Hot Lady
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 1,035
- 638
Ijumaa kareem ndugu zangu.
Wakati Sumaye anatangaza kujivua uanachama wa CCM, alisema kuwa anaenda UKAWA lakini hakubainisha anaenda chama gani. Taarifa za ndani zilisema kuwa Sumaye anahamia NCCR na kwamba ndiye anayeandaliwa kugombea Urais ikiwa Lowasa ataishia njiani.
Hata hivyo, akiwa Mkoani Simiyu, Sumaye ameonekana amevaa jezi za CHADEMA hali inayoashiria kuwa na yeye amejiunga kwenye chama hicho. Nadhani Sumaye ameangalia upepo hasa kutokana na viongozi waandamizi wa NCCR Mageuzi kumjia juu Mwenyekiti wao na kutishia kujiondoa UKAWA. Wakati Sumaye akionekana amevaa jezi za CHADEMA, Lowasa ameendelea kugombea kuvaa gwanda za chama hicho ambapo amekuwa akibadilisha mashati huku kila analovaa kutoshabihiana kabisa na sare za chama chake.
Kwa mtazamo wangu, ikiwa Sumaye ameelekea CHADEMA, ni dhahiri kwamba viongozi wote wa UKAWA kwa sasa ni CHADEMA na kwamba hata huyu Mbatia kinachomuweka NCCR ni jimbo la Vunjo tu na baada ya Uchaguzi atatimkia huko kwa vile hana uwezo wa kushinda jimbo hilo