WIKIPEDIA wamkaanga Edward Lowassa, sijui ataponea wapi huyu bana

Hot Lady

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
1,035
638
Kaka zangu, hebu pakueni wenyewe muone jinsi wenzetu wazungu walivyoandika historia ya Edward Lowasa. Hakika inahuzunisha na inasikitisha. Nilijua haya mambo anasingiziwa kumbe hata wenzetu wazungu wanamuona vivyo hivyo. Kwa ujumla wake Lowasa ni fisadi na mtumiaji vibaya wa madaraka


Edward Ngoyai Lowassa
Edward Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26 Agosti 1953) ni mwanasiasa nchini Tanzania.

Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kumi wa nchi hiyo tarehe 30 Desemba 2005 akajiuzulu tarehe 7 Februari 2008 kwa kutajwa katika kamati ya bunge ya uchunguzi katika utoaji wa tenda kwa kampuni ya umeme ya Richmond kutokana na uzembe wa watendaji walio chini yake.

Maisha
Lowassa ni mwenyeji na alikuwa mbunge wa Monduli katika Mkoa wa Arusha.
Alisoma shahada ya kwanza katika mada ya tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu shahada ya pili katika sayansi ya maendeleo ya jamii kwenye Chuo Kikuu cha Hull nchini (Uingereza).
Mnamo tarehe 28 Julai 2015 alijunga rasmi na chama cha upinzani cha CHADEMA. Hiyo ni baada ya kukatwa jina lake katika kinyang'anyiro cha Urais kupitia chama tawala cha Chama cha Mapinduzi.
Siku chache baadaye aliteuliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA mnamo Oktoba 2015.

Nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika
Lowassa ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu mbalimbali katika siasa za nchini Tanzania, kwa kuwa aliwahi kushika vyeo mbalimbali katika serikali kama vile:

  • Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhidi ya umaskini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000)
  • Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989-1990)
  • Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993)
  • Mbunge wa Monduli tangu 1990

Sakata la Richmond
Sakata la Richmond lilianza kwa kuunda tume ya kuchunguza mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura: tume hiyo ilidai kampuni ya Richmond ilikuwa kampuni ya mfukoni, jambo ambalo inawezekana lina ukweli, maana hata kabla ya tume kuundwa Lowassa alipata shaka na kampuni hiyo pale iliposuasua kutekeleza mradi akawa ameshauri mkataba na kampuni hiyo uvunjwe, lakini ushauri wa mtaalamu na wanasheria ulitaka serikali ivumilie.

Tume ilidai viongozi wa serikali wa wizara husika na Waziri Mkuu walikuwa wakihimiza Tanesco kukamilisha mchakato wa kumpata mzabuni haraka, jambo ambalo hakikuwakosha, maana ni jambo ambalo lilikuwa kwenye mujibu wao kuona nchi haiingii gizani kwa manufaa ya kiuchumi na ya kiusalama. Pia kwa umuhimu wa umeme kiuchumi na kiusalama suala la kupata mitambo ya kufua umeme wa dharura lililozungumzwa na kupata vikao vyote muhimu vya serikali ngazi ya Taifa likiwemo baraza la mawaziri.

Sinema zaidi ya kisiasa ilikuja kubainika katika mambo makubwa matatu. Kwanza ni kumtaka Waziri Mkuu apime na kuwajibika katika jambo ambalo halibainishi kosa lolote kwake, kiutawala wala kisiasa. Pili mabishano ya wanasiasa juu ya kutumia au kutoendelea kutumia mitambo ya DOWANS. Tatu mabishano ya wanasiasa juu ya kulipa au kutolipa kampuni ya DOWANS.

Ili kulinda heshima ya serikali nzima na chama tawala CCM, na pia ili kuepuka mgawanyiko miongoni mwa wanachama, wananchi na viongozi, Lowassa aliamua kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu.

Wabunge wa CCM waliokutana kama kamati kuzungumza suala hilo zaidi ya asilimia 80 walitaka Waziri Mkuu Lowassa asijiuzulu kwa kuwa hausiki na chochote. Upande wa kamati ya bunge, mwenyekiti wa kamati hiyo Harrison Mwakyembe, mnamo tarehe 15 February 2008 alikiri kuwa, Edward Lowassa alijiuzulu kwa makosa ya watendaji wa chini yake.

