Dr Slaa aibuka shujaa mpya baada ya Nyerere nchini Tanzania. Wengi wapongeza msimamo wake

Hot Lady

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
1,035
638
HOTUBA ya kwanza tangu ‘atoweke' kwenye anga za siasa ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dokta Wilbroad Slaa, aliyoitoa juzi Jumanne juu ya kujiweka pembeni, imepokelewa kwa hisia tofauti huku wengi wakimuita kuwa ni shujaa wa taifa kutokana na ujasiri wake.

Katika mahojiano yaliyowahusisha wananchi na wachambuzi mbalimbali wa mambo ya kisiasa kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mara baada ya kiongozi huyo kukutana na waandishi wa habari, walisema kuwa, Dokta Slaa ni mtu wa aina yake ambaye taifa halijapata kuwa naye tangu kuondoka kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Wengi walionesha kufurahishwa na misimamo ya kiongozi huyo tangu ajiingize kwenye masuala ya siasa, kwani siku zote amekuwa mstari wa mbele kuwatetea wanyonge, kuanika maovu na kukemea kila analoliona lipo tofauti na anavyoamini.
"Kwa kweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Dk. Slaa ni kati ya viongozi wenye msimamo asiyekubali kuyumbishwa. Amekuwa hivyo tangu nilivyomjua na hata hotuba yake aliyoitoa juzi, inadhihirisha hilo," alisema Chande Juma wa Kinondoni jijini Dar.

Alisema kama mtu alifuatilia vizuri mazungumzo yake, ni wazi kuwa viongozi wenzake walikubali kubadili msimamo ili kumwezesha Lowassa aingie Chadema, lakini yeye akakataa licha ya kamati ndogo kuundwa ili imshawishi alegeze msimamo.

Mchambuzi mmoja wa habari za siasa aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema siku zote anamtambua Dk. Slaa kama mtu mwenye kuichukia rushwa, kwani anaamini hicho ndicho chanzo cha matatizo yote yanayosababisha kero za wananchi kutoisha, licha ya nchi kuwa na rasilimali za kutosha.

"Unampata wapi sasa hivi aina ya kiongozi ambaye anaweza kukataa rushwa ya shilingi milioni 500 akitetea masilahi ya wananchi masikini? Viongozi wetu wa sasa kila mtu anaweka mbele masilahi yake na familia yake, suala la kuwatetea wanyonge wanalifanya kama maigizo tu," alisema mchambuzi huyo, akikumbushia jinsi mbunge huyo wa zamani wa Karatu alivyokataa kiasi hicho cha fedha ili ashiriki kuzuia ripoti ya Kamati ya Bunge juu ya sakata la Richmond isisomwe bungeni.

Maneno kama hayo yalisemwa pia na mkazi mmoja wa Sinza, Nicholaus John akirejea jinsi alivyokataa rushwa ya uongozi pale alipoahidiwa kazi nje ya nchi, ilimradi tu akubali kuachia ubunge wake katika Jimbo la Karatu.

Kwake ni taifa kwanza

Kitendo chake cha kueleza kuwa alitumia sehemu kubwa ya mshahara wake kumpa mkewe ili afanye ziara ya kuzunguka nchi nzima katika harakati za kukijenga chama, ni kielelezo kuwa kiongozi huyo anajali ustawi wa taifa kwa namna anavyoamini kuliko maisha binafsi ya familia yake.

"Slaa amekuwa akitanguliza masilahi ya taifa kwenye siasa zake, kama mtu anakubali yeye na familia yake wale mihogo na maharage ili kipato chao kitumike kwenye mambo ya siasa, unadhani ana uchungu kiasi gani na taifa hili?" alihoji Mama Saidi wa Mwananyamala jijini Dar.

Kuweka maisha yake rehani

Kitu kingine kinachofanya wananchi wengi kumuona Dk. Slaa kuwa ni shujaa wao ni kitendo chake cha kukubali kuweka maisha yake rehani, ilimradi tu mambo makubwa na muhimu ya nchi yanasemwa hadharani na kila mmoja ayasikie.
"Ni nani atakuwa tayari kufa kwa kuwataja watu majina kwenye uovu, tena watu hao ni vigogo wenye fedha na mamlaka ambao wanaweza kumfanya lolote. Fikiria kitendo chake cha kutaja majina ya mafisadi papa wakati ule. Huu ni ujasiri wa aina yake," alisema Liffa Jason, mwenyeji wa Shinganya aliye Dar kibiashara.Walisema Dk. Slaa alifanya hivyo akijua yeye binafsi hafaidiki na lolote, lakini aliweza kuwataja ili kuwafunua wananchi wawajue watu wanaoitafuna nchi yao.

