Pinda na Makinda wampa changamoto Kikwete. Je watajiwajibisha au kuwajibishwa?

Kwani ni wangapi wanaiunga mkono CCM? UCHAKACHUAJI wa kura ndio unaowaweka madaraka. Suluhisho, tutafute mbinu ya kulinda kura na si vinginevyo.
 
MKUU. Sisi Watanzania ni mabwege tokea zamani. Ndivyo tulivyolelewa tangu enzi za Mwalimu.
 
Siri ya posho mpya yafichuka (Toka Tanzania daima)
Hata hivyo, hatua ya serikali ya Kikwete kubariki posho mpya ya sh 200,000 kwa siku imemwokoa Spika Makinda ambaye alikuwa anakabiliwa na tishio la kung’olewa na wabunge.Habari ambazo gazeti hili limezipata zilisema kuwa baada ya Makinda kuonekana kama vile ameshindwa kutimiza ahadi yake ya mara kwa mara kwa wabunge kwamba angeongeza posho, baadhi ya wabunge, tena kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM),walipanga kuibuka na hoja ya kutokuwa na imani na Spika.
Inaelezwa kuwa hoja hiyo ilipangwa kuibuliwa na mmoja wa wabunge machachari wanawake wa CCM na kuungwa mkono na wengi ambao walionekana kukerwa na Makinda kushindwa kusimamia maslahi ya wabunge kama alivyoahidi. Mmoja wa wajumbe kutoka Kamati ya Bunge aliliambia gazeti hili kwamba tayari Spika alishawapa matumaini kwamba posho zimeongezwa, hivyo asingeeleweka kama angesema posho hazijaongezwa kwa sababu Rais hajasaini. “Unakumbuka Spika alipokurupuka na kupingana na katibu wake kuhusu posho, CCM ilitoa taarifa kupinga nyongeza hiyo kama makundi mengine yalivyofanya. Mama alilalamika kwamba chama kimemtosa.“Hata hivyo aliahidiwa kwamba serikali ingemlinda. Ndiyo maana Rais amebariki posho mpya kabla ya kuanza kikao hiki cha sita, hivyo amezima mpango wa mahasimu wa Makinda,” alisema mjumbe huyo ambaye ni mmoja wa wabunge machachari wa CCM.
 
Kutunza heshima yao kwa jamii kuna haja ya kustep down
Yaani hata wewe nae unaamini kwamba JK hajaidhinisha wabunge kulipwa posho mpya? hivi JK mpaka atawale miaka mingapi ndio mtamjuwa tabia yake? kwahiyo na wewe mpaka leo unaamini kwamba JK hawajui wamiliki wa Richmond/ Dowans?
Mnasikitisha sana.
 
Hata kama ameidhinisha au hajaizinisha, lakini kwa kauli zinazopingana, somebody lazima awajibike hapa, na kwa hili hawezi kuwa JK, should be Pinda and Makinda.

Ntakuwa wa kwanza kushangaa kama wabunge hawatakomalia hili kama walivyokomaa kwa Lowassa. Pinda anatakiwa kujipima mwenyewe ktk hili.
 
Hata kama ameidhinisha au hajaizinisha, lakini kwa kauli zinazopingana, somebody lazima awajibike hapa, na kwa hili hawezi kuwa JK, should be Pinda and Makinda.

Ntakuwa wa kwanza kushangaa kama wabunge hawatakomalia hili kama walivyokomaa kwa Lowassa. Pinda anatakiwa kujipima mwenyewe ktk hili.
Hivi huwa mnatumia angalau sekunde kutafari kabla ya kupost humu? posho wameongezewa wabunge kama walivyokuwa wanahitaji akiwemo Joseph Selasini na Magale Shibuda, sasa unataka wakomalie lipi? mbona huweleweki?
 
hali inavyoendelea sasa ni yakusikitisha sana....wachambuzi wa mambo wanaona kuna hali ya kutoelewana kati ya mihimili miwili ya uongozi yani spika wa bunge na rais akiunganishwa na waziri mkuu anae link pande zote mbili yani bunge na serikali....nini kinachoendelea sasa katika ishu ya posho? Makinda anamtuhumu rais kua alibariki,pinda nae uku rais akikanusha habari hizo...katika hali km hii inaonekana dhahiri kuna hali ya kuchokana,kutokuheshimiana na mwishowe km hali itaendelea kua hivi kila upande utaanza kukomoana hasa bunge kwa kukomalia ishu km za richmond,epa nk....nini ata ya haya yote?:a s 465:
 
Hizi ni ndoto za mchana.... labda useme kwamba ungekuwa Rais kitu ambacho ukitia nia unaweza kuupata.... lakini unaposema ungekuwa JK sikuelewi!


