Hot Lady
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 1,035
- 638
Nimetafakari sana jinsi anavyoteseka Julius Mtatiro. Nimetafakari sana jinsi Lowasa na Juma Duni Haji wanavyopitia wakati mgumu. Natafakari sana jinsi Zitto Kabwe anavyotamani kuwa kwenye chama kikubwa cha siasa. Natafakari sana jinsi Dr Slaa anavyotamani kurejea CCM. Natafakari sana jinsi David Kafulila, Moses Machali na Felix Mkosamali walivyopotea kisiasa. Natafakari sana hakika siishi kutafakari.
Kuna wanasiasa wamehama vyama kwa lengo la kutafuta madaraka na vyeo baada ya kuvikosa kwenye vyama vyao. Hata hivyo, ni wachache tu wamefanikiwa kung'ara huko walikoenda. Wanatamani kurejea kwenye chama chao ambacho hakika kinafanya vizuri lakini wanakumbana na vikwazo.
Ndipo nikafikia hatua ya kupendekeza kuwa tuwe na sheria inayoruhusu wanasiasa kutolewa kwa mkopo ili wakahoreshe viwango vyao na baada ya hapo kama chama kilichomchukua mwanasiasa wa mkopo kikaridhishwa na kiwango cha mwanasiasa huyo, asi kuwe na makubaliano rasmi baina ya vyama hivyo ili mwanasiasa huyo aweze kuuzwa kama wanavyofanya kwenye Soka. Likifanyika hili litanoresha sana mfumo wa siasa za nchi. Siasa sasa hazitakuwa uadui bali ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.
Pia, ikitokea mwanasiasa aliyeuzwa baada ya kutolewa kwa mkopo akauzwa na chama chake kipya kwenda chama kingine, basi chama kilichomlea kipate asilimia ya mauzo ya mwanasiasa huyo. Ni kama Mbwana Samatt alipouzwa na Simba TP Mazembe ambayo nayo inamuuza huko Ubelgiji. Kwa siasa iwe hivyo. Mathalan, Julius Mtatiro anaweza kutolewa kwa Mkopo kwenda NCCR ama CHADEMA. Kama vyama hivyo vitamuhitaji, basi vinaweza kumnunua. Na kama chama kingine kitamhitaji mwanasiasa huyo, basi chama chake cha awali yaani CUF kinufaike na mauzo ya Mtatiro
Ni mawazo tu hayo. Nilikuwa natafakari nikaona ni bora tutafakari kwa pamoja wana social media