Escrow: Tumuombee J. Rugemalila alindwe kwa nguvu na uweza wa Roho Mtakatifu!, Wema wake usimponze!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Wanabodi,

"Wema usizidi uwezo!" ila pia too much of anything is harmful, hivyo "wema nao ukizidi, unaweza kukuponza!".

Bwana Mungu alitupa amri kuu "mpendane"!, katika utekelezaji wa amri hii, kuna baadhi ya wenzetu waliojaaliwa uwezo mkubwa wa upendo, hadi kufikia level ya kuwa na "upendo wa mshumaa", kumulikia wengine huku kwake kunateketea!, hivi ndivyo ulivyo wema wa Mzee Wetu huyu, Mzee James Rugemalila, (Mzee JR), ule wema wake sasa unataka kumponza!. Laiti baada ya kujivutia ule mpunga wake, angelijikalia kimya na kujifanya kama ana roho mbaya ya uchoyo, labda yote haya yasingalitokea, you never know!. Tumuombee ulinzi wa Roho Mtakatifu, amlinde kwa nguvu na uwezo wake ili yasimkute yale yaliyoimbwa na mwanamuziki, Patrick Balisidya kuwa "Wema Hawana Maisha!", au Hemedi Maneti kuhusu "Wanaopendwa na Wengi!".

Nimesikia kwa juu juu, kuwa utekelezaji wa yale Maazimio batili ya Bunge kuhusu Escrow, unatarajiwa kuanza, hivyo ni pamoja na lile azimio la uonevu la kukamatwa na kutiwa nguvuni kwa Singa Singa wa PAP na Mzee wetu, mwema, Mzee James Rugemalila, mwenye roho ya upendo wa ajabu, na moyo wa huruma iliyopitiliza, kuwa na yeye anatakiwa kukamatwa!. Singa Singa atakuwa ameishajitimkia zake ughaibuni siku nyingi kama walivyotimka kina Vithlani, ila namshauri Mzee wetu James Rugemalila, yeye asitimkie popote, kwa sababu hajafanya kosa lolote na tunamuombea ulinzi kwa Mungu Baba kupitia Roho Mtakatifu wake, na sala zetu, amlinde, atampigania na atashinda!.

Naomba kwa hapa tuwe wakweli, huyu Mzee JR akamatwe kwa kosa gani?. Aliyechota fedha za escrow ni kalasinga wa PAP, fedha za Escrow zimelipwa PAP, yeye amefanya biashara halali kabisa ya kuuza hisa zake halali ndani ya VIP kwa kumuuzia PAP, na amelipwa na PAP malipo halali kwa hisa zake, na baada ya kupokea malipo, amelipa kodi zote stahiki na halali za serikali, pesa zilizobaki ndizo amezifanyia wema kuzigawa kama sadaka au asante kwa wale aliowachagua, sasa kosa lake ni lipi?!, na waliopokea sadaka ya wema ule wana kosa gani?!. Hakuna kosa lolote kwa mtu yoyote kugawa fedha zake mwenyewe kwa yeyote, na hakuna kosa lolote kwa mtu kupokea fedha zozote halali toka kwa yeyote.

Kwa mliofuatilia kisa kizima cha IPTL tangu kuingia kwake, mtakubaliana na mimi kuwa Mzee James Rugemalia amefanya sana 'wema', haiwezekani, watu wale wale waliofanyiwa 'wema' ule, leo ndio waje wamgeuke na kumtia misukosuko!. Huu utakuwa ni utovu wa fadhila unless waje wengine wasiojua wema wake!.

Naomba kukiri, nimekuwa inspired kuandika haya, kufuatia post ya mwana jf huyu.
Isitoshe, kamtumia mh rais emails zenye maelekezo ya hatua za kuchukuliwa na serikali. He owns this impotent corrupt government

Kama ni kweli, kamtumia e-mail Mhe rais, ni nyinyi tuu msiojua kuwa hiyo sio e-mail ya maelekezo, bali ni kumkumbusha tuu, mhe. Rais akumbuke fadhila!. Na mimi namuunga mkono JR kwa asilimia 100%, ombi langu ni moja tuu, nawaomba sana viongozi wetu, wasiwe watovu wa fadhila!, wawe watu wa shukrani, wakumbuke walikotoka na jinsi walivyotendewa 'wema' na Mzee wetu huyu James Rugemalila!, hivyo wanapaswa kulipa fadhila!.