Kuhusu hoja ya kulipwa DOWANS na kuendelea kutumika kwa mitambo ambayo ililetwa na DOWANS, jambo hilO lilikwenda kwenye mabaraza ya kimataifa na kuonekana wana haki ya kulipwa na mitambo iliyodaiwa na wanasiasa kuwa haifai ndiyo inayoendelea mpaka leo kufua umeme. Rais wa Marekani Baraka Obama katika ziara yake nchini aliitembelea na kusema ni mmoja kati ya mitambo bora katika bara la Afrika.

Uchaguzi mkuu 1995
Mwaka 1995 Edward Lowassa aliamua kuingia katika mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM. Wakati huo Lowassa aliombwa na Umoja wa Vijana kupitia kikao cha baraza kuu la Taifa achukue fomu akiwa miongoni mwa wana CCM wanne ambao vijana waliamini wataweza kulisaidia Taifa kupiga hatua za haraka kuelekea maendeleo endelevu, wengine waliokuwa wametajwa na Umoja wa vijana ni Salim Ahmed Salim, Laurance Gama na jaji mstaafu Mark Bomani.

Katika hatua ya kuchagua majina 3 kati ya majina 11 yaliyoomba nafasi hiyo, Lowassa akawa hakupendekezwa, lakini hakununa wala kususa bali aliamini kuwa mwanamapinduzi mwenzie Jakaya Mrisho Kikwete ataweza kutekeleza dhamira aliyokuwa nayo ya kuwaletea Watanzania maendeleo, hivyo alirudi kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana wa CCM ambao walihoji kwa nini ameenguliwa, na yeye kwa utii mkubwa kwa CCM aliwataka vijana na viongozi wengine waheshimu maamuzi ya chama na kumuunga mkono Kikwete. Ikumbukwe kuwa mwana-CCM mwingine aliyekuwa anakubalika kwa umma Lowassa aliondoka mapema CCM kwa sababu ndogo tu ya kubadilishiwa wizara na kuamua kwenda chama cha NCCR mageuzi ambako aligombea uraisi kwa chama hicho na kuleta upinzani mkubwa.

Yapo maneno ya baadhi ya wanasiasa kwamba kutoteuliwa kugombea kwa Lowassa kulitokana na kuonekana anamiliki fedha nyingi akiwa na muda mfupi kwenye utumishi wa umma, lakini pia inasemekana kuwa wale waliohoji kukatwa kwa jina lake kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Taifa, majibu yalikuwa, CCM iliamua kupeleka majina matatu kwenye mkutano mkuu ili wachague moja katika uwakilishi huo wa majina: walipenda apatikane mtu mzima mmoja, mwenye umri wa kati mmoja na kijana mmoja, watu hao ni mzee David Msuya ambae ni mtu mzima, Benjamini Mkapa ambae umri wake ulikuwa wa kati na kijana ambae ni Jakaya Kikwete.

Lakini maneno hayo ya baadhi ya wanasiasa hayakuishia hapo: wakadai baada ya Rais Mkapa kuchaguliwa, hakumteua Lowassa kwa kuwa aliagizwa na Mwalimu Nyerere asimteue mpaka achunguzwe kama uwezo kiasi wa fedha alionao unatokana na mapato halali, kama siyo halali asimteue. Mwaka 1997 Rais Mkapa akamteua Lowassa kuwa Waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa Rais mazingira. Maneno hayo ya baadhi ya wanasiasa ni ya ukweli basi uchaguzi ulifanyika na kuonekana mapato yake ni halali au vinginevyo unaweza kusema ni hisia za kimazingira.

CHANZO: Wikipedia
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    91 KB · Views: 12,268
  • image.jpg
    image.jpg
    98.8 KB · Views: 7,715
  • image.jpg
    image.jpg
    113 KB · Views: 7,295
  • image.jpg
    image.jpg
    109.1 KB · Views: 7,057
  • image.jpg
    image.jpg
    93.7 KB · Views: 6,665
  • image.jpg
    image.jpg
    73.7 KB · Views: 6,584
Kaka zangu, hebu pakueni wenyewe muone jinsi wenzetu wazungu walivyoandika historia ya Edward Lowasa. Hakika inahuzunisha na inasikitisha. Nilijua haya mambo anasingiziwa kumbe hata wenzetu wazungu wanamuona vivyo hivyo. Kwa ujumla wake Lowasa ni fisadi na mtumiaji vibaya wa madaraka
View attachment 275620View attachment 275621View attachment 275622View attachment 275623View attachment 275624View attachment 275625

https://sw.wikipedia.org/wiki/Edward_Ngoyai_Lowassa

Copy and Paste hiyo habari
 
Kwani wao ndiyo wanamchagua?Walishindwa na Kenyatta.Watanzania ndiyo wenye hakinya kuamua Fisadi yupi awaongoze Magufuli au Lowassa na si mzungu wa kabila yoyote ile.
 
  • Thanks
Reactions: bht
Kama unaamini mambo ya wikipedia utakuwa mburula kwa maisha yako yote, huko ni suala la mitazamo, uwongo na uzandiki mkubwa. Never trust wikipedia always
 
Wazungu ndyo nan?.. Akili za kuambiwa changanya na zako mtaangaika sanaaa lkn mwaka huu lazma mkaeeeeed vivaa ukawaaaaa
 
Hata ukitaka kumsifia mchepuko wako kwa shughuli zake unaweza kumweka Wikipedia.
Huo ni sawa na ukurasa wa facebook ukiwa na account unakukuluka utakavyo.
 
[h=1]Edward Ngoyai Lowassa[/h]
Edward Ngoyai Lowassa
Mbunge
Bunge laTanzania
Jimbo la uchaguziMonduli (Arusha)
Tarehe ya kuzaliwa26 Agosti 1953
ChamaCHADEMA (tangu 28/07/15)
Tar. ya kuingia bungetangu 1990
Alirudishwa mwaka2005
Waziri Mkuu wa Tanzania
Alingia ofisini2005
Alitanguliwa naFrederick Sumaye
DiniMkristo
Elimu yakeChuo Kikuu
Digrii anazoshikaMA (Development Studies) University of Bath (Uing.)
Kazimwanasiasa
Edward Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26 Agosti 1953) ni mwanasiasa nchini Tanzania.
Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kumi wa nchi hiyo tarehe 30 Desemba 2005 akalazimishwa kujiuzulu tarehe 7 Februari 2008 kwa kuhusika kwake na utoaji wa tenda kwa kampuni ya umeme ya Richmond ambapo yeye alihusika moja kwa moja na upatikanaji wa kampuni hiyo ambayo ilikuja kubainika kuwa ni kampuni hewa
[h=2]Yaliyomo[/h]




[h=2]Maisha[/h] Lowassa ni mwenyeji na alikuwa mbunge wa Monduli katika Mkoa wa Arusha.
Alisoma shahada ya kwanza katika mada ya tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu shahada ya pili katika sayansi ya maendeleo ya jamii kwenye Chuo Kikuu cha Hull nchini (Uingereza).
Mnamo tarehe 28 Julai 2015 alijunga rasmi na chama cha upinzani cha CHADEMA. Hiyo ni baada ya kukatwa jina lake katika kinyang'anyiro cha Urais kupitia chama tawala cha Chama cha Mapinduzi. CCM walilazimika kukata jina lake kutokana na mwanasiasa huyo kukumbwa na kashfa nyingi za kifisadi ikiwa ni pamoja na kashfa ya Richmond pamoja na kutoa rushwa kwa wajumbe wa vyombo vya maamuzi ndani ya chama kama NEC, Kamati Kuu na Mkutano Mkuu
Siku chache baadaye aliteuliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA mnamo Oktoba 2015.
[h=2]Nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika[/h] Lowassa ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu mbalimbali katika siasa za nchini Tanzania, kwa kuwa aliwahi kushika vyeo mbalimbali katika serikali kama vile:

  • Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhidi ya umaskini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000)
  • Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989-1990)
  • Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993)
  • Mbunge wa Monduli tangu 1990
[h=3]Waziri wa ardhi na makazi (1993-1995)[/h] Akiwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Mijini, Lowasa alitumia fursa hiyo kujitwalia na kujimilikisha viwanja kadhaa kwa manufaa yake na maswahiba wake. Lowasa anamiliki ranchi kubwa kabisa ambazo awali zilikuwa chini Ranchi ya Taifa na kuwa mikononi mwake. Lowasa anamiliki maeneo mengi huko Monduli Arusha na maeneo mengi ya mikoa ya Arusha na Manyara. Pia Lowasa anamiliki viwanja kadhaa ndani ya miji mikubwa ambapo amejenga majumba kadhaa ya kifahari na nyumba za kulala wageni. Chanzo cha fedha alizotumia kujenga majengo hayo bado kingali kujulikana
[h=3]Waziri wa Maji na Mifugo (2000-2005)[/h] Miaka 2000–2005 Edward Ngoyai Lowassa alikuwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo. Aliitumia nafasi hiyo kwa upendeleo mkubwa ambapo miradi mingi ya maji aliielekeza kwenye jimbo lake. Alihakikisha kuwa jimbo lake na mikoa ya kaskazini na hasa Arusha na Kilimanjaro inatengewa bajeti kubwa. Pia Lowasa alitumia fursa hiyo kuhamisha miradi ya maji kutoka maeneo mengine ya nchi na kupeleka jimboni kwake Monduli
[h=3]Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2005-2008)[/h] Tarehe 29 Desemba 2005 Lowassa aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Baada ya kula kiapo cha kutumikia nafasi hiyo, Lowasa alianza kupanga mikakati ya kuliibia taifa. Miongoni mwa mikakati hiyo ni kushirikiana na wataalam ili kutumia mikataba ya serikali kuwaibia wananchi. Lowasa alitumia vema fursa zilizokuwa zinajitokeza kwa manufaa yake. Fursa hizo ni pamoja na ukame na ukosefu wa umeme. Ili kukabiliana na ukame, Lowasa alikuja na mkakati wa kuagiza mvua ya kutengeneza toka Thailand. Hata hivyo, mradi huo haukuweza kutekeleza baada ya kulazimishwa kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu.
Pia Lowasa alitumia vema tatizo la ukosefu wa umeme. Ndipo Lowasa alipojiingiza kwenye kashfa ya Richmond ambapo alitishia kuwa nchi itakuwa gizani na kwamba ni lazima ipatikane kampuni ya kufua umeme wa dharura. Ndipo yeye akajifanya kuwa ni mtaalam ambapo alikuwa anaingilia majukumu ya wataalam wake. Ijapokuwa kulikuwa na makampuni mengi yenye sifa, kwa ushawishi wake, Lowasa akalazimisha ipewe kampuni ya Richmond ambayo baadaye ilikuja kugundulika kuwa ilikuwa ni kampuni ya mfukoni.
Kutokana na kadhia hiyo, Bunge lililazimima kuunda kamati Teule chini ya Mbunge wa Kyela, Dr Harrison Mwakyembe ili kufanya uchunguzi wa kampuni hiyo tata. Hatimaye Kamati ikawasilisha maoni yake Bungeni ambayo yalimfanya Lowasa asiwe na hadhi ya kuendelea kuwa Waziri Mkuu
MWAKYEMBE AMWAGA LAZI BUNGENI
MH. HARRISON MWAKYEMBE
MBUNGE WA KYELA NA MWENYEKITI WA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA MADUDU YA KAMPUNI YA RICHMOND, MH. HARRISON MWAKYEMBE, ALISOMA MBELE YA BUNGE RIPOTI YA KAMATI YAKE KWA UWAZI NA UKWELI KWA MUDA WA DAKIKA TAKRIBAN 80.
KAMATI TEULI HIYO IMEBAINI KWAMBA MKATABA WA RICHMOND ULIFIKIWA KWA UPENDELEO, RUSHWA NA UBABE WA VIONGOZI WAANDAMIZI SERIKALINI, NA KWAMBA LICHA YA USHAURI WA KITAALAMU NA HALI HALISI WAKUBWA WALILAZIMISHA USAINIWE. hIVYO PAMOJA NA MAMBO MENGINE KIBAO IMEPENDEKEZA MIKATABA YOTE YA NISHATI IPITIWE UPYA KAMA ILIVYO MIKATABA YA MADINI
KAMATI TEULE HIYO KUPITIA MDOMO WA MH. MWAKYEMBE IMETO MAPENDEKEZO KAMA 15 HIVI, BAADHI YAKE YAKIWA:
1. WAZIRI HUSIKA WA WAKATI HUO (MH. DR MSABAHA) NA KATIBU MKUU WAKE WAKATI HUO WAPEWE ADHABU KALI
2. WAZIRI WA SASA WA NISHATI NA MADINI MH. NIZAR KARAMAGI NA MWANASHERIA MKUU WAWAJIBISHWE KWA KUWEZESHA MKATABA WA RICHMOND KUHAMISHIWA KAMPUNI INGINE
3. UONGOZI WA TAKURU (SASA TAKUKURU) UFANYIWE MABADILIKO HARAKA KWA KILICHODAIWA KUTOA TATHMINI ISIYO SAHIHI JUU YA MAZINGIRA YALIYOUZUNGUKA MKATABA WA RICHMON.
4. MKATABA WA RICHMOND AMBAYO IMEIPASIA KAMPUNI YA DOWANS UCHUNGUZWE UPYA.
5. MSIMAMIZI MKUU WA SERIKALI AMBAYE NI WAZIRI MKUU ATUMIE BUSARA ZAKE KUAMUA NINI CHA KUFANYA BAADA YA RIPOTI KUANIKWA HADHARANI
AIDHA JUHUDI ZINAFANYIKA KUIPATA RIPOTI YOTE HIYO NA KUANGALIA NAMNA YA KUWEKA HADHARANI ILI HADHIRA IJUE KILA KITU KWA UWAZI NA UKWELI.
PSSST! SASA TUNASUBIRI RIPOTI YA MADINI YA KINA KABWE
[h=2]Uchaguzi mkuu 1995[/h] Mwaka 1995, Lowasa aliamua kuingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, Lowasa hakufanikiwa kupenya kwenye tano bora kati ya majina 11 yaliyojitokeza kuwania nafasi hiyo ambapo Benjamin Mkapa aliibuka kidedea.
Sababu za Lowasa kutopenya kwenye tano bora zilitolewa ndani ya Kamati Kuu ambapo moja ya sababu ni kutokuwa mwadilifu. Uadilifu ni dhana pana ambapo inajumuisha na kujihusisha kwake na kashfa mbalimbali za ufisadi. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitoa sababu za Lowasa kuondolewa licha ya kwamba alikuwa na wapambe wengi ambao baadaye ilikuja kubainika kuwa alikuwa amewahonga
 
