Siyo kweli kwamba Zitto na Makamba wanawahurumia watanzania, wana ajenda zao

Status
Not open for further replies.
Si kweli kwamba lengo la Januari makamba na zito kabwe kuhusu hoja zao binafsi wanazotajia kutoa bungeni ni kutokana na huruma yao kwa watanzania… kama ambavyo wao na wapambe wao wanavyotaka ionekane bali wanataka ku- divert attention ya watanzania kutoka kwenye masuala muhimu yanayogusa maisha na ustawi wa taifa.

Hii haina maana kwamba hoja hizo si za muhimu! La; lakini ikilinganiswa na masuala kama vile mabadiliko ya sheria ya maandalizi ya katiba mpya, sula la ufisadi, hususani lile la Jairo na wenzake, sula la bei ya umeme, na ufisadi wa EPA, Richmondo/Dowans n.k, hoja za wapangaji, mkonge na huduma za kibenki zinaweza kusubiri au kufanyiwa kazi kwa njia zingine ikiwa kweli wana nia na lengo la kuboresha maeneo hayo.

Hii ni strategic plan ya ‘Mafia’(soma mafisadi) wa Tanzania waliojaa serikalini ambao wanaona kila siku zinaibuka hoja zinazowatishia amani, wameamua kuwatumia hawa vijana, ili waingize hoja ambazo wanadhani zitameza hoja za msingi ambazo watanzania wamechoka kusubiri ufumbuzi wake kutoka serikalini.

Ili vyombo vya habari na bunge watumie ‘air time’ ya kutosha kujadili hoja hizo at the expense ya hoja za msingi zaidi zinazotakiwa kupewa kipaumbele.

Nawasihi wanaharakati, wapambambanaji, na wote wanaoitakia mema taifa hili, wasipoteze muda kwenye hoja hizi, na niseme tu sina imani na hawa watu kutokana na wanaowazunguka na mienendo yao huko nyuma, sina shaka kwamba hata hoja hizi zikipita, sheria ikatungwa kukabiliana na masuala hayo, hali itabadilika- uongozi wetu upekuwepo na unaona jinsi kilimo cha mkonge kinavyokufa hawafanyi lolote, Zito atawapa nini wazinduke na kufanya yanayotakiwa kufanywa ili kuendeleza zao hilo,

Labda cha msingi wangekuwa wanapendekeza tuwaondoe madarakani viongozi na serikali ambayo haionekani kufanya lolote, wakati kilimo cha mkonge kinakufa, au haichukui hatua yoyote kukomesha unyonyaji wa wenye nyumba na mabenki na vyombo vya fedha.

Maana siyo kwamba hizo ni hoja mpya zimejadiliwa vya kutosha na watu mbalimbali, na tafiti mbalimbali zimefanywa kwa gharama za kodi ya wananchi lakini serikali hii na viongozi hawa hawa wanaopelekewa hoja hizihizi na zito na januari, hawakufanya lolote, wako bisy na mambo yao ya kukwapua rasilimali za umma.

Hivi kwanini watanzania kwa sasa tunaugua sana ugonjwa wa kutoamini tunayoyaona bali kuona tunayoyaamini tu?
 
Wakuu posho za wabunge ni cha mtoto. Kuna miposho inalipwa hadi mtu unaogopa. Kwa wazo la zito la kuzianhalia posho kwa ijumla wake ni jema kabisa.
 
Mtoa mada una point, vilaza wengi hawataweza kukuelewa, zitto na makamba hakuna lolote, wao ni game za kisiasa tu.

Sasa jamani Tz hii itaongozwa na akina nani baada ya hawa wazee kung'atuka kwa namna yoyote ikiwa vijana tunawatilia shaka?
Nawapenda hawa vijana kwa namna mara nyingi wanavyojenga hoja.Ni kweli hawako sahihi kwa kila jambo,lakini ningependa tuwasaidie badala ya kuwa'critisize' kama ni watu hatari(hilo siamini sana ingawa inawezekana-'Never say never').
 
Wakuu posho za wabunge ni cha mtoto. Kuna miposho inalipwa hadi mtu unaogopa. Kwa wazo la zito la kuzianhalia posho kwa ijumla wake ni jema kabisa.

Hakuna anayeunga mkono posho, wala si Zitto na Makamba pekee wanaozipinga
 
Zitto ana vyanzo vya income vingi tu hivyo hawahitaji hivyo vijisenti vya bungeni.lakini kwa mmbunge wa kawaida ambaye hana source nyingine yoyote ya income kweli anastahili kuongezewa posho.

Zitto ana vyanzo vya income vingi???????? Vipi hivyo? Au unataka tu kujaza server?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom