Miaka yote iliyopita walikuwa na sababu gani ya kutowekeza mpaka sasa ndio wasingizie kusita? Au zamani walikuwa wanakuja kuwekeza lakini sasa wanakimbia? Hainiingii akilini
Na huyo kahaba ni mwanaume? au ni kifaa cha mapenzi tu? sasa iweje mchafu awe mwanaume wakati huyo kahaba ni mwanamke? kwa nini usiseme kwanza wanawake ni wachafu sana kwa kufanya ukahaba kulala na wanaume wengi? au useme kwa ujumla bila kutupia lawama wanaume peke yake?
Jitambue mkuu, wanaowapa ujauzito ni watu wazima na akili zao timamu, ili kuwasaidia hao watoto ni kuacha upumbavu wa kushiriki nao kingono halafu unakuja kutetea upumbavu wa kuwaendeleza kielimu baada ya kuwajaza mimba... Jitambue, ndio maana tukiitwa wapumbavu tunakuja juu kumbe tunapumbazana...
Ukinunua hisa IPTL na wewe unakuwa umehujumu uchumi? Kama hao SIMBA TRUST wamenunua hisa tu watakuwaje watuhumiwa? Basi kama ni hivyo hata wote wenye hisa ACACIA pia ni wezi
Ningekuwa mimi ndio mkuu wa mkoa wa Arusha ningeahirisha kukarabati hiyo hospitali na kuwapa hizo familia hizo pesa... Hakuna sababu ya kugombania pesa hiyo kwa sababu kama ni ukarabati unaweza kuanzisha harambee zikapatikana kwa njia nyingine au hata kupata ruzuku kutoka serikalini... Na...
Kama wameamua kuwashtaki basi wawashtaki na askari wa usalama barabarani ambao waliona hilo kosa lakini hawakuwachukulia hatua. Isiwe baada ya ajali ndio wanamtafuta wa kumbebesha lawama wakati wahusika ni wengi. Au ina maana njia yote hiyo kutoka Arusha mpaka walipofikwa na ajali hakukuwa na...
Jibu muafaka ni kwamba swali halijitoshelezi, kasema kufika, je ni kufika wapi? je kama pikipiki safari yake mwisho ni kilometa 50 baada ya hapo na basi ni 100 si wa pikipiki atakuwa kafika anakokwenda kabla ya basi? na je kama basi liliondoka asubuhi pikipiki ikaondoka jioni yake? si basi...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.