Kaka zangu, hebu pakueni wenyewe muone jinsi wenzetu wazungu walivyoandika historia ya Edward Lowasa. Hakika inahuzunisha na inasikitisha. Nilijua haya mambo anasingiziwa kumbe hata wenzetu wazungu wanamuona vivyo hivyo. Kwa ujumla wake Lowasa ni fisadi na mtumiaji vibaya wa madaraka
View attachment 275620View attachment 275621View attachment 275622View attachment 275623View attachment 275624View attachment 275625

https://sw.wikipedia.org/wiki/Edward_Ngoyai_Lowassa

Wikipedia can be edited.
Inawezekana ni wewe ndio ulioedit.
 
kaka zangu, hebu pakueni wenyewe muone jinsi wenzetu wazungu walivyoandika historia ya edward lowasa. Hakika inahuzunisha na inasikitisha. Nilijua haya mambo anasingiziwa kumbe hata wenzetu wazungu wanamuona vivyo hivyo. Kwa ujumla wake lowasa ni fisadi na mtumiaji vibaya wa madaraka
View attachment 275620View attachment 275621View attachment 275622View attachment 275623View attachment 275624View attachment 275625

https://sw.wikipedia.org/wiki/edward_ngoyai_lowassa


wazungu wanamuogopa lowasa akiingia biashara zao zote -mikataba inakuwa reviewed ndio maana wameanza propaganda
 
Back
Top Bottom