MANKA MUSA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2014
- 922
- 1,094
Aidi kuwatia tumbo joto majirani zake.
Sasa atangaza mapambano na yeyote atakayemsogelea.
Na. Mwandishiwa JAMVI LA HABARI.
Ikiwa ni siku mbili tu tangu gazeti hili kufichua michezo miovu ya kutumia majina ya viongozi wakuu wa kitaifa yanauofanywa na mfanyabiashara SCABA SCUBA huku akituhumiwa kuwatisha watu kupitia picha alizopiga na viongozi hao .
Mfanyabiashara huyo amezidi kutamba kwamba hakuna anayeweza kumfanya lolote kwa jambo lolote na kwamba ataendelea kufanya anavyofanya mpaka utawala wa awamu hii utakapomwambia kuwa vinginevyo.
Hayo yametokea ikiwa ni tayari malalamiko yamezidi kutolewa na wananchi kutoka kila kona ya jiji la Dar es salaam na mkoa wa pwani hususani wilaya ya kisarawe ambapo analalamikiwa kupora ardhi kwa kutumia majina ya viongozi.
Taarifa za uhakika zinasema mpaka juzi mchana, tayari SCUBA amekuwa akihaha kuwaza na kupang ni namna gani atadhibiti kuendelea kutoka kwa taarifa hizi.
Wakazi kadhaa wa eneo la kigamboni na kisarawe wamenukuliwa wakisema kuwa karibu kila kiwanja kilichopo eneo hilo ni mali yake.
Juzi na jana gazeti hili liliripoti kuwa Jina la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na lile la waziri mkuu wake Majaliwa Kassim Majaliwa, yameanza kutumika vibaya na na watu mbali mbali ikiwemo wafanyabiashara ili kujipatia mahitaji yao kirahisi JAMVI LA HABARI linathibitisha.
Taarifa za uchunguzi ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha namna watu hao wanaotumia majina ya viongozi wakubwa wakiwemo Rais na waziri mkuu wanavyosababisha usumbufu kwa watu wengine, taasisi za serikali na taasisi binafsi huku kipaumbele chao kikiwa ni kutimiza malengo yao binafsi ama ya kibiashara bila kujali wenzao watajisikiaje.
Katika tukio lililojichukulia umaarufu hivi karibuni ni lile lililofanywa na mfanyabiashara (sharrif) Abdulkadir Scaba Scuba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya amani mkoa wa Dar es salaam kuvamia na kupora ardhi zaidi ya heka 5000 zilizopo kigamboni na yeye mwenyewe kujikabidhi heka elf tatu na heka elfu mbili kuzigawa kwa watu mbalimbali wakiwemo vigogo wa taasisi mbalimbali za serikali.
Taarifa hizo zinaonyesha kuwa SCUBA amekuwa akipita akitamba maeneo mbalimbali ya jiji kuwa kwa sasa hakuna mtu yeyote katika Tanzania hii atakayeweza kumfanya chochote kwa kuwa yeye anamiliki ufunguo wa moja kwa moja kuingia ikulu saa na wakati wowote anapojisikia kufanya hivyo.
Sambamba na kujitapa huko SCUBA anadaiwa kuwatisha watu wote anaoingia nao kwenye mgogoro hasa wa kudaiana mali au anapokuwa kwenye mjadala wowote, huwatisha kwa kuwaonyesha picha zake mbali mbali alizopiga na viongozi hao wa kitaifa.
Miongoni mwa picha anazotambia SCUBA na kuwatishia watanzania wenzake ambao kwa namna moja ama nyingine hawana uwezo wa kufanya kama yeye, ni ile inayomuonyesha SCUBA akiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli picha ambayo ameisambaza pia kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii.
Picha nyingine anayoitumia kuwatisha watu inamuonyesha SCUBA akiwa na waziri mkuu Kassim Majaliwa wakiwa wamesimama ofisini na kuitambia kuwa yeye ni mtu wa kuingia ofisi zote kwa sasa.
