UPDATES 21 April 2016: Bandari ya Tanga ndiyo chaguo la serikali ya Uganda

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

==============
UPDATE 2:

Leo Thursday, 21 April 2016, 11:10 hrs.

Mawaziri wa Nishati wa Uganda na Tanzania wamemaliza kikao chao cha kupitia na kuthibitisha, "Minutes, Recommendations na Conclusions" za chaguo bora (Tanga Port) la ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi. Wawakilishi wa serikali ya Kenya wamechelewa na wamekuta kikao kimeisha.

Taarifa za Kikao cha Mawaziri zinapelekwa kwa Waheshimiwa Wakuu wa Nchi zetu. TUTASHINDA.

==============

UPDATE 1:

20.04.2016

Taarifa za hivi punde zinataarifu kuwa Waziri Prof Muhongo na jopo la wataalam wameingia Uganda jana usiku kwa ajili ya kikao cha Mawaziri wa Uganda, Tanzania na Kenya kukamilisha chaguo la Uganda la kutumia Bandari ya Tanga kusafirisha Mafuta Ghafi yake na ya nchi nyingine za Afrika Mashariki (EAC). Pia serikali ya DRC nayo itatumia Bomba hili litakalopita Kaskazini mwa Tanzania hadi Bandari ya Tanga.

Serikali ya Uganda itatoa tamko la chaguo la Bandari ya Tanga siku ya Ijumaa, 22/04/2016
 
Hivi kwa nini tunashangilia sana hili bomba la mafuta kama vile ndiyo muarobaini wa umasikini wetu? Bomba la mafuta la TAZAMA llimepita hapa nchini lakini bado sisi ni mafukara sasa sijui hili la Uganda lina tofauti gani na hili la TAZAMA,labda nielimishwe!
 
kuna hela nyingi sana mkuu hapo ukiachilia ajira etc
 
Hivi kwa nini tunashangilia sana hili bomba la mafuta kama vile ndiyo muarobaini wa umasikini wetu? Bomba la mafuta la TAZAMA llimepita hapa nchini lakini bado sisi ni mafukara sasa sijui hili la Uganda lina tofauti gani na hili la TAZAMA,labda nielimishwe!
Ngoja na Bomba la Sewage/Mavi waliielekezee huku tutafurahia tuu hivi hivi!
 
Hivi kwa nini tunashangilia sana hili bomba la mafuta kama vile ndiyo muarobaini wa umasikini wetu? Bomba la mafuta la TAZAMA llimepita hapa nchini lakini bado sisi ni mafukara sasa sijui hili la Uganda lina tofauti gani na hili la TAZAMA,labda nielimishwe!

Boss,

Nina uhakika nikikuambia unionyeshe "nyama" kwenye mwili wako iliyotengenezwa kutokana na chakula ulichokula siku ya mwaka mpya 2016 hautaweza kuiona. Lakini nina uhakika chakula hicho (sawa na vingine ambavyo unakula kila siku) kimechangia sehemu fulani katika afya uliyonayo..

Vivyo hivyo hakuna fursa yeyote ya uchumi unayoweza kusema ndio "mwarubaini" wa matatizo yetu yenyewe kama yenyewe, lakini kwa umoja wa fursa mbalimbali tunajikongoja.

Kwa namna moja fedha ambazo zitaingizwa nchini kugharamia ujenzi na uendeshaji wa hilo bomba zinapitia mifukoni mwa watanzania, jambo ambalo litachangia sehemu fulani ya "afya" ya uchumi wetu...
 
Watu tunashangilia hili bomba kupita kiasi utafikiri limetuletea hela ili tuupige teke umaskini. Tuangalie hili la tazama kwanza linaleta faida kwa wangapi kati yetu 50mil watu?
Tusidanganyane, mwarobaini wa umaskini wetu tuliowengi ni kilimo pekee.
Ili kilimo kionekane kinaleta tija kwa taifa, serikali ijikite kwenye miundombinu (maeneo yote hasa wanakozalisha bidhaa za kilimo na mijini kwenye soko la bidhaa hizo) ya usafirishaji(barabara, reli, usafiri wa majini, na anga), Upatikanaji wa nishati ya uhakika, Mawasiriano, Upatikanaji wa maji, Kilimo cha umwagiliaji na mifumo ya utunzaji hasa wa bidhaa za kilimo.
Haya mengine ni muhimu ila binafsi naona tija yake kwa waliowengi ni kidogo sana.
 
Uchumi wa nchi unaundwa na "Sekta" nyingi. Sekta moja haipunguzi umuhimu wa sekta nyingine. Kilimo ni muhimu kwa uchumi wetu lakini hakipunguzi umuhimu wa bomba la mafuta linalopendekezwa. Kama wewe fani yako ni kilimo komaa huko huko. Kuna watakaofaidika na bomba la mafuta.
 
