Wewe ndugu,una hasira sana na Dr. Slaa,angalia usije ukamshambulia ukapitiliza baadaye tukashindwa kuamini hata ukweli utakaosema.
Kwanza siamini kuwa udaktari wake ni 'fake'kama ulivyosema,kwani sidhani kama una ushahidi.Yapo mapungufu yake yaseme hayo akiweza ajirekebishe kama huyaoni hayo...
Si wabunge tu,nchi haina watu kwani kama sisi ni watu kwa vigezo vya utu tusingewapeleka hawa watu kusimamia mambo yetu.Sasa naamini hawa ni 'sample' yetu, hivyo wanawakilisha tabia yetu sie tuliowachagua.Kwani hata mimi badala ya kuchukua hatua itakayofanya watu hawa wawajibike naishia kuandika...
Sasa jamani Tz hii itaongozwa na akina nani baada ya hawa wazee kung'atuka kwa namna yoyote ikiwa vijana tunawatilia shaka?
Nawapenda hawa vijana kwa namna mara nyingi wanavyojenga hoja.Ni kweli hawako sahihi kwa kila jambo,lakini ningependa tuwasaidie badala ya kuwa'critisize' kama ni watu...
Kama zimeongezwa bila idhini yake, ikulu haioni kuwa imedhalilishwa?
Nadhani ingekuwa hajaidhinisha asingenyamazia kubezwa kwa kiasi hicho,vinginevyo rais wetu anadharauliwa sana na wasaidizi wake kitu ambacho ni kibaya huenda kuliko hata kuidhinisha posho ambayo anataka kunawa mikono kuwa...
Kweli kuna watu wengine wameridhika.Hivi kama matatizo umeyakuta si ndio kazi uliyoomba ya kuyaondoa?Hata angekuwa Slaa yuko Magogoni kama hali ingekuwa hivi angeulizwa 'ee Bwana unakotupeleka ndiko ulikoahidi?'
Hata hivyo sikulaumu mitizamo tunatofautiana na hata namna ya ku'react'.
Kosa la Zito sijaliona kwa wazi kama huyu jamaa anayejiita eti ni mbunge anavyo'address'.Nadhani ni vizuri angekuwa wazi kuwa yeye ni 'ant-Zito' tangu zamani na alikuwa akitafuta mahali ambapo atateleza ili aweze 'kumnanga', lakini bahati mbaya kwake 'timing' yake imekuwa mbovu, amejaribu kuvuka...
Nakubaliana na wanaosema kuwa ajali ya mh.Regia haikutokana na ulemavu wake bali ni kulipita gari mahali ambapo hapakustahili na hili linawatokea wengi na kwakweli linatupotezea wapendwa wetu wengi.
Ni kweli pia haipendezi kumjadili marehemu lakini kama tunaweza kujifunza kitu kutokana na...
Zito uko sawa,mara nyingi huwa nakukubali.Watu kukuongelea kuwa unapenda kugombea urais kupitia CDM ni dalili kuwa wanahisi una uwezo na wala sidhani kama ni kosa mtu kuwa na malengo kama hayo suala ni taratibu zizingatiwe na mtu akitaka kuteuliwa na chama chake asionekane kuwa anataka kukigawa...
Ni masikitiko makubwa kwa watanzania,ingawa kufa ni lazima lakini ni ngumu kukubali kwa binti mdogo kama huyu hata hivyo itoshe tu kuwa mapenzi ya Mungu yametimia.Upumzike kwa amani-Amen!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.