Mswalishaji unamaanisha kuna nchi ama taasisi ya ma-profesa inayoongozwa na mwenye diploma?
1. Kama unamaanisha urais wa nchi; kumbuka kwa kila nchi hasa zile ambazo wachangiaji wengi wanarejea zina mambumbu wengi ambao ndio wapigakura kuliko wasomi kuanzia hiyo diploma mpaka PhD, kwa muktadha...
Tulimchagua kuwa rais wa watanzania hivyo matatizo ya watanzania inatakiwa iwe ni kipaumbele nambari moja kwa rais anayejitambua. Hongera Mh. Magufuli kwa kutambua fika jukumu lako kama rais. Watanzania wenzako wanahitaji msaada wa haraka hivyo safari kwa sasa zikome kwanza. Ukiendelea hivi...
Kama mtu alizoea vya burebure, kweli gap ni kubwa na bado linaongezeka maana zama hizi usipofanyakazi huwezi kula. Tumwache JK ajipumzikie zake msoga. Hapa kazi tuu umbeya kwenu
Mh. DC kasema kitu cha kweli ila hakupaswa kuishia hapo kama kweli analijua tatizo la ajira na changamoto za kujiajiri hasa Tanzania hapa. Maneno ya utumwa na utwana kwa wanaomaliza chuo ni kejeli kwa mfumo wetu wa elimu ambao hautuandai kujiajiri na hakuna mazingira rafiki ya kujiajiri direct...
Duh! Mh. Mbowe waswahili wanasema "Ukitaka kuruka agana na nyonga" wewe mwenzetu twakuona kama mzalendo nambari one kumbe hata kodi halali za serikali hulipi?
Sasa na nyinyi CDM bado tuu mnaendelea na mwenyekiti mwenye questionable integrity waziwazi namna hii? Halafu mnatwambia mmekuja...
Hivi kusema na la haki ni mtalii gani na wa aina gani(wa ndani ama wa nje) aliyenukuliwa kusema VAT inamsumbua na imemkwamisha kufanya utalii? Naamini ni madalali wa utalii ndio wanatusumbua, utalii ni hiari si lazima, ukiona VAT ni mzigo kwenye utalii iepuke kwa kutokuja kutalii kwa sababu...
Nawapongeza TRA kwa kuchukua hatua hizi, in fact fictitious VAT traders ni wengi mnooo hapa nchini. Hatua hizi zikichukuliwa kwa wakati nchi hii ni tajiri na makusanyo ya trilioni 29.5 ya bajeti ya 2016/2017 yatafikiwa.
Yericko uko sahihi kabisaaa. Jambo la kuchangia kwa magari haya madogomadogo na haya ya abiria binafsi naona ni dalili za hujuma kwa wananchi kutoka kwa serikali yao. Kwa msingi huu hakuna unafuu wowote kwa wanakigamboni na watumiaji wa hilo daraja kwa ujumla. hata hizo tozo kwa magari makubwa...
Nawapongeza kwa uchambuzi huu wa wafanyakazi hewa. Tufike pahala tuchambuane hata wafanyakazi mizigo wapo wengi tuu. Kuna watu humu maofisini input yao ni sifuri kazi kuchat na umbea tuu hawa nao ni hewa tuu japo wanatembea.
Ifike pahala tuwe na uwezo wa kupimana kwa tunachomzalishia mwajiri...
Watu hapa tunashindwa kuelewana. Watu wengi tunaliangalia hili bomba na litakachoongeza kwenye pato la Taifa tunaacha kuangalia linaongeza kiasi gani mfukoni kwa tuliowengi. Hata kama hili bomba litaongeza TZS 10bill@day kwenye pato la Taifa, mimi sioni tatizo. Tukumbuke kuwa GDP pekee sio...
Watu tunashangilia hili bomba kupita kiasi utafikiri limetuletea hela ili tuupige teke umaskini. Tuangalie hili la tazama kwanza linaleta faida kwa wangapi kati yetu 50mil watu?
Tusidanganyane, mwarobaini wa umaskini wetu tuliowengi ni kilimo pekee.
Ili kilimo kionekane kinaleta tija kwa taifa...
sasa picha inamtishaje mtu kwa mfano?
waandishi mnapoacha kuandika mambo ya maana na kujikita kwenye majungu na umbea ndio matokeo yake.
Angalau mwandishi angeeleza ni kwa namna gani skuba kapata hekari 5000 (kama ni kweli) badala ya maneno ya ugombanishi tuu aliyoyatumia.
wacha ndg. Rais azibe mianya kwanza. Na hata wewe mleta uzi kama ofisi yako ni ya ujanja ujanja utaifunga tuu maana deal zinaenda kufungwa inabaki haki bin haki.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.