Mimi nakikumbuka kukisoma kisa kimoja cha 'wema' fulani Mzee wetu huyu, alioutandaza kipindi cha kukaribia sikukuu ya Krismasi fulani!, aliwazungukia "wanene" wote wanaohusika na usajili wa VIP na kuwatendea 'wema' stahiki. Katika waliotendewa wema huo, kuna jitu fulani moja la ajabu sana likiitwa li Patrick Rutabanzibwa, lenyewe lilikuwa ni jitu bold, kiburi, jeuri na roho mbaya ya ajabu, hata kuthubutu, kuukataa 'wema' wa James Rugemalila, kwa vile 'wema' wenyewe uliachwa nyumba hadi nyumba kabla ya sikukuu, wengine wote waliukubali wema ule na wakaupokea na kusherehea krismasi njema! kwa raha mustarehe kwa 'wema' wa JR!. Hiri rijamaa, li Patrick Rutabanzibwa na jiroho lake baya, lilikuwa bold, kiburi na jeuri ya ajabu ya kuthubutu kuukataa 'wema' wa JR ulioachwa nyumbani kwake kabla ya Krismasi, kisa hawezi kupokea 'wema' wa mashaka bila kujua 'wema' huo ni wa nini!. hivyo baada tuu ya sikukuu, ya Krismass li Patrick Rutabanzibwa, liliubeba 'wema' ule vile vile ulivyo, likaurudisha kwa JR!.

JR akaripoti kwa mabosi wake ambao wao waliopokea 'wema' wake, hao mabosi wakalikomesha hilo lijamaa kwa kulikomoa, na kuliadhibu kwa kuliweka pembeni!, IPTL ikapita!.

Sasa hii IPTL ilipita pitaje na ni kina nani waliipitisha, na kwa 'wema' upi wa mradi huu!, wote tunaojua, tunajua!, na wahusika wanajulikana kwa majina na 'wema' wote waliotendewa na huyu Mzee wetu wa wema, James Rugemalila!, unajulikana!, iweje leo wakose shukrani?!, wakose fadhila kutaka kumuadhibu?!. Not this time labda wakija wengine!.

Haya majina yanayopigiwa kelele humu kuwa wamelipwa, ni majina ya 'wema' kiduchu tuu wa kale kajibenki kadogo tuu, ka Mkombozi ambako kazi yake ni kuwakomboa watu!, laiti watu wangeliyaona majina ya recipients wa sadaka za wema kubwa wa PAP toka libenki likubwa la Stanbic!, au majina ya 'wema' mkubwa wa JR kutoka kwenye ile account yake ya nchini Holland, kuwa transifia "wanene" kupitia account zao zilizoko Credit Suisse!, watu humu wangebaki midomo wazi!.

Haiwezekani mtu ufanye 'wema' huo wote!, alafu leo wema wako uje kukuponza usumbuliwe na vijitu vidogo vidogo visivyojua kitu!. Enyi wote mliofanyiwa wema na JR kumbukeni fadhila wajameni!, huwezi kutendewa mema ukalipa kwa maovu, hata Mungu hapendi!, mtalaaniwa!.

Kama Mzee wetu huyu, JR, hata baada ya wema wote huo, na bado anasumbuliwa!, mimi ninachohofia sasa, ni uwezekano wa kumyamazisha jumla!.

Majina yote yaliyo leak, ni yale majina ya tuji 'sadaka' tudogo twa "Mkombozi tuu!", no names kwenye ile miji bingo mikubwa minene ya 'mijisadaka' mikubwa ya PAP iliyochotea cash kutoka Stanbic bank na kubebwa kwe magunia ya sandarusi, na no names za big fishes wa 'mijisadaka' mikubwa ya account yake ya Holland!.