Umenena vizuri sana mkuu...nakupa. HEKO
Boss,

Nina uhakika nikikuambia unionyeshe "nyama" kwenye mwili wako iliyotengenezwa kutokana na chakula ulichokula siku ya mwaka mpya 2016 hautaweza kuiona. Lakini nina uhakika chakula hicho (sawa na vingine ambavyo unakula kila siku) kimechangia sehemu fulani katika afya uliyonayo..

Vivyo hivyo hakuna fursa yeyote ya uchumi unayoweza kusema ndio "mwarubaini" wa matatizo yetu yenyewe kama yenyewe, lakini kwa umoja wa fursa mbalimbali tunajikongoja.

Kwa namna moja fedha ambazo zitaingizwa nchini kugharamia ujenzi na uendeshaji wa hilo bomba zinapitia mifukoni mwa watanzania, jambo ambalo litachangia sehemu fulani ya "afya" ya uchumi wetu...
 
Hivi kwa nini tunashangilia sana hili bomba la mafuta kama vile ndiyo muarobaini wa umasikini wetu? Bomba la mafuta la TAZAMA llimepita hapa nchini lakini bado sisi ni mafukara sasa sijui hili la Uganda lina tofauti gani na hili la TAZAMA,labda nielimishwe!
...Watu wanashangilia kwa sababu waKenya wamekuwa wanaringa na kudharau watu humu. Its a "gotcha" moment. That is, likipita kwetu.

...Sio muarobaini wa umasikini wetu, ndio. Lakini bado kutakuwa na manufaa fulani, ambayo yashaongelewa kwa kirefu humu.

...La TAZAMA linatua Dar, hili Tanga. A plus to Tanga Port.

...Ume elimishwa!
 
Hivi kwa nini tunashangilia sana hili bomba la mafuta kama vile ndiyo muarobaini wa umasikini wetu? Bomba la mafuta la TAZAMA llimepita hapa nchini lakini bado sisi ni mafukara sasa sijui hili la Uganda lina tofauti gani na hili la TAZAMA,labda nielimishwe!
Mkuu kwani tunaposema Bandari ya Dar pekee inachangia zaidi ya 60% ya pato la taifa unafikiri ni mizigo peke yake??

Bomba la Uganda linaongeza zaidi ya Trillioni 1 kwenye pato la taifa, kwa nini usishangilie??

Au hujui faida ya bomba hili moja ni sawa na viwanda 30 ndani ya nchi yako??
 
Kwa namna moja fedha ambazo zitaingizwa nchini kugharamia ujenzi na uendeshaji wa hilo bomba zinapitia mifukoni mwa watanzania, jambo ambalo litachangia sehemu fulani ya "afya" ya uchumi wetu...
...Na cha muhimu ni local content katika mradi, kwenye materials, human resource, n.k.
 
Watu tunashangilia hili bomba kupita kiasi utafikiri limetuletea hela ili tuupige teke umaskini. Tuangalie hili la tazama kwanza linaleta faida kwa wangapi kati yetu 50mil watu?
Tusidanganyane, mwarobaini wa umaskini wetu tuliowengi ni kilimo pekee.
Ili kilimo kionekane kinaleta tija kwa taifa, serikali ijikite kwenye miundombinu (maeneo yote hasa wanakozalisha bidhaa za kilimo na mijini kwenye soko la bidhaa hizo) ya usafirishaji(barabara, reli, usafiri wa majini, na anga), Upatikanaji wa nishati ya uhakika, Mawasiriano, Upatikanaji wa maji, Kilimo cha umwagiliaji na mifumo ya utunzaji hasa wa bidhaa za kilimo.
Haya mengine ni muhimu ila binafsi naona tija yake kwa waliowengi ni kidogo sana.
Mkuu, huoni faida ya bomba linaloingiza zaidi ta Tshs Billioni 4 kwa siku kwenye pato la taifa??

Are you serious??
 
Hivi kwa nini tunashangilia sana hili bomba la mafuta kama vile ndiyo muarobaini wa umasikini wetu? Bomba la mafuta la TAZAMA llimepita hapa nchini lakini bado sisi ni mafukara sasa sijui hili la Uganda lina tofauti gani na hili la TAZAMA,labda nielimishwe!
Hili la Uganda likikamilika litakua linapitisha mafuta ghafi pipa laki 2 kwa siku, kila pipa tutalipwa kati ya USD 10-15.piga hesabu hapo. Hili la TAZAMA labda mkataba wake ni tofauti kwakua linatoa mafuta kutoka nje kwenda Zambia baada ya kupakuliwa kutoka melini lkn la Uganda ni mafuta wanayoyachimba wenyewe na yanapita kwetu kwenda kuuzwa kwenye soko la Dunia.
 
Back
Top Bottom