Kikwete: Sina tatizo na uwepo wa Serikali tatu Tanzania!

Wananchi wapi anaowazungumzia zaidi ya wale waliokuwa presented kwenye data za Warioba ?. Kumbuka alihoji uhalali wa data za Warioba ! Labda hao wananchi ana maana ni viongozi wa CCM !

Na vile vile alisema kama mnataka serikali tatu subirini kwanza mimi niondoke !

Bado tu hujaona undumilakuwili wake ?
Kilo ndilo jibu ameshalitoa. Kwamba ngoja amalize kula muwa wake akiondoka haoni faida muwa huo haumhusu. Sio mara moja kalisema hilo, hukumbuki aliwaambia wanaccm kwenye mkutano mkuu fulani kwamba hataki ccm ivunjikie mikononi mwake? Mpaka wakamsusia kukampeni kpindi chake cha pili kwa sababu walishamshitukia, ndio maana ya 24% ya kura za watanzania wote zilimpa ulaji wa pili. Leo kakuambia wazi kwamba subiri amalize ndio Tanganyika ije maana ikija leo itatengeneza Katiba ambayo huenda itampokonya haki ya kunyonyonga aliyoizoea na kutakiwa achinje badala yake naye hajui kuchinja au kuna tija ndogo kibinafsi. Nilimsikia katika kipande kilichorushwa akiwa London anawambia hawakuitumia vizuri mitandao ya kijamii kumwambia Warioa kwamba na uraia wa nchi mbili uwepo asilaumiwe katika minong'ono iliyopo kuwa ameingilia mchakato ila ni maoni yake tu.
 
Anawajua wauza dawa za kulevya. Ana majina kama 40 ya waua tembo. Hamjui mmiliki wa Dowans. Anawajua wezi wa EPA na aliwaomba warudishe walichoiba.

Hapa kinyonga pale mjusi. Leo mamba kesho kenge. Tanzania Chui London Kondoo.......
....

Aiseee
 
Ameenda kusemea mbali akijua huko ataonekana ni mwana demokrasia katika nchi yake. Angesemea hapa maccm wenzake wangemmeza. Arudi sasa aje arudie akiwa hapa aone hiyo ngoma.
 
nimemsikiza vizuri mwanzo kati na mwisho. amenikumbusha vituko vya Aden Rage na wana-Simba alipowaita mbumbumbu hadharani na baadae kuwaomba radhi hapohapo hadharani na wao wakaendelea kumchekea. Jakaya kafanya hayohayo kwa ma-CCM

saisi huyu kamuona mnyika dhaifu
 
JK akiwa London amesema maamuzi ya wananchi ndiyo yatakayoheshimiwa kwa sababu kama wananchi wataamua basi CCM wajiandae hizo serikali tatu.

Pia amesema alishawashauri CCM kwenye vikao vya ndani wajiandae kupokea hiyo serikali tatu kama wananchi wataamua.

Inaonekana CCM ni wabishi sana na JK alishaona serikali tatu hazikwepeki.
Kwa hiyo kama JK ameongea huko UK kuwa kama wabunge wa bunge la katiba watapitisha rasimu ya serikali 3, basi wananchi wajuandae kuupokea.

Hiyo itakuwa na maana JK aliyepiga mkwara kwenye bunge la katiba kuwa msimano wake yeye na chama chake cha CCM, ni serkali 2, na akaapa kuwa serikali 3 hazitakuwepo wakati yeye yuko madarakani, kama mfumo huo wa serikali 3 ndiyo wanaoutaka wananchi, basi wasubiri yeye aondoke madarakani ndipo waulete mfumo huo.

Je sasa anachotaka kutuambia kuwa JK aliyewapiga mkwara wajumbe wa katiba hakuwa yeye, bali aliletwa mtu pale bungeni kuhutubia, anayefanana naye?!
 
Ingekuwa heri akarudi tena Bungeni kueleza alichoeleza London, na kutangaza rasmi kuwa alichoandikiwa na kukisoma Ijumaa ilopita anakifuta. Aweke wazi bila kumung'unya maneno.
 
Tusiwaamini wanasiasa.

Haswa wanasiasa wa Tanzania maana hawaamini katika sayansi na teknologia. Wamaabudu uwongo, na vitu vya siri siri na ujanja ujanja na kulindana wanapotenda maovu, vitu visivyokua na tija kwa Taifa.
 
Hakuna tofauti, tatizo wanachadema ikiwa pamoja na wewe hamuelewi neno "demokrasia". Elimu ya uraia inahitajika zaidi.

Kwa kukusaidia ni kwamba alichosema Bungeni ni jinsi yeye anavyoamini kuwa serikali Mbili ndio njia muafaka kwa maendeleo ya watanzania. Alichosema London ni kwamba kama wananchi wataamua serikali tatu, yeye atayakubali maamuzi ya wananchi na atafanya kazi nao kwa maendeleo ya Tanzania. Kiswahili kigumu au demokrasia ni ngumu.

Mfano hai: Uchaguzi mkuu 2010 CHADEMA waliamini kuwa Raisi ajae katika uchaguzi huo atakuwa mtu anayeitwa " Dr Slaa". Lakini wananchi wakasema vinginevyo na kumpeleka ikulu Kijana anayeitw "Kikwete". CHADEMA WAKAsema hawatafanya nae kazi. Ingekuwa kama ndio Slaa amechaguliwa ,Kikwete angepanda jukwaani na kusema nimekubali maamuzi ya wananchi na nitafanya kazi na Slaa. Hivi huu ndio undume la kuwili.

Du CHADEMA mnaniacha hoi. Jamani mtaharibu nchi.
Kwa hiyo unachotaka kutuambia ni kuwa JK aliyetamka kwenye bunge la katiba kuwa kamwe hataruhusu ujio wa muundo wa serikali 3 akiwa bado yupo madarakani, siyo JK huyo aliyetamka Uingereza kuwa kama wananchi wa Tanzania uamuzi wao ni kuwa na serikali 3 basi nchi haina budi kuupokea!!
 
Anawajua wauza dawa za kulevya. Ana majina kama 40 ya waua tembo. Hamjui mmiliki wa Dowans. Anawajua wezi wa EPA na aliwaomba warudishe walichoiba.

Hapa kinyonga pale mjusi. Leo mamba kesho kenge. Tanzania Chui London Kondoo.......
....

...Kiongozi umikosea Londoni Kondoo Chui Bongo na siyo ulivyosema...
 
Sasa atakapoondoka si kitiba mpya itakuwa imepatikana? Itakuwa ipi ya serikali mbili au tatu?
 
Back
Top Bottom