Threat kubwa kwa JR, sasa ni kutoka kwa hao hao "big fish" recipients, aliowatendea 'wema' mkubwa kwa mijisadaka mikubwa mikubwa, ambao kama ni kweli JR atatiwa misuko suko, watakosa amani kwa kuhofia asije kuwa harassed too much, akakasirika na hatimaye mwisho akaamua kufungua mdomo!.

Ili kujihakikishia usalama wao na majina yao kutotajwa, wanaweza kabisa kuamua "kumfunga mdomo" jumla!, kwa kuitumia ile kanuni ya ikibidi punda afe, na afe tuu ili mradi mzigo ufike!, kama usalama wao ni ile "silence yake", silence hiyo ikiwa threatened, kuliko wao kujulikana, bora kumremainisha silent!.

Watanzania wote wenye mapenzi mema na uhai wa binadamu, na wenye kupenda kuujua ukweli, majina ya Mkombozi ni cha mtoto!, tuungane kwa sala na maombi, kumuombea uzima Mzee wetu James Rugemalila, tena sii kwa ulinzi tuu wa binadamu tuu, maana hatuwezi, hila za mwovu shetani ni nyingi, tuombe na tumfungie novena apate ulinzi wa nguvu na uweza wa Roho Mtakatifu, awe salama, ili siku ya siku itafika ataweza kumulikiwa na ule mwanga mkubwa kama wa Sauli kwenye ile njia ya kwenda Jeriko, mwanga ule ukamfungulia, Sauli akaona mwanga, akanena, akabadilika na kuwa Paulo. Vivyo hivyo tumuombe uzima Mzee wetu James Rugemalila, ili ifike siku na yeye aone mwanga!, atanena!, ndipo mtaujua ukweli!.

Kitakachokuja kumtokea James Rugemalila ni kile kile kilichowatokea wana wa Israel utumwani Misri. Aliyewaleta Israel Misri ni Yusufu kwa wema alioutenda wa kutabiri ile ndoto ya Farao. Hivyo Waisrael wakahamia Misri kwa shangwe. Baada ya muda akatokea Farao mwingine ambaye hakuujua wema wa Yusufu, hivyo akawageuza Wa Israel kuwa ni watumwa!.

Hivyo tuendelee kuomba na hapa nchini kwetu kusije tokea utawala mwingine ambao haujui wema wa James Rugemalila, hivyo msije kushangaa siku ya siku mambo yakabadilika huu wema Rugemalila alioutenda ukaja kumponza na kumtokea puani!.

Mimi ni muumini wa "ukweli usemwe!", "the truth must be told no matter who, what, where, when, and how (5W+H) hivyo kuna siku itafika na ukweli utasemwa!.

Eh Mungu, kupitia Roho Mtakatifu wako, na jeshi lako lote la Malaika wa Mbinguni, mlinde Mzee Wetu, James Rugemalila na majaribu yote yaliyo mbele yake, hadi afike ile siku uliompangia ya ukweli kujulikana kwanza, na ndipo baadaye aje atimize mapenzi yako kwa kadri ulivyompangia wewe!.

Amen.

Paskali.
 
boot-licker.jpg
 
Hakuna aliyemwema duniani na mbinguni isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee yake.
Pili,usingizie ukristo kwenye mambo ya kishenzi na kishetani.
Tatu,mwogopeni Mungu. Unasema analipa wema? Kwa lipi hilo?
Waliolipwa wote walikuwa kwenye uratibu mnzima wa kuhujumu nchi toka mwanzo huku rais kikwte akifaham hilo. Unakuja kusema analipa wema? Kwa bure?
There is nothing free in this world.
 
Wanabodi,

"Wema usizidi uwezo!" ila "wema nao ukizidi, unaweza kukuponza!", Mzee Wetu James Rugemalila, ule wema wake sasa unataka kumponza!. Laiti baada ya kujivutia ule mpunga wake, angejikalia kimya na roho mbaya ya uchoyo, labda yote haya yasingetokea, you never know!. Tumuombe ulinzi wa Roho Mtakatifu, ili yasimkute yale yaliyoimbwa na mwanamuziki, Patrick Balisidya kuwa "Wema Hawana Maisha!", au Hemedi Maneti kuhusu "Waopendwa na Wengi!".