Hana tamaa

Kingine kilichoelezwa na watu hao ni kwamba kiongozi huyo hana tamaa ya fedha wala madaraka, kwani alikubali kuacha ubunge, wenye mshahara na marupurupu mengi na kwenda kufanya kazi ya kukijenga chama, kitu ambacho alifanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Lakini kikubwa zaidi, wamedai kwamba Dk. Slaa angeweza kunyamaza kimya na kufanya kazi ya kumnadi Lowassa, kwani kwa vyovyote mwisho wa siku angepata kuteuliwa katika nafasi kubwa na nyeti serikalini.
"Kiukweli hana tamaa, naamini angekaa kimya na ukatibu mkuu wake wa chama, bado maisha yake yangekuwa mazuri, kaamua kujiweka pembeni bila kujali athari atakayoipata ili tu asikumbatie mafisadi ndani ya Chadema," anasema Elika wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Apewe ulinzi

Kwa kuzingatia mambo yote yanayoendelea katika maisha yake ya kisiasa, wananchi waliozungumza suala hili walitaka kiongozi huyo, kwani kazi yake kubwa kwa nchi inawakera watu wachache wanaoweza kumdhuru kwa namna yoyote.
"Unajua tangu siku alipoongea na kuwalipua viongozi wa Ukawa, ni lazima kutakuwa na vitisho, wengine wamemtukana na kudai kajidhalilisha, lakini ukweli unabaki palepale kuwa yeye ni shujaa na anastahili ulinzi ili wasitokee wa kumdhuru," alisema Modesta George wa Oysterbay jijini Dar na kuongeza:

"Lakini pia kwa kila mwenye mapenzi na nchi ya Tanzania, anayechukia ufisadi, rushwa na uonevu ndani ya vyama vya siasa anayeona kuwa alichokifanya Slaa ni kitendo cha kishujaa, tuungane kumuombea ili Mungu amuepeshe na balaa."

Aibomoa VIBAYA Ukawa, aacha majeraha

Kitendo chake cha kutoa maneno makali kwa viongozi wenzake wa Chadema na Ukawa, kimesababisha majeraha kwa umoja huo, kwani viongozi sasa wamegawanyika juu ya nani ni mkweli kati ya yanayosemwa kuhusiana na sakata zima la Dk. Slaa.
"Dk. Slaa ametuacha njia panda, sasa kama yeye alikataa kumkaribisha fisadi bila kutimiza masharti, lakini wenzake wakafanya ina maana sisi sasa tushike lipi?" alihoji Bruno Kei wa Tegeta Kibaoni.
 
Hakuna kitu hapo! Shujaa wenu nyie mliomwandalia madesa na wala usimlinganishe na Mwalimu kwani Mwalimu ni level nyingine kabisa. Mnajifariji na Babu yenu mla mihogo, mliyemlipia airtime za Radio na TV, lakini sisi malofa hatuangalii makunyanzi. Mambo yote 25 oktoba!
 
Wewe nguberi la kiume unajipa Id na Avatar za kike sijui kwanini au umenogewa na mpini?
 
Naona watu wamesusia uzi wako teh teh teh!Hii ni dalili tosha kuwa hakuna aliyeachwa njia panda ila kila mtu kasombwa na mafuriko!
Mlitegemea press itayumbisha ukawa lakini ndio inazidi kuwajenga,sasa mmepanic mmemuandalia tena kipindi dr star tv akajaribu tena kulikoroga!
Lowasaaaaaaaaa mabadilikoooooo*2 lowasaaaaa
 
Sasa napata shaka na ile hotuba ya dr nilikuwa naifikiria sana,lakini baada ya kuona ccm wenzangu wameikomalia sasa naamini kuna kitu nyuma ya dr.
 
Dr Slaa anawahenyesha UKAWA ile mbaya. Sas wamebaki kubwabwaja tu. hakuna mwenye uwezo wa kujibu hoja zake

sasa tutamjibu vp wakati tushasombwa na mafuriko?Ndege ishapaa,naona mmeona hakuna impact mpaka mnakodi vijana kuaminisha watu kuwa wamemuunga mkono dr teh teh,jaman kumuunga mkono dr ni kujiunga na CCM!
Mmekwama ndio maana mnamuandalia vipindi kwenye luninga ili ajaribu kukoroga zaidi!
Hamjui mkizidi kumponda watu ndio wanazidi kumkubali!
 
dr slaa anawahenyesha ukawa ile mbaya. Sas wamebaki kubwabwaja tu. Hakuna mwenye uwezo wa kujibu hoja zake

dr yupi mla miyogo akamalizane na mke wake kwanza mzee amri ya sita ilimshinda atawezaje kufanana na nyerere!
 
