Hakika jambo hili linasikitisha na kufikirisha sana. Jana nilikuwa na mtu akasema, hivi kwanini Lisu anahangaika, si atulie yeye na familia yake? Nilimtazama kwa hasira, kisha nikamwambia, nchi yetu inaangamia kwa sababu ya ukimya wa watu kama yeye. Nikaondoka. Tunahitaji kubadilika kifikra.