Nimesikia kwa juu juu, kuwa utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Escrow, unatarajiwa kuanza, hivyo ni pamoja na lile azimio la kukamatwa na kutiwa nguvuni kwa Singa Singa wa PAP na Mzee wetu, mwenye huruma, na moyo mwema wa kujitolea na roho nzuri ya ajabu, Mzee James Rugemalila!.

Naomba kwa hapa tuwe wakweli, huyu Mzee akamatwe kwa kosa gani?, amefanya biashara halali ya kuuza hisa zake, amelipwa pesa zake, amelipa kodi za serikali, zilizobaki amegawa kama sadaka au asante kwa aliowachagua, sasa kosa lake ni lipi?!.

Kwa mliofuatilia kisa kizima cha IPTL tangu kuingia kwake, mtakubaliana na mimi kuwa Mzee James Rugemalia amefanya sana "wema", haiwezekani, watu wale wale waliofanyiwa "wema" ule, leo waje wamgeuke na kumtia misukosuko!.

Naomba kukiri, nimekuwa inspired kuandika haya, kufuatia post ya mwana jf huyu.

Kama ni kweli, kamtumia e-mail Mhe rais, mimi ombi langu ni moja tuu, nawaomba sana viongozi wetu, wasiwe wachovu wa fadhila!, wakumbuke walikotoka na jinsi walivyotendewa "wema" na Mzee wetu huyu James Rugemalila!, mimi nakumbuka kuusoma "wema" fulani alioutandaza kipindi cha kukaribia Krismasi fulani!, kuja jitu fulani lenyewe likiitwa Partic Rutabanzibwa, lilikuwa na roho mbaya ya ajabu, hata kuukataa "wema" wa James Rugemalila, lakini wengine wote waliukubali na kuneemeka!. Dawa ya roho mbaya huyo, ilikuwa ni kumuweka pembeni!, IPTL ikapita!, ilipitaje pitaje, na kina nani waliipitisha, na wema upi wa mradi huu, wote wanajulikana, na majina yote ya waliotendewa wema, na ni wema gani, anayo Mzee wetu wa wema, James Rugemalila!.

Haya majina yanayopigiwa kelele, ni majina ya "wema" wa kajibenki kadogo tuu, "Mkombozi", laiti watu wangeyaona majina ya recipients za sadaka za wema wa PAP toka libenki likubwa la Stanbic, au majina ya "wema" mkubwa wa JR kutoka kwenye account yake ya nchini Holland, kuwa transfia "wanene" kupitia Credit Susie!, watu humu wangebaki midomo wazi!. Haiwezekani mtu ufanye "wema " huo wote!, alafu leo uje usumbuliwe na vijitu vidogo vidogo!, mliofanyiwa wema kumbukeni fadhila wajameni, huwezi kutendewa mema ukalipa kwa maovu, hata Mungu hapendi!, mtalaaniwa!.

Kama Mzee wetu huyu, JR, hata baada ya wema wote huo, na bado anasumbuliwa!, mimi ninachohofia sasa, ni uwezekano wa kumyamazisha JR jumla!.

majina yote yaliyo leak, ni yale majina ya "sadaka" ya "Mkombozi tuu!", no names kwenye "sadaka" ya PAP na no names za big fishes wa "sadaka" za account yake ya Holland!. Threat kubwa kwa JR, sasa ni kutoka kwa hao hao "big fish" recipients, kwa kuhofia asije kuwa harassed too much, akasirika na hatimaye kufungua mdomo!, wanaweza kabisa "kumfunga mdomo" jumla!, kwa kuitumia ile kanuni ya ikibidi punda afe, na afe tuu ili mradi mzigo ufike!, kama usalama wao ni ile "silence yake", silence hiyo ikiwa threatened, kuliko wao kujulikana, bora kumremainisha silent!.