Dr Slaa yupi awe shujaa? Huyu haramia alotelekeza mke na watoto na kwenda kuishi na malaya au mwingine. Ushujaa wake kwa kununuliwa?
 
Tena Naomba mtoa Mada asidhubutu kumfananisha hata kidogo slaa na baba wa Taifa la Tanzania. Najua akija leo kwa kweli atalia machozi jinsi CCM ilivyoharibu nchi
 
Slaa amekuwa shujaa Wa wana Lumumba na chimwaga na amegeuka msaliti Wa wana mabadiliko
 
Msimamo wa Slaa ni msimamo wa NYERERE

NYERERE hakuwa muongo
eti kuna contena la makaratasi ya kura lipo Tunduma, alitaka kuiingiza nchi kwenye vita kabisa, kufungua contena hakuna kitu

ndio umfananishe na Nyerere huyo
 
HOTUBA ya kwanza tangu ‘atoweke’ kwenye anga za siasa ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dokta Wilbroad Slaa, aliyoitoa juzi Jumanne juu ya kujiweka pembeni, imepokelewa kwa hisia tofauti huku wengi wakimuita kuwa ni shujaa wa taifa kutokana na ujasiri wake.

Katika mahojiano yaliyowahusisha wananchi na wachambuzi mbalimbali wa mambo ya kisiasa kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mara baada ya kiongozi huyo kukutana na waandishi wa habari, walisema kuwa, Dokta Slaa ni mtu wa aina yake ambaye taifa halijapata kuwa naye tangu kuondoka kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Wengi walionesha kufurahishwa na misimamo ya kiongozi huyo tangu ajiingize kwenye masuala ya siasa, kwani siku zote amekuwa mstari wa mbele kuwatetea wanyonge, kuanika maovu na kukemea kila analoliona lipo tofauti na anavyoamini.
“Kwa kweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Dk. Slaa ni kati ya viongozi wenye msimamo asiyekubali kuyumbishwa. Amekuwa hivyo tangu nilivyomjua na hata hotuba yake aliyoitoa juzi, inadhihirisha hilo,” alisema Chande Juma wa Kinondoni jijini Dar.

Alisema kama mtu alifuatilia vizuri mazungumzo yake, ni wazi kuwa viongozi wenzake walikubali kubadili msimamo ili kumwezesha Lowassa aingie Chadema, lakini yeye akakataa licha ya kamati ndogo kuundwa ili imshawishi alegeze msimamo.

Mchambuzi mmoja wa habari za siasa aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema siku zote anamtambua Dk. Slaa kama mtu mwenye kuichukia rushwa, kwani anaamini hicho ndicho chanzo cha matatizo yote yanayosababisha kero za wananchi kutoisha, licha ya nchi kuwa na rasilimali za kutosha.

“Unampata wapi sasa hivi aina ya kiongozi ambaye anaweza kukataa rushwa ya shilingi milioni 500 akitetea masilahi ya wananchi masikini? Viongozi wetu wa sasa kila mtu anaweka mbele masilahi yake na familia yake, suala la kuwatetea wanyonge wanalifanya kama maigizo tu,” alisema mchambuzi huyo, akikumbushia jinsi mbunge huyo wa zamani wa Karatu alivyokataa kiasi hicho cha fedha ili ashiriki kuzuia ripoti ya Kamati ya Bunge juu ya sakata la Richmond isisomwe bungeni.

Maneno kama hayo yalisemwa pia na mkazi mmoja wa Sinza, Nicholaus John akirejea jinsi alivyokataa rushwa ya uongozi pale alipoahidiwa kazi nje ya nchi, ilimradi tu akubali kuachia ubunge wake katika Jimbo la Karatu.

Kwake ni taifa kwanza

Kitendo chake cha kueleza kuwa alitumia sehemu kubwa ya mshahara wake kumpa mkewe ili afanye ziara ya kuzunguka nchi nzima katika harakati za kukijenga chama, ni kielelezo kuwa kiongozi huyo anajali ustawi wa taifa kwa namna anavyoamini kuliko maisha binafsi ya familia yake.

“Slaa amekuwa akitanguliza masilahi ya taifa kwenye siasa zake, kama mtu anakubali yeye na familia yake wale mihogo na maharage ili kipato chao kitumike kwenye mambo ya siasa, unadhani ana uchungu kiasi gani na taifa hili?” alihoji Mama Saidi wa Mwananyamala jijini Dar.

