WALIMU: No 'big result now' without 'big salary now'!

WALIMU: No 'big result now' without 'big salary now'!

Kufundisha nimfundishe mie, mtihani nimpe mie, misifa apate yeye!!! Utoro afanye yeye sifuri apate yeye, lawama nipewe mie!!! Mibangi avute yeye, nidhamu akose yeye BIG RESULT NOW nifanye mie!!! MAJANGAAA! MAJANGAAA! ONA MAJANGAAA ! ONA MAJANGAAA. ONE Tuzitoe sie wataalamu tuwafundishe sie, mishahara mikubwa wapate wao!!! MAJANGAA! MAJANGAA! ONA MAJANGAA! ONA MAJANGAA!! Jumapili njema mwalimu
 
Katika mazingira magumu km haya wamekuja tena na kitu kinaitwa ophras sijui hopeless hawa watawala sijui wa karne gani kwani ni upuuzi kumbana mwalimu ambaye maslahi yake ni duni hata ukimbana hana kitu cha kupoteza

Mkuu, hapo penye red nadhani ulikuwa unamaanisha Open Performance Review and Appraisal System (OPRAS). Kuna nini kibaya dhidi ya OPRAS? au mlizoea kuwa evaluated kwa kupitia mafaili yenu tu?
 
Matokeo makubwa sasa bila mikakati ya muda mrefu ni upumbavu mkubwa,hiyo pesa ya semina wangenunulia madawati huko vijijini ambako magogo yanavunwa lakini bado wanakaa chini,

1)Shule ziwe na mazingira ya kusoma kweli
2)Mitaala ya masomo irekebishwe
3)Walimu wapewe wanachokidai
4)Wazazi watimize wajibu wao
5)Vijijini kupewe nguvu ya ziada kubadili hali ya elimu

Tofauti na hapo tusubiri hili janga lifike elimu ya juu muda siyo mrefu

Afadhali umeliona na hili, sio mishahara tu inayohitaji kuangaliwa!
 
Hivi hapo Kinondoni Mtaa wa Ufipa hicho kiasi mnacholipwa kinatosheleza kukidhi mahitaji yenu muhimu?

mkuu Lusewa, waliokutuma waambie kuwa this time walimu hatutaandamana lakin tutaonana kwenye matokeo.
Serikal boreshen mishahara ya walimu, lipen malimbikizo yote na stahiki zote, boreshen mazingira ya kufundisha na kujifunzia.
Kama sio hivyo jipange kufanya extreme standardization in the near future.
 
waalimu mtapewa incentives kama Tv sets na madaftari,vijijini shule ina waalimu 3 na watoto wanakalia mawe mishahara yenyewe kama mikia ya mbuzi alafu nasikia waalimu wanaapa pia ...this is shameless poor results now
 
Katika mazingira magumu km haya wamekuja tena na kitu kinaitwa ophras sijui hopeless hawa watawala sijui wa karne gani kwani ni upuuzi kumbana mwalimu ambaye maslahi yake ni duni hata ukimbana hana kitu cha kupoteza

headmaster wangu alikuja na hilo likitina la öphras akatuambia tusome nilichofanya nikwenda kutupa kwenye makabati mpaka leo sijui liko wapi.
 
Lol, hawa waalimu nao wana-overestimate umuhimu wao. Ukweli ni kwamba walimu hawa ukiwapa mtihani wanaofanya wanafunzi wao, wao na wanafunzi wao watapata marks zinazofanana. Na ndiyo maana wapo kwenye matatizo waliyo nayo. Tanzania, kwa bahati mbaya imetoka kwenye hatua ya kuwa na walimu wazuri kwenye shule za serikali, na walimu wazuri wote wapo kwenye shule binafsi. Mimi nimesoma wakati ambapo kusoma shule ya serikali ilikuwa ni sifa kuliko kusoma shule binafsi. Na shule yangu ya serikali (Tanga school) ilikuwa ikizikanyaga shule nyingi sana binafsi, kama siyo zote. Lakini sasa wakati umebadilika na shule binafsi ndizo zimekuwa bora kuliko za serikali. Sasa katika uchumi/soko huria, kama wewe mwalimu unadhania wewe ni mwalimu mzuri na unastahili malipo mazuri, sasa kwa nini unafundisha shule ya serikali? Kama hakuna shule binafsi inayokutaka, basi ujue kwamba ualimu wako siyo bora kuliko unavyofikiria. Inawezekana mshahara unaopewa ndiyo unaostahili.
 
jamani ndugu zangu waalimu tukae chini tujiulize. hivi kufundisha vizuri kunahitaji mishahara mikubwa(Big Salary)? Wengine mna watoto wenu wa kuwazaa huko shuleni kama mimi. Mnataka kuniambia mnawafundisha vizuri kuliko wengine? na wana BRN?. Nilidhani mimi na wengine tuungane kuiomba serikali itusaidie tujue mbinu za kufundisha kwenye mazingira haya haya tuliyonayo!!
 
Kule ulaya watoto wanafundishiwa nyumbani shule wanaenda kucheza na wenzao na kufanya mitihani. Wewe je wamfundihsa mwanao BGR usisome imba bongo fleva then iba mitihani faulu then ajiriwa then BGR saSA iba ujenge nyumba mapema nk.
 
Yah! Nakubaliana na wazo la Walimu kuboreshewa mishahara inaweza ikasaidia. Japo kwa upande mwingine "SHIBE NI MWANA MALEVYA". Wakati fulani inaweza ikawa ni tamaa ya maslahi tu.

Kwa ushauri wangu, Walimu tupunguze KUKOPA, na badala yake tuishi kulingana na kipato chetu. Wapo wanaopata kima cha chini cha mshahara wa Serikali lakini wanaonekana ni nafuu kuliko walimu. HIVI KWELI MTU MWENYE MSHAHARA WA 500,000/= ANAKOPA HADI UNABAKI NA TAKE HOME YA 10,000/= tukubaliane naye anapoilaumu serikali? Tuwe wakweli; mishahara iongezwe, lakini na ninyi WALIMU PUNGUZENI KUKOPAAAAAAAAAA! Vinginevyo hata mkipewa Mil. 10 kwa mwezi, mtakopa na tatizo litabaki lilelile

Nikirudi kwenye "Big result now" ninapata shida kidogo, maana MPANGO WOWOTE MZURI WENYE MATOKEO MAKUBWA NA MAZURI HAUWEZI KUWA HARAKA. "Matokeo makubwa sasa" ni upande mmoja, je Uzuri/ubora wa hayo matokeo umezingatiwa?
 
"The way you treat your EMPLOYEE is the way they treat your CUSTOMERS, there is no big result now without big salary now"
huo ni ujumbe unaosomeka katika sms zinazo sambaa kwa walimu.

Mimi kama mwalimu naunga mkono hoja kwa 100% kwan hamna Taifa imara bila walimu madhubuti na wanao thaminiwa, kueshimiwa.

Teaching is the mother of all profesionals in the world.
Teachers can either build a strong or weak country.
Cry my beloved country! governed by Slogans & Catch phrases, Siasa ni Kilimo, Mkurabita, Mkukuta, Kilimo kwanza now enter BIG RESULTS NOW! its for Wabunge tu! poor teachers shall have to wait a long long time.
 
"The way you treat your EMPLOYEE is the way they treat your CUSTOMERS, there is no big result now without big salary now"
huo ni ujumbe unaosomeka katika sms zinazo sambaa kwa walimu.

Mimi kama mwalimu naunga mkono hoja kwa 100% kwan hamna Taifa imara bila walimu madhubuti na wanao thaminiwa, kueshimiwa.

Teaching is the mother of all profesionals in the world.
Teachers can either build a strong or weak country.

serikali ya ccm hawana lengo la kuwapa raia wake elimu thabit wakihofia wakielimisha watawatoa madarakani kwa maovu yao
 
Kufundisha nimfundishe mie, mtihani nimpe mie, misifa apate yeye!!! Utoro afanye yeye sifuri apate yeye, lawama nipewe mie!!! Mibangi avute yeye, nidhamu akose yeye BIG RESULT NOW nifanye mie!!! MAJANGAAA! MAJANGAAA! ONA MAJANGAAA ! ONA MAJANGAAA. ONE Tuzitoe sie wataalamu tuwafundishe sie, mishahara mikubwa wapate wao!!! MAJANGAA! MAJANGAA! ONA MAJANGAA! ONA MAJANGAA!! Jumapili njema mwalimu

mkuu mwombe mhusika ukatoe rimix
 
Back
Top Bottom