Viwango vya gharama daraja la Kigamboni ni uhalifu dhidi ya ubinadamu

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Ama kweli ukistaajabu ya watumishi hewa utayaona ya siasa za sukari Tanzania, Hakika nimestushwa na gharama ya huduma ama niite biashara ya daraja la kigamboni maarufu kama daraja la mzee Julius Nyerere,

Nimestushwa kwakuwa awali mamlaka zilituimbisha zile nyimbo tamu za matumaini ya unafuu wa maisha kwa wa kazi wa jiji kwakuwaondolea gharama kubwa kwenye pantoni na foleni na kisha kuwapa kilichoitwa "huduma" ya daraja.

Katika moja ya maamuzi ya mamlaka nikuwa waenda kwa miguu watapita bure, hilo ni jambo zuri, lakini ni ukweli kuwa kijiografia hakuna mwananchi atakayepita kwa miguu eneo hilo la daraja hasa mazingira yake ni hatarishi kwa wapita njia hasa nyakati za usiku. Yani ni umbali wakilomita moja isiyo na makazi wala shughuli za kibiashara ni vigumu mtu wa kawaida kupita kwa miguu eneo hilo.

Baskeli imepangwa kulipiwa 300 hii haina tofauti na ilivyo sasa kwenye pantoni
Pikipiki ni shilingi 600 hii inazidi 100 ukipita kwenye Panton ambako tulizoea kulipa 500.
Magari madogo mpaka pick up ni 1500 hadi 2000 sawa na sasa ukitumia Pantoni.

Daladala Hiace abiria 15 ni shilingi 3000, hii ni mara mbili na ilivyo kwenye pantoni ambako hulipia 1500/2000
Basi la abiria kuanzia watu 29 na kuendelea litalipiwa shilingi 7,000 (Haya ndio mabasi yaliyopewa vibali vya kutoa HUDUMA ya kusafirisha umma kupitia daraja hilo.

Sasa ndugu zangu naomba twende katika namba ili tujue daraja hili ni HUDUMA au ni BIASHARA?

Basi la abiria mfano UDA linabeba watu 40, hivyo daraja 7000 ÷ 40= Abiria 15..

Hivyo katika kila basi litakalovuka hapo abiria wake 15 watalipia daraja......

Mabasi ya Feri Kariakoo/Machinga Complex kwa siku yanafanya safari kumi.

Hivyo kila basi la abiria kwa siku liyavuka mara kumi kwenye daraja na litalipa 7000 × 10= 70000

Hesabu ya mabasi ya hayo kwa tajiri kila siku ni 120,000... Jiulize kwa siku basi hilo litapatafaida gani kwa kuhudumia wananchi wa kigamboni kupitia daraja hilo?

Binafsi nilitaraji huduma hii ya uvushaji watu kwa mabasi yote yaliyosajiriwa iwe bure kama ilivyo bure kwa waenda kwa miguu, ama iwe uchangiaji kidogo usiozidi angalau elfu moja (1,000/=) ili kusaidia uokozi dhidhi ya adha hii ya usafiri kwa wanadarisalamu.

Ni tajiri gani atakaepeleka gari yake katika eneo ambalo atafanya kazi ya kuilipa serikali tu bila kupata faida?

Matokeo yake hapa ni kuwa tutaraji ukosefu ama uhaba wa mabasi toka Feri hadi katikati ya jiji na viunga vyake yanayotumia daraja hilo.

Hii ni hujuma dhidi ya wananchi wa Kigamboni na wakazi wa jiji ambao ndio watumiaji wakuu wa daraja hilo kwa njia ya mabasi.

Serikali ishirikiane na wadau wote wa usafurishaji na watumiaji katika kuweka viwango vya gharama za "huduma" hii kwakuwa sio biashara kama inavyotafsiriwa sasa.
FB_IMG_1462909070002.jpg
 
Una hoja ya msingi kabisa. Mimi sikuwa nimeona ilivyo gharama kwa wasafirishaji wa abiria! Umenifungua macho! Hili ni la kufanyia kazi mara moja (kama serikali itasikiliza) Mabasi ya abiria yanaweza kuwekewa tozo za mwezi, mfano waambiwe walipe sh elfu 5 au 10 kwa mwezi. Vinginevyo ni gharama sana!

NB: Nadhani ingekuwa vizuri vile vile kama wangeweka ''seasonal pass'', kwa mfano mkazi wa Kigamboni mwenye gari binafsi awe na pass ya mwezi au wiki itakayomruhusu ku-cross kadiri anavyotaka. Wanaweza wakamlipisha sh 20,000 ka mwezi halafu yeye kila napopita anaonyesha pass. Hakuna mantiki ya kumtoza kila anapopita darajani kwani kwa siku mtu anaweza kujikuta anakwenda mjini hata mara tatu.
 