Kuweka maisha yake rehani

Kitu kingine kinachofanya wananchi wengi kumuona Dk. Slaa kuwa ni shujaa wao ni kitendo chake cha kukubali kuweka maisha yake rehani, ilimradi tu mambo makubwa na muhimu ya nchi yanasemwa hadharani na kila mmoja ayasikie.
“Ni nani atakuwa tayari kufa kwa kuwataja watu majina kwenye uovu, tena watu hao ni vigogo wenye fedha na mamlaka ambao wanaweza kumfanya lolote. Fikiria kitendo chake cha kutaja majina ya mafisadi papa wakati ule. Huu ni ujasiri wa aina yake,” alisema Liffa Jason, mwenyeji wa Shinganya aliye Dar kibiashara.Walisema Dk. Slaa alifanya hivyo akijua yeye binafsi hafaidiki na lolote, lakini aliweza kuwataja ili kuwafunua wananchi wawajue watu wanaoitafuna nchi yao.

Hana tamaa

Kingine kilichoelezwa na watu hao ni kwamba kiongozi huyo hana tamaa ya fedha wala madaraka, kwani alikubali kuacha ubunge, wenye mshahara na marupurupu mengi na kwenda kufanya kazi ya kukijenga chama, kitu ambacho alifanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Lakini kikubwa zaidi, wamedai kwamba Dk. Slaa angeweza kunyamaza kimya na kufanya kazi ya kumnadi Lowassa, kwani kwa vyovyote mwisho wa siku angepata kuteuliwa katika nafasi kubwa na nyeti serikalini.
“Kiukweli hana tamaa, naamini angekaa kimya na ukatibu mkuu wake wa chama, bado maisha yake yangekuwa mazuri, kaamua kujiweka pembeni bila kujali athari atakayoipata ili tu asikumbatie mafisadi ndani ya Chadema,” anasema Elika wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Apewe ulinzi

Kwa kuzingatia mambo yote yanayoendelea katika maisha yake ya kisiasa, wananchi waliozungumza suala hili walitaka kiongozi huyo, kwani kazi yake kubwa kwa nchi inawakera watu wachache wanaoweza kumdhuru kwa namna yoyote.
“Unajua tangu siku alipoongea na kuwalipua viongozi wa Ukawa, ni lazima kutakuwa na vitisho, wengine wamemtukana na kudai kajidhalilisha, lakini ukweli unabaki palepale kuwa yeye ni shujaa na anastahili ulinzi ili wasitokee wa kumdhuru,” alisema Modesta George wa Oysterbay jijini Dar na kuongeza:

“Lakini pia kwa kila mwenye mapenzi na nchi ya Tanzania, anayechukia ufisadi, rushwa na uonevu ndani ya vyama vya siasa anayeona kuwa alichokifanya Slaa ni kitendo cha kishujaa, tuungane kumuombea ili Mungu amuepeshe na balaa.”

Aibomoa VIBAYA Ukawa, aacha majeraha

Kitendo chake cha kutoa maneno makali kwa viongozi wenzake wa Chadema na Ukawa, kimesababisha majeraha kwa umoja huo, kwani viongozi sasa wamegawanyika juu ya nani ni mkweli kati ya yanayosemwa kuhusiana na sakata zima la Dk. Slaa.
“Dk. Slaa ametuacha njia panda, sasa kama yeye alikataa kumkaribisha fisadi bila kutimiza masharti, lakini wenzake wakafanya ina maana sisi sasa tushike lipi?” alihoji Bruno Kei wa Tegeta Kibaoni.

Shujaaa wa lumumba
 
imekuwaje leo mnasema msimamo wa slaa ni msimamo wa nyerere? wakati ndo nyie mlompachika majina ya ovyo kusema ni mzushi na mropokaji mkaenda mbali zaidi mkasema padri mzinifu...cha ajabu zaidi mmefurahi alipomkandia lowassa tu ila aliposema ccm ni sawa na choo cha mavi chenye vinyesi ni kama hamkumsikia vile....mbona mda upo ghafla atarudi kwenye choo chake cha mavi....!
 
mtoa uzi ungejaribu kuongeza idadi ya watu uliowahoji maana umetia chumvi mno kwa kuhoji watu ambao hata 10 hawajafika....ungejaribu kumhoji slaa kuhusu tuhuma alizomtoleaga magufuli ambae nae ni mgombea urais....mnavyozidi kuyarudia ya slaa ndo mnazidi kuidimiza ccm....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom