Huyu mtu mnasahau lakini atapata cheo kwa mshangao wa wengi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,858
Huyu si mwingine bali ni bwana ni mwanaharakati fulani.Naona mpaka sasa amejiandalia mazingira mazuri hasa katika sekta ya Bandari anakoonekana kuwa na upeo na utalamu mkubwa katika eneo hilo ingawa pia anaweza kupewa nafasi katika eneo tofauti.

Kama ilivyokuwa kwa bwana Polepole,huyu bwana nae amekuwa akipewa airtime sana Star tv na Channel 10 ila kinachoweza kumuaribia ni msimamo wake kuhusu Katiba inayopendekezwa ambayo ametangaza kuipinga kwa nguvu zake zote ingawa wanaweza kumziba mdomo kwa kumpa cheo

Hata kama ungekuwa ni wewe, ukimsikiliza utashawishika kumpa nafasi pale bandarini atusaidie kudhibiti wizi na upotevu wa mapato ya serikali.Hata hivyo,mtu anaweza kuwa mmuongeaji mzuri lakini akawa mbovu katika utendaji.
 
Atakuwa mzee Mkinga nini? Tena wakati anaongea anachombeza na Jina la Lowassa. kwa kweli kwa hapo Magufuli ni lazima ampe cheo.
 
Renatus Mkinga?

Huyu si mwingine bali ni bwana ni mwanaharakati fulani.. Naona mpaka sasa amejiandalia mazingira mazuri hasa katika sekta ya Bandari anakoonekana kuwa na upeo na utalamu mkubwa katika eneo hilo ingawa pia anaweza kupewa nafasi katika eneo tofauti.

Hata kama ungekuwa ni wewe, ukimsikiliza utashawishika kumpa nafasi pale bandarini atusaidie kudhibiti wizi na upotevu wa mapato ya serikali.Hata hivyo,mtu anaweza kuwa mmuongeaji mzuri lakini akawa mbovu katika utendaji.
 
Back
Top Bottom