Watanzania wote wenye mapenzi mema na uhai wa binadamu, tuungane kwa sala kumuombea uzima Mzee wetu James Rugemalila, tena kwa ulinzi tuu wa binadamu hatuwezi, tumfungie novena apate ulinzi wa nguvu na uwezo wa Roho Mtakatifu, awe salama, ili siku ya siku ataweza kumulikiwa na ule mwanga mkubwa kama wa Sauli kwenye ile njia ya kwenda Jeriko, mwanga ule ukamfungulia, Sauli akaona mwanga, akanena, akabadilika na kuwa Paulo. Vivyo hivyo tumuombe uzima Mzee wetu James Rugemalila, ili ifike siku na yeye atanena!, ndipo mtaujua ukweli!.

Mimi ni muumini wa "ukweli usemwe!",

Eh Mungu, kupitia Roho Mtakatifu wako, na jesho lote la Malaika wa Mbinguni, mlinde Mzee Wetu, James Rugemalila na majaribu yaliyo mbele yake.

Amen.

Pasco.

Wachache sana wataelewa andiko lako
 
Mkuu mara nyingi Politicians ndivyo walivyo,wakibanwa na waajiri wao hawakawii kuwatosa wafadhili wao/ washirika kwenye uwizi na mwisho inakuwa vita za Kimafia kati yao.

Ila kiuhalisia JR hana wema wowote pamoja na ukweli uliousema kuwa awe makini kuhusiana na maisha yake.
Kama hilo anaona ni ngumu ni vizuri akubali kuwa mtumwa kuaanzia muda huu kwa kupitishwa mbele ya majaji wale wale waliompatia nafuu nyingi katika kesi zake za kibiashara na yeye akawapa zawadi.
Lakini pia anaweza kukubaliana na staili ya Daudi Balali.

Wanabodi,

"Wema usizidi uwezo!" ila "wema nao ukizidi, unaweza kukuponza!", Mzee Wetu James Rugemalila, ule wema wake sasa unataka kumponza!. Laiti baada ya kujivutia ule mpunga wake, angejikalia kimya na roho mbaya ya uchoyo, labda yote haya yasingetokea, you never know!. Tumuombe ulinzi wa Roho Mtakatifu, ili yasimkute yale yaliyoimbwa na mwanamuziki, Patrick Balisidya kuwa "Wema Hawana Maisha!", au Hemedi Maneti kuhusu "Waopendwa na Wengi!".

Nimesikia kwa juu juu, kuwa utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Escrow, unatarajiwa kuanza, hivyo ni pamoja na lile azimio la kukamatwa na kutiwa nguvuni kwa Singa Singa wa PAP na Mzee wetu, mwenye huruma, na moyo mwema wa kujitolea na roho nzuri ya ajabu, Mzee James Rugemalila!.

Naomba kwa hapa tuwe wakweli, huyu Mzee akamatwe kwa kosa gani?, amefanya biashara halali ya kuuza hisa zake, amelipwa pesa zake, amelipa kodi za serikali, zilizobaki amegawa kama sadaka au asante kwa aliowachagua, sasa kosa lake ni lipi?!.

Kwa mliofuatilia kisa kizima cha IPTL tangu kuingia kwake, mtakubaliana na mimi kuwa Mzee James Rugemalia amefanya sana "wema", haiwezekani, watu wale wale waliofanyiwa "wema" ule, leo waje wamgeuke na kumtia misukosuko!.

Naomba kukiri, nimekuwa inspired kuandika haya, kufuatia post ya mwana jf huyu.

Kama ni kweli, kamtumia e-mail Mhe rais, mimi ombi langu ni moja tuu, nawaomba sana viongozi wetu, wasiwe wachovu wa fadhila!, wakumbuke walikotoka na jinsi walivyotendewa "wema" na Mzee wetu huyu James Rugemalila!, mimi nakumbuka kuusoma "wema" fulani alioutandaza kipindi cha kukaribia Krismasi fulani!, kuja jitu fulani lenyewe likiitwa Partic Rutabanzibwa, lilikuwa na roho mbaya ya ajabu, hata kuukataa "wema" wa James Rugemalila, lakini wengine wote waliukubali na kuneemeka!. Dawa ya roho mbaya huyo, ilikuwa ni kumuweka pembeni!, IPTL ikapita!, ilipitaje pitaje, na kina nani waliipitisha, na wema upi wa mradi huu, wote wanajulikana, na majina yote ya waliotendewa wema, na ni wema gani, anayo Mzee wetu wa wema, James Rugemalila!.

