Wanabodi,
Kama ni kweli, kamtumia e-mail Mhe rais, ni nyinyi tuu msiojua kuwa hiyo sio e-mail ya maelekezo, bali ni kumkumbusha tuu, akumbuke fadhila
Kuna jitu fulani moja la ajabu sana likiitwa Patrick Rutabanzibwa, lenyewe lilikuwa jeuri na roho mbaya ya ajabu, hata kuthubutu, kuukataa 'wema' wa James Rugemalila, kwa vile 'wema' wenyewe uliachwa nyumba hadi hadi nyumba kabla ya sikukuu, wengine wote waliukubali. wakaupokea na kusherehea krismasi njema! kwa raha mustarehe kwa 'wema' wa JR!. Hiri rijamaa, li Patrick Rutabanzibwa na jiroho lake baya, lilikuwa na kiburi na jeuri ya ajabu yards kuthubutu kuukataa 'wema' wa JR ulioachwa nyumbani kwake kabla ya Krismasi, hivyo baada tuu ya sikukuu, ya Krismass liliubeba 'wema' ule vile vile ulivyo, likaurudisha kwa JR!. JR akaripoti kwa mabosi wake waliopokea 'wema' wake, hao mabosi wakalikomesha hilo lijamaa kwa kulikomoa, na kuliadhibu kwa kuliweka pembeni!, IPTL ikapita!.
Haya majina yanayopigiwa kelele humu kuwa wamelipwa, ni majina ya 'wema' wa kajibenki kadogo tuu, ka Mkombozi ambako kazi yake ni kuwakomboa watu!, laiti watu wangeliyaona majina ya recipients wa sadaka za wema kubwa wa PAP toka libenki likubwa la Stanbic!, au majina ya 'wema' mkubwa wa JR kutoka kwenye ile account yake ya nchini Holland, kuwa transifia "wanene" kupitia account zao zilizoko Credit Susie!, watu humu wangebaki midomo wazi!.
Majina yote yaliyo leak, ni yale majina ya tuji 'sadaka' tudogo twa "Mkombozi tuu!", no names kwenye miji binge yards 'mijisadaka' mikubwa ya PAP na no names za big fishes wa 'mijisadaka' mikubwa ya account yake ya Holland!. Threat kubwa kwa JR, sasa ni kutoka kwa hao hao "big fish" recipients, aliowatendea 'wema' mkubwa kwa mijisadaka mikubwa mikubwa, ambao kama ni kweli JR atatiwa misuko suko, watakosa amani kwa kuhofia asije kuwa harassed too much, akakasirika na hatimaye akaamua kufungua mdomo!.
Mimi ni muumini wa "ukweli usemwe!", "the truth must be told no matter who, what, where, when, and how (5W+H) hivyo kuna siku itafika na ukweli utasemwa!.