Nawaza kwa sauti juu ya hatma ya Edward Lowasa

Hot Lady

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
1,035
638
  1. Nawaza kwa kina sijui vile vicoba vilivyokuwa vinafadhiliwa na Lowasa vitaendelea kupata mgawo. Nawaza tu
  2. Nawaza kwa sauti sijui zile helkopta alizokuwa anakodi Lowasa kwenye trip zake za kisiasa zitaendelea kutumika. Nawaza tu
  3. Nawaza kwa kina sijui kama Lowasa ataendelea kuchangia ujenzi wa nyumba za ibada. Sijui labda wenzangu mtanisaidia
  4. Nawaza kwa kina sijui kama wale masheikh na mapadre walio kwenye payroll ya Lowasa wataendelea kuoata mgawo wa kila mwezi. Nawaza tu wadau.
  5. Nawaza kwa kirefu zijui wale maafisa wa serikali aliowaajiri Lowasa na kuwalipa mishahara wataendelea kunufaika na ajira zao hizo. Nawaza tu
  6. Nawaza kwa sauti kubwa kama Apson Mwang'onda ataendelea kuwa mshauri mkuu wa Lowasa. Nawaza tu
  7. Nawaza kwa kina kama Kingunge Ngombare Mwiru ataendelea kuitisha press conference kuisema CCM. Sijui mie nawaza tu
  8. Nawaza kwa upana kama zile Redio, TV na Magazeti ya Rostam, Reginald Mengi na Ruge vitaendelea kumpamba na kumpa air time ya kutosha Lowasa. Nawaza tu jamani.
  9. Nawaza kwa kina sijui wale vijana wa bodaboda waliokuwa wanapewa mgawo wa mafuta kila wiki na Lowasa wataendelea kunufaika
  10. Nawaza kwa kina sijui yale ma Yutong yaliyorembwa kwa rangi za njano na kijani huku yakiwa na maandishi ya safari ya matumaini na picha za Lowasa yataendelea kuwa hivyo. Nawaza tu wadau.
  11. Nawaza kwa kina siju wale wenyeviti wa mikoa na wilaya wa CCM walioasi chama na kumtumikia Lowasa wataendelea kubaki hivyo. Najua wengine wamesharudi kundini ila sina hakika kama wale wengine wapo hivyo. Nawaza tu wadau.
  12. wadau naendelea kuwaza na nyie mtanisaidia pia mpaka tupate majibu
 
Back
Top Bottom