Sasa mi mfanyakazi napita hapo kwenda na kurudi,ina maana nitatakiwa kulipa 60,000 kwa mwezi?mmh bado mafuta ya gari 150,000 kwa mwezi,pango nalokaa 70,000,umeme na maji 30,000,makato ya kodi ya serikali 315,000,motorvehicle inabidi nikusanye 25,000 kila mwezi ili mwisho wa mwaka nilipie,hapo bado sijala wala kuvaa plus dharura za hapa na pale!mmmh hakuna akiba
 
Ama kweli ukistaajabu ya watumishi hewa utayaona ya siasa za sukari Tanzania, Hakika nimestushwa na gharama ya huduma ama niite biashara ya daraja la kigamboni maarufu kama daraja la mzee Julius Nyerere,

Nimestushwa kwakuwa awali mamlaka zilituimbisha zile nyimbo tamu za matumaini ya unafuu wa maisha kwa wa kazi wa jiji kwakuwaondolea gharama kubwa kwenye pantoni na foleni na kisha kuwapa kilichoitwa "huduma" ya daraja.

Katika moja ya maamuzi ya mamlaka nikuwa waenda kwa miguu watapita bure, hilo ni jambo zuri, lakini ni ukweli kuwa kijiografia hakuna mwananchi atakayepita kwa miguu eneo hilo la daraja hasa mazingira yake ni hatarishi kwa wapita njia hasa nyakati za usiku. Yani ni umbali wakilomita moja isiyo na makazi wala shughuli za kibiashara ni vigumu mtu wa kawaida kupita kwa miguu eneo hilo.

Baskeli imepangwa kulipiwa 300 hii haina tofauti na ilivyo sasa kwenye pantoni
Pikipiki ni shilingi 600 hii inazidi 100 ukipita kwenye Panton ambako tulizoea kulipa 500.
Magari madogo mpaka pick up ni 1500 hadi 2000 sawa na sasa ukitumia Pantoni.

Daladala Hiace abiria 15 ni shilingi 3000, hii ni mara mbili na ilivyo kwenye pantoni ambako hulipia 1500/2000
Basi la abiria kuanzia watu 29 na kuendelea litalipiwa shilingi 7,000 (Haya ndio mabasi yaliyopewa vibali vya kutoa HUDUMA ya kusafirisha umma kupitia daraja hilo.

Sasa ndugu zangu naomba twende katika namba ili tujue daraja hili ni HUDUMA au ni BIASHARA?

Basi la abiria mfano UDA linabeba watu 40, hivyo daraja 7000 ÷ 40= Abiria 15..

Hivyo katika kila basi litakalovuka hapo abiria wake 15 watalipia daraja......

Mabasi ya Feri Kariakoo/Machinga Complex kwa siku yanafanya safari kumi.

Hivyo kila basi la abiria kwa siku liyavuka mara kumi kwenye daraja na litalipa 7000 × 10= 70000

Hesabu ya mabasi ya hayo kwa tajiri kila siku ni 120,000... Jiulize kwa siku basi hilo litapatafaida gani kwa kuhudumia wananchi wa kigamboni kupitia daraja hilo?

Binafsi nilitaraji huduma hii ya uvushaji watu kwa mabasi yote yaliyosajiriwa iwe bure kama ilivyo bure kwa waenda kwa miguu, ama iwe uchangiaji kidogo usiozidi angalau elfu moja (1,000/=) ili kusaidia uokozi dhidhi ya adha hii ya usafiri kwa wanadarisalamu.

Ni tajiri gani atakaepeleka gari yake katika eneo ambalo atafanya kazi ya kuilipa serikali tu bila kupata faida?

Matokeo yake hapa ni kuwa tutaraji ukosefu ama uhaba wa mabasi toka Feri hadi katikati ya jiji na viunga vyake yanayotumia daraja hilo.

Hii ni hujuma dhidi ya wananchi wa Kigamboni na wakazi wa jiji ambao ndio watumiaji wakuu wa daraja hilo kwa njia ya mabasi.

Serikali ishirikiane na wadau wote wa usafurishaji na watumiaji katika kuweka viwango vya gharama za "huduma" hii kwakuwa sio biashara kama inavyotafsiriwa sasa.
View attachment 346699

Umeanzisha hii thread kwa mwelekeo ule ule wa kupinga tu kila kinachofanywa na Serikali ambayo inaongozwa na chama ambacho hukukipigia kura....nchi zote makini zinatumia mtindo huu wa malipo .
 
Yericko uko sahihi kabisaaa. Jambo la kuchangia kwa magari haya madogomadogo na haya ya abiria binafsi naona ni dalili za hujuma kwa wananchi kutoka kwa serikali yao. Kwa msingi huu hakuna unafuu wowote kwa wanakigamboni na watumiaji wa hilo daraja kwa ujumla. hata hizo tozo kwa magari makubwa na magari mengine pia ni kubwa mnoo. Wananchi tunalipa kodi, tunachangia NSSF kunanini tena NSSF kugeuka mfanyabiashara kisa daraja kajenga?
Serikali iilipe NSSF madeni ya ujenzi wa daraja hilo ituache wananchi kutunyonya mara mbilimbili maana sasa huu ni unyonyaji wa wazi kabisa. Kwa mantiki hii foleni hata ile ya mbagala tusitegemee kupungua hata kidogo
 
Back
Top Bottom