. Hot Lady

    Ukame wa wana CCM kuhamia CHADEMA, je Lowassa amefilisika au ameuziwa mbuzi kwenye gunia?

    Wakati Lowasa anahamia CHADEMA, alienda kwa tambo nyingi huku akiwaahidi viongozi wa CHADEMA kuwa kuna mafuriko ya wana CCM kuhama chama chao na kujiunga na CHADEMA. Hata hivyo, mpaka sasa, ni takriban wiki tatu sasa tangu mwanasiasa huyo ahamie CHADEMA na hakuna dalili za yale mafuriko...
  9. Hot Lady

    Lowassa aunda Timu ya watu watano kukabiliana na nguvu ya Magufuli Kanda ya Ziwa

    Habari za Jumatatu wapendwa. Taarifa nilizopata hivi punde zinasema kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA na UKAWA, Edward Lowasa ameteua timu ya watu watano ambao ndio watakaosimamia kampeni za kumnadi mwanasiasa huyo kanda ya Ziwa. Taarifa zinasema kuwa walioteuliwa kuchukua jukumu hilo ni...
  10. Hot Lady

    WIKIPEDIA wamkaanga Edward Lowassa, sijui ataponea wapi huyu bana

    Kaka zangu, hebu pakueni wenyewe muone jinsi wenzetu wazungu walivyoandika historia ya Edward Lowasa. Hakika inahuzunisha na inasikitisha. Nilijua haya mambo anasingiziwa kumbe hata wenzetu wazungu wanamuona vivyo hivyo. Kwa ujumla wake Lowasa ni fisadi na mtumiaji vibaya wa madaraka CHANZO...
  11. Hot Lady

    Kashfa nyingine ya Mbowe: Kumbe Juma Duni Haji hajakabidhiwa kadi ya CHADEMA

    Kaka zangu na wasomaji wote wa JF. Taarifa nilizopata hivi punde zinasema kuwa kilichofanyika kwa Juma Duni Haji ni ulaghai wa kisiasa. Kwamba, Juma Duni Haji ameteuliwa kuwa Mgombea Mwenza bila ya kuwa mwanachama wa CHADEMA. Hakika hii ni fedheha kubwa sana kwa MBOWE na chama chake cha...
  12. Hot Lady

    Nawaza kwa sauti juu ya hatma ya Edward Lowasa

    Nawaza kwa kina sijui vile vicoba vilivyokuwa vinafadhiliwa na Lowasa vitaendelea kupata mgawo. Nawaza tu Nawaza kwa sauti sijui zile helkopta alizokuwa anakodi Lowasa kwenye trip zake za kisiasa zitaendelea kutumika. Nawaza tu Nawaza kwa kina sijui kama Lowasa ataendelea kuchangia ujenzi wa...
  13. Hot Lady

    Ni sahihi kwa Mbowe kulala Hotel ya Dola 700 kwa siku huku wafuasi wake wakishindia Mikate na Maji?

    Jamani kaka zangu na dada zangu, natumai kuwa hamjambo. Leo nimeona na mie nianzishe mada baada ya kuwa mchangiaji kwa muda mrefu. Kama mtakumbuka kuwa baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutoa maneno ya uchochezi sambamba na kutangaza maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima kwa kile...
  14. Hot Lady

    Apson Mwang'onda, Mtaalam wa kuunda Mitandao isiyo na tija kisiasa, Lowassa kaa chonjo

    Wana body, nawasalimu nyote. Kwa siku kadhaa sasa, tumekuwa tukishuhudia mada mbalimbali zinazohusu mtandao wa Saidia Lowasa Aingie Ikulu ambao kwa mujibu wa taarifa hiyo mwenyekiti wke ametajwa kuwa ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa kati ya 1996 na 2006, APSON...
Back
Top Bottom