Hapa ni tatizo tu ama la uelewa au la matumizi ya lugha vinginevyo usingehoji.....jambo la msingi hapo sio jina bali ni kuangalia muktadha....kwamba hapo JK amesimama kama mwana wa b/moyo au rais wa nchi...!!
 
JK ndie mnafki.. Yalianza kwa Jairo, mchakato wa Katiba, yamekuja kwenye posho.. Ni rais wa kusoma upepo unaenda wapi..
 
Kweli hii nchi sasa haina mwenyewe:

-Spika wa Bunge, Anne Makinda: “Siyo kwamba tutaanza kutoa, tulishaanza kutoa na Rais (Jakaya Kikwete), ameshatoa kibali chake.

-Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu: Hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

-Pinda: Tayari Rais Kikwete alikuwa ameidhinisha ongezeko la posho za vikao.

-Zitto Kabwe: Taarifa nilizonazo ni kwamba Rais Kikwete alikuwa hajasaini kuidhinisha posho hizo.


Jibu sahihi ni.................................??**

**=Fill in the blanks
 
Kitabu cha Guinness kiko wapi jamani ili hii Idiotian government iingizwe kwenye record ya serikali ya kustaajabisha zaidi duniani!
 
Nchi imechoka,kama serikali hii itatuvusha basi naamini hakuna serikali yoyote itakayokuja itakayoshindwa-Hii ndiyo 'margin' yetu.
 
Posho za wabunge

Licha ya wanachi waliowengi kulalamikia kitendo cha wabunge kujiongezea posho, lakini wawakilishi hao wa wananchi bado wameweka pamba masikoni bila aibu wameshikilia tama zao za fedha bila kuwajali waliowachagua na jana 31 jan 2012 Waziri Mkuu mh Mizengo Pinda akatangaza kuwa posho hizo zimeongezeka naye Spika wa bunge akathibitisha kuwa rais Jakaya Kikwete ameshasaini muswada wa posho na sasa ni sheria kuwa wabunge walipwe posho hizo mpya wanazodai. Kwa hesabu za haraka haraka kwa mwaka mmoja tu posho za wabunge (ukiondoa mishahara yao, posho za vikao vya kamati, posho za semina wakati wa wikiend, gharama za mafuta, mchango wa maedeleo ya jimbo) zinafika karibu bil. 12,474,000,000/=. Hapa nimechukua wastani wa siku mia moja wanazotakiwa kukaa bungeni kwa mwaka mzima( wiki 3 mwezi February, wiki 3 mwezi April, wiki 3 mwezi October na siku 72 kwenye bunge la bageti mwezi June ukatoa wikiendi zote). Hizi ni gharama za vivuko viwili kama cha mv. Magogoni. Hapa najiuliza hawa wabunge wanania ya kweli kumtetea mwananchi?




1. Mikael P Aweda


GHARAMA
Safari ya mwisho ( safari ya 322) ya Davos iliigharimu Serikali Tsh mil 300. Nikiamu kuchukua theluthi mbili ya gharama hizo - yaani mil 200, kisha nikazidisha kwa idadi ya tripu 322. Jumla yake ni 64,400,000,000. Mabilioni haya ni mengi sana. Ukizigawa mil 50 ambazo ndio gharama ya kujenga zahanati mmoja kwa wastani, utapata jumla ya Zahanati 1288. Zahanati hizi ni sawa na idadi ya siku alizokaa nje ya nchi Rais wetu(refer red above).
Pili,Kiasi hiki hizi zingetosha kuweka Zahanati kwenye zaidi ya 50% ya kila kata nchi nzima. Nchi yetu ina kata 2000 na kidogo. Ikumbukwe kuwa Tz wanawake wajawazito kati 24 hadi 36 kwa siku wanakufa kwa sababu kadhaa ikiwepo kutokuwepo kwa zahanati au ziko

Kuna jamaa wawili wamechambua gharama za wabunge na Rais kama ilivyo hapo juu.

Kama hizo ni estimates ziko karibu na ukweli sioni ni jinsi gani JK atakwepa kupandisha hizo posho. JK ametumia zaidi ya 64 Billion kwa safari za nje tu wakati wabunge posho zao ni around 12 Billion (8 x less za JK ndani ya miaka 6). Mimi naona tatizo hapa ni wabunge tu na JK hajui namna ya kuucheza huu mchezo.................. Wenzake wanamtegea bomu.
 
Back
Top Bottom