Haya majina yanayopigiwa kelele, ni majina ya "wema" wa kajibenki kadogo tuu, "Mkombozi", laiti watu wangeyaona majina ya recipients za sadaka za wema wa PAP toka libenki likubwa la Stanbic, au majina ya "wema" mkubwa wa JR kutoka kwenye account yake ya nchini Holland, kuwa transfia "wanene" kupitia Credit Susie!, watu humu wangebaki midomo wazi!. Haiwezekani mtu ufanye "wema " huo wote!, alafu leo uje usumbuliwe na vijitu vidogo vidogo!, mliofanyiwa wema kumbukeni fadhila wajameni, huwezi kutendewa mema ukalipa kwa maovu, hata Mungu hapendi!, mtalaaniwa!.

Kama Mzee wetu huyu, JR, hata baada ya wema wote huo, na bado anasumbuliwa!, mimi ninachohofia sasa, ni uwezekano wa kumyamazisha JR jumla!.

majina yote yaliyo leak, ni yale majina ya "sadaka" ya "Mkombozi tuu!", no names kwenye "sadaka" ya PAP na no names za big fishes wa "sadaka" za account yake ya Holland!. Threat kubwa kwa JR, sasa ni kutoka kwa hao hao "big fish" recipients, kwa kuhofia asije kuwa harassed too much, akasirika na hatimaye kufungua mdomo!, wanaweza kabisa "kumfunga mdomo" jumla!, kwa kuitumia ile kanuni ya ikibidi punda afe, na afe tuu ili mradi mzigo ufike!, kama usalama wao ni ile "silence yake", silence hiyo ikiwa threatened, kuliko wao kujulikana, bora kumremainisha silent!.

Watanzania wote wenye mapenzi mema na uhai wa binadamu, tuungane kwa sala kumuombea uzima Mzee wetu James Rugemalila, tena kwa ulinzi tuu wa binadamu hatuwezi, tumfungie novena apate ulinzi wa nguvu na uwezo wa Roho Mtakatifu, awe salama, ili siku ya siku ataweza kumulikiwa na ule mwanga mkubwa kama wa Sauli kwenye ile njia ya kwenda Jeriko, mwanga ule ukamfungulia, Sauli akaona mwanga, akanena, akabadilika na kuwa Paulo. Vivyo hivyo tumuombe uzima Mzee wetu James Rugemalila, ili ifike siku na yeye atanena!, ndipo mtaujua ukweli!.

Mimi ni muumini wa "ukweli usemwe!",

Eh Mungu, kupitia Roho Mtakatifu wako, na jesho lote la Malaika wa Mbinguni, mlinde Mzee Wetu, James Rugemalila na majaribu yaliyo mbele yake.

Amen.

Pasco.

Nafikiri kwako wewe ni sula la BEI
 
Mimi pia namwombea sana Mama Tiba lakini tatizo kila anavyozidi kujitetea ndio anaharibu. Angelikubali kuuchuna kama Mh. Chenge na wengine angelifit sana kwenye 'familia' hii badala kwenda tofauti na wanafamilia wenzie.
 
James Lugemalila nilianza kumfahamu siku aliyomfungulia kesi ya kumzuia yule kijana ambaye baada ya kupata vipesa vyake na "kudanganywa" kwamba eti akifanya biashara ya bia za Heinken itamlipa, yule kijana akaingiza kamtaji kake mbuzi akaagiza kontena zake kadhaa za Heineken, akazilipia kodi. Ile anataka kuzipeleka sokoni tu, James Rugemalila kwa kutumia mahakama akamzuia asiuze hata bia moja kwakuwa mwenye haki ya kuingiza na kuuza bia hizo hapa nchini ni yeye, JR tu. Yule kijana akaomba, kama imeshindikana yeye kuuza, basi akamwwomba JR amrudishie gharama zake za manunuzi ili asipate hasara na aangalie biashara nyingine ya kuweza kumfanya alipe ka-mkopo kake alikokachukua benki ili kufanyia biashara. Kama kumkomoa, hata ombi hilo James Rugemalila akalikataa. Yule kijana sijui aliishia wapi?

