Nataka kwenda Australia kutafuta maisha

Ivindo

Senior Member
Feb 11, 2016
168
239
Wakuu baada ya kumaliza chuo miaka kadhaa na kuhangaika kupata masters degree naona bado future yangu haiko salama ikiwa nikiwa naishi hapa Tz. Kupata mshahara wa 950,0000 na allowance ya 600,000 kila mwezi naona inaishia kuishi maisha ya hand to mouth. Sasa umri unaenda, na hakuna cha maana kinafanyika, na mzee Magu amebana mno hata hakuna deal kabisa, naomba msaada wa ushauri tu kwa wale wenye uzoefu wa Australia, na sio kwingine au kutoa kejeli zisizojenga kwani.

Mpaka nimefikia uamuzi huo wa kwenda huko kwa wazungu kwa sababu nina jirani yangu hapa alikwenda akasoma (Bachelor of nursing na akawa registered nurse), na bahati nzuri akapata PR na anafanya kazi ya nursing salary yake kwa saa ni aud 59 (90,000 tsh) na weekend (sunday) ni aud 118/hr (180,000 tsh). Expenditure zake ni aud 500/week rent, groceries ni aud 150-200/week, gas aud 70-80/week.

Haki ya nani huyu dada anajenga bonge la ghorofa hapa jirani, pamoja na kuwa amenipa clues tu chache na kuona positivity yake bado naomba michango yenu.

Asante sana, nikifanikiwa nitarejea kutoa ushuhuda
 
Tafuta shule uondoke kwa baraka, mwajiri wako aendelee kuwa na mategemeo ya wewe kurudi. Ili ukienda mambo yakawa ndivyo sivyo urudi uendelee na mambo mengine. Huyu mdada umuulize vizuri imemchukua muda gani kufika hapo alipo? Na je wewe unategemea kufika hapo alipo baada ya muda gani? Dadisi details zote zikiwemo backups plans kama mambo yataenda sivyo.

Tunakoelekea bongo ndo huko huko, kila kitu kitakuwa tight na matumizi yasiyokuwa ya lazima yatakoma. Hakuna tena dili za hovyo hovyo au kuvizia vizia lazima kila mtu afanye kazi na apate anachostahili kulipwa. Siyo mtu unalipwa 1.5m, unagawana na watu kama 10 wakati wanaweza wakafanya kazi wakalipa kodi, wakajipatia riziki zao wenyewe.
 
Nurses huko kwa wenzetu mnahitajija kama lulu, tena tafuta kazi sehemu ngumu ngumu kama nyumba za wazee,nk. Nenda mkuu tuache sisi tuendelee kupigwa na wagonjwa kisa nimezalisha katoto kamekufa, wakati mama mjamzito alienda kliniki Mara moja, kaswende hakupimwa maana vitenganishi hakuna na hapa labour ward taa hakuna tunazalishia mwanga wa mshumaa...
 
Ushauri mzuri sana mkuu

Mtoa mada asisahau kuleta mrejesho siku akianza kunyanyua ghorofa
 
Ondoka haraka, Nchi hii hao Kama Magu hata wawe 10 hawawezi kubadilisha maisha ya Watz, watu wanaishi kwa "Hope and Dreams" mpk Mauti yanamkuta. Wenzetu kule tayari kila kitu kumewekwa juu ya meza mpk miaka 1000 Mbele.

Australia Na Canada Ndio Taifa Lililo zuri kwa sekta ya Ajira mpk saivi Hapa Canada Nursey analipwa mpk Can 35 kwa saa.
 
Kibongo bongo Mpaka unamaliza bachelor na masters haraka haraka unachezea 29-30 years. okay lets say unaenda Australia kusoma hadi kuwa certified na kuingia kwenye mfumo wa ajira rasmi miaka 8-10. Hapo utakuwa na miaka 40 tayari. Huoni kwamba hiyo miaka 10 ungewekeza hata kwenye kilimo cha biashara ungetoka kirahisi tu kuliko kwenda kujitaabisha na maisha ya kusikia. Tatizo la watanzania hawasemi kwa namna gani wanapigana kufikia walipofika ila wanakuelezea tu mafanikio yao. Kweli nursing inalipa ila huwezi kufika tu Na kufikia mafanikio.
 
