Waziri Kivuli wa Afya na Ustawi wa Jamii Gervas Mbassa akomalia mgomo wa madaktari bungeni kwa kutaka Bunge lieleze ni kwanini taarifa ya serikali haipo kwenye ratiba ya bunge. Mbassa aliomba muongozo huo kutokana na maelekezo yaliyotolewa jana na Spika kufuatia hoja ya dharura iliyoanza iliyotolewa na Zitto Kabwe naibu kiongozi wa upinzani bungeni. Katika maelekezo yake Spika alielekeza kwamba kabla ya hoja hiyo ya Zitto tayari Spika alishakubaliana na serikali iwasilishe kauli kuhusu mgomo wa madaktari. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge akitoa maelezo ya nyongeza kufuatia maelezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Bunge George Simbachawene alisema kwamba serikali itawasilisha kauli yake katika siku itakayopangwa na Spika. Mfululizo huu wa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani kuhoji kuhusu suala hilo kunaelekea kuwa ni utekelezaji wa tamko lilotolewa na CHADEMA kwamba Chama kimewasiliana na kimeitaka kambi rasmi ya upinzani bungeni inayoongozwa na CHADEMA kufanya uchambuzi wa kina kuhusu maelezo hayo na kutumia njia za kibunge katika kuisimamia serikali kushughulikia migogoro kati yake na madaktari, maslahi ya watumishi wa umma katika sekta ya afya pamoja na uboreshaji wa huduma katika hospitali, zahanati na sekta ya afya nchini.
Serikali ya wajanja imejaa ujanjaujanja kama wa kina Lukuvi, kukwepesha mambo na changamoto za msingi za nchi si njia ya kutatua matatizo ni bora masuala haya yangejadiliwa wazi na kwa mapana yake ili kufikia ufumbuzi kamili, ukimya, ukwepaji wa changamoto si njia sahihi kutatatua masuala kama haya. JK shtuka, ngoma inazama mkuu........:hatari:
Nchii hii hatuna Bunge, ila tunakundi la wanasiasa wa chama tawala na waupinzani wakiwa pamoja.
ivi lukuvi kaishia levo gani ya elimu?kwan kuna kauli ya serikali na kauli ya mawaziri?au anadhani serikali inaongozwa na nani akiondoa mawaziri?pia kwel govt iko serious mpaka leo kimya?madaktari ebu ungana tena kieleweke.