Yah! Nakubaliana na wazo la Walimu kuboreshewa mishahara inaweza ikasaidia. Japo kwa upande mwingine "SHIBE NI MWANA MALEVYA". Wakati fulani inaweza ikawa ni tamaa ya maslahi tu.
Kwa ushauri wangu, Walimu tupunguze KUKOPA, na badala yake tuishi kulingana na kipato chetu. Wapo wanaopata kima...
Si yeye tu, kwa sasa kila mtanzania anatakiwa kusoma alama za nyakati na kutetea mstakabali wa Taifa letu; Dalili za KIFO cha uzee ni maradhi ya mara kwa mara. Hiv ndiyo hali ya CCM ilivyo. Maana kila lenye mwanzo halikosi mwisho, tuachane na kufanya mambo kwa MAZOEA
Tupende tusipende, huu ni wakati wa kuchunguza TUNAPOTAKA KUJIKWAA kabla hatujafika hatua ya kuulizana pale tutakapodondoka. Salama yetu ni MUNGU PEKEE. Tumrudie yeye ili aweze kutukinga na kimbunga kunachotuandama
Viongozi wetu bado wanautumia ule usemi wa "MTOTO AKILILIA WEMBE MPE" pale wanapoamua kukaa kimya huku wakishuhudia matukio yanayohatarisha amani hapa Nchini. Huo usemi haupaswi kuzingatiwa katika hili.
Tumechoshwa na AMANI tunajidanganya kufikiri kuwa VURUGU zitatuacha pazuri. Ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha anapinga vikali UDINI unaoendelea kushika kasi kila kukicha. MUNGU tusaidie.....!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.