Bongo kua nesi ni aibu kwa mwanaume
 
mkuu kama kweli unataka utusue maisha tafadhali nenda katika nchi zifuatazo Shelisheli Ipo Africa,st Vincent And Grenadies,british Virgin Island Zipo Marekani Kaskazin Bila Kusahau Cape Verde Nakuhakikishia Ukirud Baada Ya Miaka Miwili Kama Hujajenga Magorofa Matatu Kwa Mpigo Mimi Fala..
 
Nurses huko kwa wenzetu mnahitajija kama lulu, tena tafuta kazi sehemu ngumu ngumu kama nyumba za wazee,nk. Nenda mkuu tuache sisi tuendelee kupigwa na wagonjwa kisa nimezalisha katoto kamekufa, wakati mama mjamzito alienda kliniki Mara moja, kaswende hakupimwa maana vitenganishi hakuna na hapa labour ward taa hakuna tunazalishia mwanga wa mshumaa...
Yamenigusa.
 
Kibongo bongo Mpaka unamaliza bachelor na masters haraka haraka unachezea 29-30 years. okay lets say unaenda Australia kusoma hadi kuwa certified na kuingia kwenye mfumo wa ajira rasmi miaka 8-10. Hapo utakuwa na miaka 40 tayari. Huoni kwamba hiyo miaka 10 ungewekeza hata kwenye kilimo cha biashara ungetoka kirahisi tu kuliko kwenda kujitaabisha na maisha ya kusikia. Tatizo la watanzania hawasemi kwa namna gani wanapigana kufikia walipofika ila wanakuelezea tu mafanikio yao. Kweli nursing inalipa ila huwezi kufika tu Na kufikia mafanikio.

Ni kweli Binti Magufuli
Huyo dada ni mid50, alikwenda akiwa 45 mwaka 2007 alisoma kwa miaka 3 akamaliza ndipo akaajiriwa (kwa sababu ukimaliza tu degree=registered nurse). So ameajiriwa akiwa na miaka 48, lakini mafanikio aliyopata in 5years ni zaidi ya miaka 25 alofanya kazi Bongo. Mimi nimeshafanya kazi miaka 10 kama ofisa wa serikali, sasaivi nina miaka 35 (10 yrs less than her).

Sina sababu ya kushindwa, pia nilishaenda kwa miezi mi3 ila sikupata exposure ya miji mingi kwa vile nilienda tu Melbourne
 
mkuu kama kweli unataka utusue maisha tafadhali nenda katika nchi zifuatazo Shelisheli Ipo Africa,st Vincent And Grenadies,british Virgin Island Zipo Marekani Kaskazin Bila Kusahau Cape Verde Nakuhakikishia Ukirud Baada Ya Miaka Miwili Kama Hujajenga Magorofa Matatu Kwa Mpigo Mimi Fala..
Mkuu huko hata sijawahi waza kwenda, ila kwa ushauri wako niaahidi kuwa nitafautilia na kuona kama naweza kufit kufanya chochote, Australia nilishafika ila tatizo nilikaa mda mfupi sana na jimbo moja tu so sina uzoefu wa ujumla
 
Hamna Sehemu Nzuri Za Kuishi Kama Sehemu Hizo Mfano Shelisheli Nyumba Bure,umeme Bure,elimu Afya We Unatafuta Hela Ya Kufanya Maendeleo Tu Mishahara Mizuri Raia Wenyewe Wapo Laki Mbili Tu Na Per Capita Income Ni Usd 280 Kwa Kila Raia Kwa Kila Raia Yaan Ukiwa Na Elimu Katika Nchi Hiyo Hadi Raha
 
Back
Top Bottom