Leo hii huyu shetani amegeuka malaika wa kugawa hela hivi hivi tu? Tena kwa watu wenye nyadhifa serikalini badala ya kwa Wahitaji?

Lile alilomfanyia yule kijana wa Heinken, Mungu atamlipa hapa hapa duniani
 
Huyo Ruge hakamatwi ktk uhalisia wake... Serikali inafanya maigizo ili kuupoteza kabisa upepo Wa ESCROW na kujenga picha nzuri mbele ya dunia....

Mchezo ni huu: Ruge atakamatwa na kufunguliwa mashtaka pamoja na Seth then serikali itatangazia umma kuwa imechukua hatua ili yasahaulike na wafadhili wafungulie mabilioni ya misaada baas!!!!!

Kitendo cha kukamatwa huyu bwana ni usanii mtupu na nasikia kuna jitihada za kumwondoa singa singa nchini ili kuzima kabisa sakata hili......
 
.asnte Pasco. Kwa mawazo yangu, ili kumnusuru JR, inabidi mwenye kujua majina ya wengine walio na wanaopokea hizo fedha yawekwe hadharani mapemaaaa kweupeee...ili wanaotaka kumzima asiseme washindwe kutimiza haja yao hiiyo. Maana wakitimiza uma utakuwa umewatamhua kuwa ni wao ja WATAHUKUMIWA. Maoni yangu hayo.
 
Wanabodi,

"Wema usizidi uwezo!" ila "wema nao ukizidi, unaweza kukuponza!", Mzee Wetu James Rugemalila, ule wema wake sasa unataka kumponza!. Laiti baada ya kujivutia ule mpunga wake, angejikalia kimya na roho mbaya ya uchoyo, labda yote haya yasingetokea, you never know!. Tumuombe ulinzi wa Roho Mtakatifu, ili yasimkute yale yaliyoimbwa na mwanamuziki, Patrick Balisidya kuwa "Wema Hawana Maisha!", au Hemedi Maneti kuhusu "Waopendwa na Wengi!".

Nimesikia kwa juu juu, kuwa utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Escrow, unatarajiwa kuanza, hivyo ni pamoja na lile azimio la kukamatwa na kutiwa nguvuni kwa Singa Singa wa PAP na Mzee wetu, mwenye huruma, na moyo mwema wa kujitolea na roho nzuri ya ajabu, Mzee James Rugemalila!.

Naomba kwa hapa tuwe wakweli, huyu Mzee akamatwe kwa kosa gani?, amefanya biashara halali ya kuuza hisa zake, amelipwa pesa zake, amelipa kodi za serikali, zilizobaki amegawa kama sadaka au asante kwa aliowachagua, sasa kosa lake ni lipi?!.

Kwa mliofuatilia kisa kizima cha IPTL tangu kuingia kwake, mtakubaliana na mimi kuwa Mzee James Rugemalia amefanya sana "wema", haiwezekani, watu wale wale waliofanyiwa "wema" ule, leo waje wamgeuke na kumtia misukosuko!.

Naomba kukiri, nimekuwa inspired kuandika haya, kufuatia post ya mwana jf huyu.

