Apson Mwang'onda, Mtaalam wa kuunda Mitandao isiyo na tija kisiasa, Lowassa kaa chonjo

Hot Lady

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
1,035
638
Wana body, nawasalimu nyote.

Kwa siku kadhaa sasa, tumekuwa tukishuhudia mada mbalimbali zinazohusu mtandao wa Saidia Lowasa Aingie Ikulu ambao kwa mujibu wa taarifa hiyo mwenyekiti wke ametajwa kuwa ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa kati ya 1996 na 2006, APSON MWANG'ONDA.

Awali taarifa hizo ambazo zimekuwa zikitiririshwa na mdau muhimu sana humu JF, Chabruma, zilionekana kama ni za kutunga. Lakini kadri ya michango ya wadau mbalimbali na utetezi wake Apson Mwang'onda, imedhihirika kuwa taarifa hizo ni za kweli.

Hapa naomba mtambue kuwa kwa kawaida Apson hajawahi kujitokeza kwenye media kutoa ufafanuzi au kujibu hoja zilizoelekezwa juu yake. Apson hujitokeza kujibu hoja za kweli kwa lengo la kukanusha lakini mara zote amejikuta kikombe kikimwangukia yeye.

Katika kumbukumbu zangu, Apson amewahi kujitokeza mara mbili kukanusha hoja zilizomlenga. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2012 wakati Prof Mark Mwandosya alipotoa kitabu chake kiitwacho, Sauti ya Umma ni Sauti ya Demokrasia.

Katika kitabu hicho, Mwandosya alimshutumu Apson kwa kucheza rafu za kisiasa kwa kutumia taaluma yake ya Intelijensia kutengeneza mtandao wa kumfanya mwanaye, Thomas aka Thom Apson Mwang'onda awe M- NEC kwenye wilaya anayotoka Mwandosya mwaka 2007.

Mwandosya alilalamika kuwa Apson akisaidiwa na swahiba wake mkubwa, Edward Lowassa walitumia kiasi kikubwa cha fedha kinachokadiriwa kuwa ni milioni 300 ili tu mwanaye Thom awe M-NEC huku akifanya kila hila kumkandamiza kisiasa. Katika Utetezi wake, Apson alijibu kuwa hizo ni hasira tu za Mwandosya kwa vile hakumsaidia wakati wa harakati zake za kuingia Ikulu mwaka 2005.

Mara ya pili ambayo naikumbuka Apson kujitokeza hadharani ni hii juzi ambapo inadaiwa kuwa nyumba ya Apson inatumika kukutanisha wanasiasa ambao ni mtandao wa Edward Lowassa ambapo yeye ametajwa kuwa ndiye mwenyekiti wa mtandao huo. Katika utetezi wake, Apson anajibu kuwa yeye si mwenyekiti wa mtandao huo. Hata hivyo akasema kuwa kwani kuna tabu gani yeye kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Lowassa ilhali kwa sasa yupo huru?

Wadau, kutokana na saga hili, nikaamua kujichimbia ili kubaini uhalisia wa uhusika wa Apson kwenye mitandao. Baada ya kujichimbia, nimebaini kuwa Apson hajawahi kuanzisha mtandao wa kisiasa na kupata ushindi. nitaeleza kwa kifupi hapa chini.

Wakati wa kuelekea uchaguzi wa 2005, Apson Mwang'onda alianzisha kampeni kali za kumzuia Jakaya Kikwete asiwe Rais wa Tanzania. Apson akiwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa alihakikisha kuwa JK hapiti kwenye mchujo ndani ya chama chake, CCM. Hata hivyo, kwa vile nyota ya JK iliangaza kila kona, njama zake zikashindwa. Apson alikuwa kwenye Mtandao wa Prof Mark Mwandosya ambapo alimtumia mtoto wake Thom Mwang'onda kuratibu mtandao huo.