SCUBA, kwa kujiamini kabisa, anawatisha watu kwa kuwaonyesha pia picha ya yeye akiwa na waziri mkuu tena, safari hii wakiwa wamevaa kanzu na kofia ikiwa ni ishara kuwa walikuwa kwenye shuhuli ya kidini.
Gazeti hili linafahamu kwamba, ni jambo la kawaida sana kwa viongozi wa kitaifa kupiga picha na watu mbali mbali hapa nchini pindi yanapotokea matukio mbalimbali ya kijamii yanayowakutanisha watu wengi na viongozi wao ambao sio mara kwa mara hukutana.
Rais Magufuli ni miongoni mwa viongozi wengi barani afrika ambao wanapoombwa kupiga picha na mtu hukubali bila kinyongo na mara nyingine yeye mwenyewe huwaambia watu aliokutana nao haya njooni tupige picha (mfano alipotembelea ghafla wizara ya fedha na kuwakuta wafanyakazi wameondoka. Akawaambia waliopo wapige naye picha).
Kitu kinachoshangaza na kuonyesha kutaka kumtumia vibaya Rais na waziri mkuu wake, ni kitendo cha mfanyabiashara huyu kuzitumia picha hizo kama kinga yake ya kibiashara na kuendelea kuwatisha watu kwa simu.
mmoja wa wahanga wa mikwara ya mfanyabiashara huyo amenukuliwa akisema kwao sasa imekuwa ni kero na mateso kiasi cha kutokuamini kama Rais Magufuli analijua hili na kama analiunga mkono.
‘’kwa kweli sielewi kama Rais analifahamu hili, maana yeye mwenyewe anasema ametumwa na Rais na Waziri mkuu. Hivyo hana wasiwasi, lakini siamini kama waziri mkuu au Rais anaweza Kumtuma Kufanya vitu vya namna hii’’. Alisema
Akiongea kwa masikitiko ameendelea ‘’huyu bwana huku kigamboni sasa hivi amefikia hatua mpaka ya kujiita Rais wa huku, ukimuuliza kwa nini anakwambia yeye na Magufuli ni damudamu’’.
‘’Mara anatuonyesha Missed Call ya Rais, Mara ya waziri Mkuu, mara atuulize sisi kama tulishawahi kukutana na Rais ama hata kupiga naye picha?. Kama ni kweli Rais na waziri mkuu wanampigiaga simu huyu bwana basi anafaidi huu sana huu utawala na ndio maana anatutesa’’. aliongeza
Vithibitisho ambavyo gazeti hili linavyo vinaonyesha kwamba SCUBA amekuwa na tabia hiyo na zaidi amekuwa akiwatisha hata polisi kutomchukulia hatua yoyote yanapopelekwa malalamiko dhidi yake na mara nyingi malalamiko hayo hugeuzwa na kuwa mashitaka dhidi ya aliyelalamika.
Katika tukio la kupora ardhi hiyo ya heka 5000, SCUBA anadaiwa kuigawa heka 2000 kwa watu kadhaa mashuhuri hapa nchini ambao gazeti hili lina orodha yao, miongoni mwa watu hao wamo askari polisi, wanajeshi, wafanyakazi wa serikali na viongozi kadhaa wa umma.
Gazeti hili linaendelea na uchunguzi juu ya SCUBA na watanzania wengine wote wenye tabia na mienendo kama yake.
Katika hali ya kawaida ni hatari kwa ustawi wa nchi kwa watu wa tasnia mbalimbali kutumia majina ya viongozi kujinufaisha.
Gazeti hili litaendelea kuuhjuza umma kuhusiana na maswala mbalimbali ikiwemo mahusiano yake na jeshi la polisi anayotamba kuwa hakuna mtu anayeweza kupata haki dhidi yake mahakamani wala polisi.
Jitihada za kumpata mfanyabiashara huyo kuzungumzia suala hili zinaendelea.