Kama ni kweli, kamtumia e-mail Mhe rais, mimi ombi langu ni moja tuu, nawaomba sana viongozi wetu, wasiwe wachovu wa fadhila!, wakumbuke walikotoka na jinsi walivyotendewa "wema" na Mzee wetu huyu James Rugemalila!, mimi nakumbuka kuusoma "wema" fulani alioutandaza kipindi cha kukaribia Krismasi fulani!, kuja jitu fulani lenyewe likiitwa Partic Rutabanzibwa, lilikuwa na roho mbaya ya ajabu, hata kuukataa "wema" wa James Rugemalila, lakini wengine wote waliukubali na kuneemeka!. Dawa ya roho mbaya huyo, ilikuwa ni kumuweka pembeni!, IPTL ikapita!, ilipitaje pitaje, na kina nani waliipitisha, na wema upi wa mradi huu, wote wanajulikana, na majina yote ya waliotendewa wema, na ni wema gani, anayo Mzee wetu wa wema, James Rugemalila!.

Haya majina yanayopigiwa kelele, ni majina ya "wema" wa kajibenki kadogo tuu, "Mkombozi", laiti watu wangeyaona majina ya recipients za sadaka za wema wa PAP toka libenki likubwa la Stanbic, au majina ya "wema" mkubwa wa JR kutoka kwenye account yake ya nchini Holland, kuwa transfia "wanene" kupitia Credit Susie!, watu humu wangebaki midomo wazi!. Haiwezekani mtu ufanye "wema " huo wote!, alafu leo uje usumbuliwe na vijitu vidogo vidogo!, mliofanyiwa wema kumbukeni fadhila wajameni, huwezi kutendewa mema ukalipa kwa maovu, hata Mungu hapendi!, mtalaaniwa!.

Kama Mzee wetu huyu, JR, hata baada ya wema wote huo, na bado anasumbuliwa!, mimi ninachohofia sasa, ni uwezekano wa kumyamazisha JR jumla!.

majina yote yaliyo leak, ni yale majina ya "sadaka" ya "Mkombozi tuu!", no names kwenye "sadaka" ya PAP na no names za big fishes wa "sadaka" za account yake ya Holland!. Threat kubwa kwa JR, sasa ni kutoka kwa hao hao "big fish" recipients, kwa kuhofia asije kuwa harassed too much, akasirika na hatimaye kufungua mdomo!, wanaweza kabisa "kumfunga mdomo" jumla!, kwa kuitumia ile kanuni ya ikibidi punda afe, na afe tuu ili mradi mzigo ufike!, kama usalama wao ni ile "silence yake", silence hiyo ikiwa threatened, kuliko wao kujulikana, bora kumremainisha silent!.

Watanzania wote wenye mapenzi mema na uhai wa binadamu, tuungane kwa sala kumuombea uzima Mzee wetu James Rugemalila, tena kwa ulinzi tuu wa binadamu hatuwezi, tumfungie novena apate ulinzi wa nguvu na uwezo wa Roho Mtakatifu, awe salama, ili siku ya siku ataweza kumulikiwa na ule mwanga mkubwa kama wa Sauli kwenye ile njia ya kwenda Jeriko, mwanga ule ukamfungulia, Sauli akaona mwanga, akanena, akabadilika na kuwa Paulo. Vivyo hivyo tumuombe uzima Mzee wetu James Rugemalila, ili ifike siku na yeye atanena!, ndipo mtaujua ukweli!.

Mimi ni muumini wa "ukweli usemwe!",

Eh Mungu, kupitia Roho Mtakatifu wako, na jesho lote la Malaika wa Mbinguni, mlinde Mzee Wetu, James Rugemalila na majaribu yaliyo mbele yake.

Amen.

Pasco.

Mshahara wa dhambi ni mauti, na afe tuuuu; jasho la masikini wa nchi hii kukamuliwa mabili makubwamakubwa ya umeme ili watu wakagawane pesa waonekane wenye heri halikumwagika bure ni lazima litawalambisha watu mauti.
 
Mkuu Amiliki, sipendi binadamu wanaowaita binadamu wenzao mashetani lakini mfano uliotumia kuhalalisha bandiko lako ni zaidi ya relevant. Nakugongea 'like' nyingine 1000.
Huyu Pasco ni mtu mjanja sana, yaani baada ya kuona alikosa mgao wa awali ananyemelea mgao wa sasa ambao ni kwa ajili ya wazee ' kupindisha mambo na kusafisha'
 
Back
Top Bottom