Mwaka 2007 wakati wa uchaguzi ndani ya CCM hasa katika nafasi ya U- NEC, Apson alitengeneza mtandao wa kuhakikisha mtoto wake Thom anakuwa mbadala wa Prof Mark Mwandosya. Katika mtandao huo, inadaiwa kuwa Apson alitumia kiasi kikubwa cha fedha kinachokadiriwa kufikia milioni 300 ambacho inaelezwa kuwa alipewa na swahiba wake mkubwa, Edward Lowasa.

Hapo pia Apson aliangukia pua na Mwandosya aliibuka kuwa mshindi kwenye nafasi hiyo. Inadaiwa kuwa Apson anamchukia sana Mwandosya na kwamba hata masahibu yaliyomkuta ya kuugua kwa muda mrefu yana mkono wake.

Kwa sasa Apson ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Lowasa. Hata hivyo. Taswira ya Lowasa kisiasa ni mbaya hasa kutokana na kutopea kwenye ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Pia inaelezwa kuwa afya ya mwanasiasa huyo ni mbaya sana kiasi kwamba hawezi kumudu majukumu ya Ukuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

Hata hivyo, Apson bado anang'ang'ana huku akimdanganya Lowasa kuwa atashinda nafasi hiyo kwa vile haoni mtu ambaye ni tishio kwake. Tamaa ya fedha na kutaka kuendelea kushawishi siasa ya nchi hii kumeelezwa kuwa ndo kunamsukuma Apson kuwa kwenye mtandao wa Lowasa.

Hata hivyo, ni vema Lowasa akasoma alama za nyakati na sijui kama alichukua muda wa kutosha kuchunguza ubora wa Mwenyekiti wa kamati yake, Apson. Hakuna mahala pamethibitika kuwa Apson ameshawishi kisiasa na akafanikiwa. Yeye ni mtu wa kufeli. Sijui kazaliwa siku ya Jumanne? Lowasa zinduka na kaa chonjo. Apson hatakusaidia na badala yake atakusababishia shinikizo la damu pale utakapoona kuwa jina lako halipo miongoni mwa wagombea watano waliopendekezwa na Kamati Kuu ya chama chako kwa ajili ya kupigiwa kura na mkutano Mkuu. Ni bora ukatumia fedha ulizonazo kupanga vema muda wako wa uhai uliosalia.
 
Naona vijana wa membe mnaangaika kweli.. nenda mwambie boss wenu kuwa hamuwezi lowassa kamwe.
 
Mtake msitake LOWASSA ndo rais ajaye wa JMT,hilo niko tayari kulisemea bila uwoga wowote kwani CCM hawana any option,if they want to loose and kuwaganyika vipande vipande wajaribu kutompitisha LOWASSA chezea morani wa kimasai wewe shye,sisi haogopi kuliwa na simba na sio kumeswa na samaki ni aibu etii kwa morani
 
Mkuu, kwani humu JF tunatumia pen au penseli wakati wa kuchangia?

Mkuu si lazima itumike kalamu ya wino au ya risasi ili utambue mawazo ya mtu yanayoishi katika maandishi yake...

Neno 'mwandiko' lisikuchanganye sana!!!
 
Mtake msitake LOWASSA ndo rais ajaye wa JMT,hilo niko tayari kulisemea bila uwoga wowote kwani CCM hawana any option,if they want to loose and kuwaganyika vipande vipande wajaribu kutompitisha LOWASSA chezea morani wa kimasai wewe shye,sisi haogopi kuliwa na simba na sio kumeswa na samaki ni aibu etii kwa morani
Mkuu, kwani wewe ni CC ya CCM?
 
Khaaa wewe dada, mwache babu Lowasa apumue jamani. Kila kukicha mnamwandama. Kawakosea nini? Mtamuua kwa pressure bure. Si mnaona jinsi afya yake ilivyo mgogoro?
 
Khaaa wewe dada, mwache babu Lowasa apumue jamani. Kila kukicha mnamwandama. Kawakosea nini? Mtamuua kwa pressure bure. Si mnaona jinsi afya yake ilivyo mgogoro?
Mtu kama anashindwa kucare afya yake ni bora mkaendelea tu kumwandama. Inaelekea yeye tamaa ya madaraka ni bora zaidi kwake kuliko afya yake
 
Back
Top Bottom