Ok... nilikuwa nimechoka....Duh !, ikawaje mh.
Ujue Kuna watu wanachukulia poa haya mambo. Wewe ndugu naona kuuliza kwako kulikukusaidia kidgo .
Duh , kaka naona uliwahi kushtukia hilo jambo mapema, hawo washenzii wangenda hata kukutoa kafara. Maana wanajua ulikuwa auna Cha kuwapa.Ok... nilikuwa nimechoka....
Sasa ikabidi twende kwa huyo tajiri.., hapo tuko watatu mimi ndo mdogo niko form three hapo... Wengine age yao around 27 hivi... Halafu ni usiku kama saa mbili kasoro nikapewa mimi mzigo maana jamaa yule aliogopa kuubeba... Alisema kuna mwingine aliwaonesha boda wakapita nao alikuwa nato tuwili...njiani wakati tunaenda akili iko junction nawaza nikipata hiyo heka naifanyia nini? Nyingine inanisanua hii dili ikifeli nitajuta sana.. Nyingine mzigo ninao mimi sasa hapa nikufanya namna nichukue kidogo nipite hivi. Hapo nimewekwa mtu kati hakuna kukimbia... Nikakumbuka tamaa mbele mauti nyuma hawa jamaa ni kama siwaelewi kwanini mipango yao haipingani hata kidogo.... Nikawaambia oy nyie nendeni mimi bado nasoma... Jamaa wakareact et dogo acha ujinga utajiri ndio huu mhh... Nikaachananao
Kwa kweli ni mungu tuu , peke angu nisingeweza .Mungu amekusaidia sana.
Ungetapeliwa vibaya mno.
Hakika tena kama issue hizi za dhahabu matambiko ni lazima., ila nishakutananao wawili tena wa hivihivi...wakiniuliza nawajibu tu... sijui usemalo naangalia na pembeni huyo....Duh , kaka naona uliwahi kushtukia hilo jambo mapema, hawo washenzii wangenda hata kukutoa kafara. Maana wanajua ulikuwa auna Cha kuwapa.
Bac itakuwa niliwaza tofauti, kutokana na matukio ninayoyajua.Ulikua unatapeliwa tu easy.
Wala hamna mambo ya figo
Ahsante ndugu yangu .Hahahaha pole sana
😂😂😂, kwa sasa nadhani hata mm nitakuwa makini.... Maana sometimes sisi Wanaume tunakawaida ya kupuuzia mambo sana.Hakika tena kama issue hizi za dhahabu matambiko ni lazima., ila nishakutananao wawili tena wa hivihivi...wakiniuliza nawajibu tu... sijui usemalo naangalia na pembeni huyo....
Take careKweli kabisa , naona mungu alikuwa na Mimi changanya na nyuzii zenu za kutuelimisha watu huwa tunapata mwangaza wa mambo mbalimbali .
Huu wizi wa miaka ya 70Hivi kuna watu bado wanaibiwa kizembe ivo
Mi mwenyewe Dodoma hapo hapo nusu nitapeliwe hivyo hivyo, waliiba simu ya rafiki yangu wakawa wanatuma meseji..
Naomba niwasimulie tuu,
Leo nimepatwa na jaribu gumu sana kwa mara yangu ya kwanza katika maisha yangu. Nimekuwa nikisoma thread nyingi tu humu JF kuhusu vijana kuacha masuala mazima ya tamaa, pamoja na mikasa ya watu iliyowapata kama story ya yule jamaa aliyekuwa wakimwita Apostle. Mtanisamehe pia kwa uandishi wangu, siyo mzuri. Twende kazi.
Nikiwa ghetto nasoma kujiandaa na UE kwa ajili ya kwenda kesho nikafanye paper la Industrial Economics, mara simu yangu ikaanza kuita.
Mimi: "Haloo, habari?"
Namba ngeni: "Safi huko, poa mwanangu."
Hii sauti ilimatch kabisa na ya mwanangu mmoja ambaye tunapenda kuitana Kindindi Kindindi tangu tupo shule ya msingi.
Mimi: "Kumbe mwanangu Kindindi! Vipi huko, upo poa wewe?"
Namba ngeni: "Nipo poa kabisa mwanangu. Hivi upo Dodoma sehemu gani wewe?"
Sikuhofia kwa kuwa huyu rafiki yangu anajua kuwa mimi nasoma UDOM, pia makazi yangu yapo nje ya chuo.
Mimi: "Ninakaa Makulu hapa mwanangu. Kwani wewe upo wapi kaka? Kwani upo Dodoma?"
Namba ngeni: "Ndiyo nipo Dodoma mwanangu, sema nipo Kibaigwa huku. Kuna mradi wa Kilimo Kwanza nimekuja kusimamia."
Mimi: "Mmmh! Kwani mwanangu UE kwenu vipi? Maana hiki ni kipindi cha mitihani halafu upo huku. Kwamba mmeshamaliza UE au? Au nyie kwenu bado?" Nikajiongeza kwa kumuuliza, "Au kwa sababu ya ile GPA ya tano uliyoipata ndiyo umepata chance mwanangu? Duuh! Na posho vipi, uhakika wanakugea ya kutosha kaka?"
Huyu rafiki yangu anasoma chuo cha TIA pale DSM.
Namba ngeni: "Ndiyo mwanangu, sisi UE bado tuna kama week tatu mbele. Huu mradi nausimamia kwa muda mfupi halafu nageuza. Ila kuna issue nataka nikupange mwanangu. Unajua wewe kama mwanangu nimeona nikupe hili dili.
"Kuna boss wangu hapa, yeye nipo naye huku lakini makazi yake ni hapo Dodoma Town. Kuna wateja wake wapo Dodoma Hotel ndipo walipopumzikia, sasa anahitaji mtu mwaminifu amsaidie kwa kuwa yeye yupo mbali na huko. Ila wewe mwanangu najua upo karibu na Town, hivyo itakuwa rahisi kumsaidia."
Mimi: "Anhaa! Usiwaze kaka. Ingawa kesho nina mitihani, lakini kama itachukua siku ya leo tu nitafanya mwanangu. Ila isizidi leo?"
Namba ngeni: "Sawa mwanangu, usiwaze. Ni leo tu basi. Cha msingi uwe mwaminifu kwa sababu huyu boss wangu ananiamini na kunikubali sana."
Mimi: "Usijali kaka kuhusu hilo."
Namba ngeni: "Sawa mwanangu, ngoja nimpe namba yako atakupigia uongee naye."
Mimi: "Sawa."
Basi hapo nikawa nimekaa nafurahi. Ukiangalia wanachuo sasa hivi boom limepukutika, hivyo nikawaza naweza kupata hata kaelfu kumi kanisaidie kula siku chache mbele hadi mwezi utakapoisha. Nikawa sasa nimekaa kiaskari kumsubiria huyo boss wake aliyekutana naye huko anipigie.
Muda si mrefu kidogo simu ikaanza kuita.
Inaendelea..................................................
Sehemu ya pili.............................Namba ngeni ya pili (ambaye ni boss wake): "Halo, habari yako kijana?"
Mimi: "Safi ndugu, sijui wewe kwema?"
Boss: "Safi kabisa kijana. Mimi nimepewa namba na rafiki yako. Ameniambia wewe ni kijana mwaminifu kabisa. Mimi kwa majina naitwa Mzee Mabuha, natokea Kibaigwa. Kuna kitu nataka unisaidie hapo Town, lakini naomba unipe address kuhusu wewe, unapotokea ni sehemu gani."
Mimi: Kwa majina naitwa... Nikawaza fasta nikachakata chap nimtajie jina langu lenyewe. Nikakumbuka kuwa ni boss wa rafiki yangu, nikasema ngoja nimtajie tu. Nikamwambia, "Mimi naitwa Travellar. Natokea Mkalama hapa."
Kwa kuwa nilikuwa najua ni mwenyeji, nikajua lazima atakuwa anapajua.
Boss: "Mkalama Singida au? Maana nimemwambia huyu rafiki yako nahitaji mtu wa karibu na huku."
Mimi: "Ndiyo, nipo Mkalama, nipo karibu chini ya Makulu. Ni Dodoma tu hapa hapa."
Boss: "Anhaa!" Akacheka, kisha akasema, "Hapo sawa. Sasa kijana wangu, nadhani Dodoma Hotel unaijua vizuri sana."
Nikamjibu, "Naifahamu."
Akaendelea akasema, "Sasa kuna wateja wangu wapo Dodoma Hotel, wanatokea DSM. Huwa nawauzia water pumps kwa shilingi laki tatu (300,000). Yaani hapo nimeweka cha juu. Lakini hizo water pumps ninanunua kutoka kwa Mzee Masanja, ambaye yeye anafanya delivery na kupakia mzigo bure. Mimi ni mteja wake, ananifahamu kama Mzee Mabuha."
Akaendelea...
"Huyu Mzee Masanja yeye anauza water pumps kwa shilingi laki moja na nusu (150,000), lakini mimi wale wateja nawauzia kwa laki tatu. Kwa hiyo sitaki wajue sehemu ninayonunulia mzigo, ndiyo maana nataka nikutumie wewe kama kijana wangu unisaidie kwa hilo, kwa sababu mimi niko mbali na huko.
"Hizo water pumps wanahitaji 30, ambapo ukizidisha mara laki tatu unapata milioni tisa. Hicho ndicho kiwango cha fedha nitakachopokea kutoka kwa wale wateja wangu.
"Kisha katika hiyo fedha nitatoa milioni nne na laki tano ambazo nitamlipa Mzee Masanja anayeuza zile water pumps kwa shilingi laki moja na nusu (150,000).
"Kisha itabaki milioni nne na laki tano. Ambayo ndiyo ya kwetu. Nitakutumia milioni tatu, halafu mimi nichukue milioni moja na laki tano."
Nikamjibu, "Sawa."
Akasema, "Nakutumia namba ya Mzee Masanja. Tutawasiliana hatua kwa hatua kijana wangu, sawa?"
Nilimjibu kwa kujiamini, "Sawa Mzee Mabuha."
Nilionyesha ushupavu, licha ya kwamba kazi yenyewe niliona ni nzito sana, hasa ukizingatia ni mtu nisiyemjua, halafu fedha zinazozungumziwa ni nyingi sana. Lakini nilijitahidi kuonyesha ushupavu ili anione kuwa mimi ni kijana mzuri na kazi nitaiweza.
Kisha akakata simu.
Mimi: Nikaanza kuwaza kidogo. Nikaanza kurelate na ile story ya jamaa aliyekuwa wakimwita Apostle ambaye alielezea kisa chake. Kisha nikaanza kurelate na thread ya majuzi iliyotuambia vijana tuache tamaa.
Nikaanza kumuwazia huyu rafiki yangu. Kwamba siku hizi amekuwa tapeli, haliingii akilini kwa sababu namjua vizuri sana.
Nikaanza kuwaza pia kuwa leo nimepigiwa simu nyumbani na mama yangu mdogo. Nilipopokea simu nililaumiwa sana kuhusu kutopiga simu nyumbani. Nilisemwa sana, kwa kifupi. Nikakubali makosa yangu, maana ukweli mimi ni mmoja wa watoto wanaopiga simu nyumbani kwa manati.
Kisha nikambiwa mama yangu anataka kuongea na mimi.
Baada ya kuongea na mama yangu, aliniambia niache tabia ya kubadilisha laini mara kwa mara. Pia aliniambia kuwa jana ameniotea vibaya sana.
Akaniuliza kama siumwi.
Nikamwambia, "Mimi niko salama kabisa."
Basi tukaongea sana, akanisisitiza sana suala zima la ibada.
Kisha tukaagana.
Baadaye nikarelate na jambo hilo, lakini nikasema acha nilipuuzie, kwa kuwa ninamwamini sana rafiki yangu, tena amenipa dili. Nikajisemea:
"Acha nikalifanye bhana."
Sehemu ya tatu ......................
Sasa wakati nataka niende kuoga ili nijiandae kwa kuanza safari, nikiwa nawaza huku ni kama nimepigwa zongo, ndipo mawazo yakanijia.
Kuna diary yangu ambayo nimeandika baadhi ya surah ambazo huwa nazisoma mara kwa mara. Nikasema, acha nisome kwanza hizi surah nne za ulinzi, maana naenda sijui nakwenda kukutana na nini, ingawa bado nilikuwa na imani kidogo kwa yule rafiki yangu.
Nikasoma Ayatul Kursiy, Suratul Ikhlas, Suratul Falaq na Suratun Nas.
Kisha nikaanza kupasha moto maji.
Sasa ndipo wazo likanijia:
"Kwa nini usimpigie kwanza rafiki yako Kindindi kwenye namba zake nyingine?"
Hapo nikahisi kama nimetoka kwenye usingizi mzito. Akili ikaanza kufanya kazi vizuri.
Sikurudia ile namba ya mwanzo iliyojitambulisha kuwa ni rafiki yangu.
Nikawaza, kama hawa ni matapeli, huenda wamemteka hata rafiki yangu bila yeye kujua. Sasa akili ilikuwa imetulia na niliweza kuwaza kwa mantiki kidogo.
Nikakumbuka vizuri kisa cha Apostle, jinsi walivyokuwa wanatumia namba ngeni badala ya namba zao halisi. Nikasema huenda hata rafiki yangu wamefanya hivyo.
Nikajisemea:
"Ngoja nipige namba zake nyingine ambazo ninazo. Kama wameitrack ile namba, hizi nyingine hawawezi kuzijua."
Mimi nikaanza kupiga simu.
Namba ya kwanza ya rafiki yangu haikupatikana.
Nikapiga nyingine ambayo pia ninayo, ikaanza kuita.
Rafiki yangu: "Halo, vipi mwanangu Kindindi?"
Nilitaka kujiridhisha kama kweli ndiye au tayari tulikuwa tumeshaongea muda mfupi uliopita.
Mimi: "Safi kaka. Pande gani hapo?" (Niliuliza swali la mtego ili nipate uthibitisho.)
Rafiki yangu: "Nipo zangu Yombo tu, nimepoa. Maana UE tumeshamaliza."
Kwa kweli niliogopa sana.
Yule mtu aliyenipigia simu mwanzo alikuwa anafanana na rafiki yangu kwa kila kitu, hasa sauti.
Ikanibidi nimuulize moja kwa moja.
Mimi: "Wewe mwanangu hujanipigia simu muda si mrefu kwa namba ngeni? Ukaniambia upo Kibaigwa?"
Nilikuwa naongea kama mtu aliyedata kidogo, aliyeona maajabu.
Rafiki yangu: "Kindindi, tulia mwanangu. Kuna nini kwani? Mbona sikuelewi? Mimi nimekupigia? Sijakuelewa bado."
Hapo ndipo nilipopata uhakika.
Nikajisemea:
"Duuh! Mungu ni mkubwa kwa kweli."
Nikaanza kumsimulia rafiki yangu kila kitu kilichokuwa kimetokea.
Baada ya kunisikiliza, alinipa pole sana, kisha akaniambia niiripoti namba zile TCRA ili zifuatiliwe.
Baada ya kumaliza kuongea naye, nilikaa kimya kwa muda mrefu.
Kwa kweli nilichoka sana.
Hata hamu ya kuendelea kusoma ikakata kidogo.
Nikawa nawaza matukio kama haya ambayo yameshawahi kuwatokea baadhi ya dada zetu wa vyuoni. Wengine walidanganywa kwa tamaa za pesa na watu waliojifanya matajiri, wakawaita mikoani kwa ahadi mbalimbali, na mwisho wakapoteza maisha.
Nilihisi hofu kubwa sana.
Nikajiuliza:
"Leo mimi kingenitokea nini kama nisingeshtuka mapema?" Aisee mungu mwacheni aitwe mungu tu.
Mwisho, napenda kuwapongeza sana wanajukwaa wa JamiiForums.
Thread zenu nyingi zimekuwa darasa kubwa kwa vijana wengi. Mnaelimisha, mnaonya na mnatujengea uelewa kuhusu mbinu mbalimbali zinazotumiwa na matapeli.
Nawashukuru sana watu kama Mr. Apostle (kama sikosei jina), Brother Mshana, pamoja na wanajukwaa wengine wote ambao huwa mnaandika nyuzi zenye mafunzo na kutupa matumaini sisi vijana.
Kwa kweli huwa nasoma thread zenu nyingi, na kila mara zinaniongezea maarifa.
Asanteni sana.
Kwa hiyo ndiyo hivyo umemaliza kunywa "kyai" yako? Au iliishapoa?.