Hii ndiyo mikakati ya CHADEMA kuingia Ikulu 2015

Jangakuu

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
513
221
MAPEMA wiki hii Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilifanya mikutano yake mikuu kikiwa na lengo kujipanga kuingia Ikulu mwaka 2015.

Chama hicho kinachounda kambi rasmi ya upinzani Bungeni kinapewa nafasi kubwa ya kuleta ushindani mkali katika uchaguzi wa mwaka 2015 katika nafasi za rais, ubunge na udiwani hasa kutokana na ushindani ulioonekana mwaka 2010 na utekelezaji wa operesheni zake zinazovuta maelfu ya wananchi.


Katika mikutano hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti, mkutano wa kwanza ulishirikisha Kamati Kuu ya chama hicho pamoja na wabunge, lengo likiwa ni kuongeza nguvu ya kiuamuzi kutokana na wao kuwa karibu na wananchi.

Kulikuwa na wajumbe 356 kati ya 400 kutoka Tanzania bara na Visiwani ambao ni sawa na asilimia 86 huku wakimpokea rasmi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Laurence Tara na kukabidhiwa kadi ya chama hicho.

Tara aliwahi kuwa Diwani wa Babati Vijijini Mkoani Manyara kwa awamu tatu mfululizo na Mbowe alimtaka kurudi kuhakikisha anaendeleza harakati zake za kisiasa akiwa Chadema.


Mashambulizi sasa kwa kanda
Akieleza mikakati ya chama hicho ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikifanya mikutano ya vuguvugu la mabadiliko (M4C), Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ametangaza mkakati wa mashambuzi nchi nzima kupitia kanda 10.

Amezitaja kanda hizo 10 akisema kuwa zitakuwa mwarobaini wa utawala wa CCM kuanzia mwakani wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa ni
Kanda ya Ziwa Magharibi aitakayojumuisha mikoa mitatu ya Mwanza,Geita na Kagera.
Kanda ya Ziwa Mashariki itajumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga. Kanda ya Magharibi itakuwa ni Kigoma,Tabora,Katavi na Rukwa.


Kanda zingine ni Kanda ya Kati itakayokuwa na mikoa ya Singida, Dodoma na Morogoro.Kanda ya Nyanda za Juu Kusini itakuwa ni Iringa, Njombe, Mbeya na Ruvuma.
Kanda ya Kusini itakuwa ni Lindi na Mtwara. Kanda ya Mashariki itakuwa Dar es Salaam, Pwani na Tanga. Kanda ya Kaskazini itakuwa Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Kanda ya Pemba itajumuisha mikoa yote ya Pemba na Kanda ya Ugunja itajumuisha pia mikoa yote iliyoko Unguja.

Mbowe amesema kuwa kanda hizo zitatumika kuandaa wabunge na madiwani watakaoshiriki katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 lakini pia uchaguzi wa mwakani wa Serikali za Mitaa.


“Hapa naweza kusema mwaka huu tayari ni mwaka wa nguvu ya umma na tunachokitaka kila mmoja ni kutekeleza wajibu wake ipasavyo,” anasema Mbowe na kuongeza:
“Kuna baadhi yao wamekuwa wakitumiwa na CCM kuhakikisha inatugombanisha sisi viongozi na wanachama, sasa natangaza kwamba atakayebainika kutugombanisha tutamchukulia hatua kali na kuendeleza mapambano kama kawaida,” anasema kwa msisitizo.

Mbowe anasema harakati za kuingia Ikulu zinahitaji kujipanga na kupanga mikakati madhubuti ya kujijenga kuanzia matawi hadi taifa.
Anaendelea kwa kusema kuwa ymbali na kusimamia mienendo ya chama pia kitafanya majukumu ambayo yalikuwa yakifanywa awali na makao makuu.
Kila kanda itakuwa na ofisi yake ambayo itakuwa na hadhi kama ofisi yetu ya makao makuu na huko ndiko tutafanikisha azima ya nguvu ya umma” anasema Mbowe na kuongeza:
“Tutapeleka magari, pikipiki na vitendea kazi ili kuhakikusha mwaka 2015 tunaing’oa CCM madarakani na kushika dola” anasema.

Mwenyekiti huyo hakuishia hapo, bali anasema kuwa CCM ikishirikiana na Serikali yake kupitia kanda hizo haitakuwa tena na uwezo wa kuzuia M4C isifanyike kama inavyofanya hivi sasa.
Anasema ukitaka kufanya M4C hivi sasa utasikia visingizio kibao lakini viongozi wetu wa kanda watakuwa na uwezo wa kuratibu shughuli zote kama kawaida.

Tume ya Uchaguzi
Wakati chama hicho kikiweka mipango hiyo kabambe, bado kina hofu ya kukwamishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikiwa kwa kutokuwa huru wala kutenda haki hasa kwa vyama vya upinzani.

Mbowe anasema kuwa endapo katika mabadiliko ya katiba hakutakuwapo na kipengele cha kuwapo kwa Tume Huru ya Uchaguzi hawataingia katika uchaguzi utakaofanyika mwaka 2015 kwani tume hiyo yenye uongozi ulioteuliwa na rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM haina sifa ya kuwa huru.

“Tunaiomba Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhakikisha inakizingatia kipengele hicho ili tuweze kufanya uchaguzi uliokuwa wa haki na kutokuegemea upande wowote” anasema Mbowe. Malalamiko hayo ya Chadema yamekuja wakati tayari Nec imeshatoa maoni yake kwenye ya Katiba ikitaka viongozi wake wasiteuliwe na rais kama ilivyo sasa. Je, hilo litapitishwa?


Muungano
Akielezea Muungano ambao unatakiwa kuwapo ili kutoa mianya kwa kila upande kuweza kunufaika anasema muungano wa Serikali tatu ndiyo suluhisho.

Mbowe anasema hakuna sababu ya kung’ang’ania muungano wa Serikali mbili huku Wazanzibari wakitaka kuwa na Zanzibar huru, tuwe na uhuru wa kuamua tukipendacho.
“Chadema hatupingi Muungano hata siku moja ila tunachotaka ni kuona Muungano unakuwepo wa Serikali tatu na usiokuwa wa kulazimishana” anasema na kuongeza:

“Tunataka Tanganyika yetu huru na wao wawe na Zanzibar kwani wana Bendera na Wimbo wao wa taifa, Serikali yao, Katiba, Rais pamoja na Makamu wake sasa kipi ambacho tunataka” anasema Mbowe.

Katiba Mpya
Akielezea mchakato wa kukusanya maoni ya kuandikwa kwa Katiba Mpya, Tume inatakiwa kuhakikisha inakuja na Katiba inayokidhi matakwa ya wananchi.
Mbowe anaendelea kusema kuwa Katiba ni jambo moja na kuipitisha ni jambo jingine, hivyo bila katiba bora tutaipinga.
 
Wel program,na naamini things will go as it was planned na magamba lazima wakae chini na kupiga kelele za maumivu
 
Back
Top Bottom