Huyu jamaa anafaa kuwa rais wa nchi hii lakini tatizo ni dini yake tu. Sijui kama atapewa maana watu wa dini yake hawatakiwi kushika huo wadhifa na wakiushika moto wake si mchezo. Hupigwa vita kila kona.[/QUOTE"
Hapana,sikubaliani na wewe kuwa dini ya mtu ndiyo inayofanya Rais asikubalike.Mimi naamini kushindwa kuongoza kwa ufanisi au vinginevyo hakutokani na dini yake.Watanzania tuache kuficha udhaifu wetu kwa kisingizio cha dini.
Kikwete kapigiwa kelele kwasababu ya kushindwa kwake kuyafikia matarajio ya wananchi aliyowaahidi yeye mwenyewe na chama chake na siyo dini yake.
Nakumbuka awamu yake ya kwanza alipendwa na watanzania wengi na alichaguliwa kwa zaidi kidogo ya 80% ya kura zote Je,watu hawakuijua dini yake?
Kipindi kilichofuata akapata kama 61% ya kura akiwa na dini yake hiyohiyo,kwahiyo kwa mtazamo wangu dini ya mtu si kigezo cha kuwakatisha tamaa watu wenye uwezo wa kuwatumikia watanzania,Zito akiwa mmoja wao na wapiga kura wataamua kwa jinsi watakavyompima katika utendaji wake.
Kwa maelezo haya nadhani inajulikana kuwa namkubali Zito kwasasa nikimlinganisha na wengine.