Mtazamo: Watanzania wengi wataishi maisha mazuri Sana muongo mmoja ujao kwasababu ya misingi anayoiweka Magufuli

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,461
31,033
Mimi kidogo nimesoma uchumi.Hivyo nitatoa short analysis ya kiuchumi.

Miaka kumi ijayo Tanzania itakuwa Kama afrika ya kusini au ureno.

Hebu fikiria yafuatayo.

Umeme mkubwa wa stiglaz gorge ambao utailuminate nchi yote na bado tukabakiwa na ziada.

Mradi wa REA ambao umeiluminate vijiji vingi Tanzania na kama ujuavyo palipo na umeme sio bushi Tena.

Imagine vituo vya afya vilivyozagaa mpaka maporini maana yake ni kwamba life expectancy ya watanzania itapanda pia.

Viwanda vikubwa vitajengwa kwasababu uhakika wa umeme upo 24/7/365 hivyo itachochea ajira nyingi Sana.

Sasa ona.

Una usafiri wa uhakika wa
Lami
Tren
Ndege

Una uhakika wa matibabu

Hospital
Vituo vya afya
Zahanati

Una nishati ya kutosha

Umeme
Gesi

Shule
Usalama
Nk

Hivi ndio vitu vitakavyotokea wafanya watanzania waishi maisha mazuri muongo mmoja ujao hii ni hakika.

Baniani mbaya kiatu chake dawa.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Afrika Kusini na Ureno hawaishi maisha mazuri. Matabaka ni makubwa, yaani masikini ni masikini haswaa na tajiri ni tajiri haswaa. Hili sidhani kama limekaa vizuri kiuchumi na sitegemei kuona Tanzania inakuwa kama Ureno au Afrika Kusini.

Kama mchumi nilitegemea ungeelezea ni jinsi gani hii miradi ambayo imeanzishwa na Raisi Magufuli italeta maendeleo chanya na ya moja kwa moja kwa watanzania. Elezea ni jinsi gani hii miradi inaweza kuinua sekta muhimu za mtanzania wa kawaida kama makazi, malazi, elimu, afya na chakula.

Binafsi nifahamuvyo ni kwamba kuwa na treni za umeme, barabara, nishati ya kutosha na miundo mbinu mingine haimaanishi kwamba nchi ina maendeleo au watu wanaishia vizuri. Lazima maendeleo ya vitu yaende sawa na yale ya watu. Raisi wetu ana mkakati gani wa kuhakikisha kwamba maendeleo ya vitu yanaenda sawa na yale ya watu ?

Kama mchumi nilitegemea ungeleta takwimu za uchambuzi wako kutoka kwa hizo nchi ambazo umezitolea mfano hapa. Lakini hujaleta, hivyo hoja yako inakuwa nyepesi.
 
Kuna legacy wanaweka viongozi ni kuwekeza kwa wananchi. Mfano Fidel Castro aliwekeza kwenye elimu. Sasa hivi Cuba ina madaktari wengi na wengi wameajiriwa nje ya nchi. Cuba wasiojua kusoma na kuandika ni wqchache mno.

China wamewekeza kwenye ujuzi. madada wa Kichina wengi ni Civil Engineers na wanapata kazi nje ya nchi, kipato chao kinaboresha nchi.

India ni wataalamu wa soft ware engineering, wanapata kazi duniani kwa ujuzi wao mkubwa wa IT.

Nchi za Africa zifikirie kuwekeza kwa raia wake.
 
Nas

Nashukuru kwa kujibu kwa hoja.

Hivi kweli uwepo wa umeme wa uhakika katika maelfu ya vijiji tz sio kiashiria Cha maisha Bora? Imagine wakazi wa makere kule kigoma ndani kabisa wanaumeme tafsiri yake tayari Wana uchumi mkubwa.

Watafungua saloon maduka ya kuuza vyakula barafu mabaa kumbi za starehe nk.
Umeme ndio maendeleo hebu niambie Kijiji alichokiacha mkapa chenye shule ya msingi Leo hii kina

Smsingi
Sekondari
Zahanati
Umeme
Maji
Umeme
Mabaa
Saluni ke na me

Hapa utapaita kijijini Tena?

Hii itafanya vijana wasione umuhimu wa kwenda darisalama teeeenaaa.
Kwasababu pamoja na kupata mahitaji yote hayo bado ana aridhi kubwa Sana. Kwahiyo kifupi magufuli anawafanya watanzania wadharau kwenda mijini kunyanyasika.
 
Unaweza kuwatengenezea miundombinu wawekezaji pamoja na foreign employees ilhali watu wako wakawa wanafaidika kwa kiasi kidogo sana maana hawakuandaliwa kuwa competent kuchukua fursa unazozitengeneza. Kinachofuatia ni social unrests na xenophobic attacks kama south
 
Kuna legacy wanaweka viongozi ni kuwekeza kwa wananchi. Mfano Fidel Castro aliwekeza kwenye elimu. Sasa hivi Cuba ina madaktari wengi na wengi wameajiriwa nje ya nchi. Cuba wasiojua kusoma na kuandika ni wqchache mno.

China wamewekeza kwenye ujuzi. madada wa Kichina wengi ni Civil Engineers na wanapata kazi nje ya nchi, kipato chao kinaboresha nchi.

India ni wataalamu wa soft ware engineering, wanapata kazi duniani kwa ujuzi wao mkubwa wa IT.

Nchi za Africa zifikirie kuwekeza kwa raia wake.
Zote hapa ni Elimu. Sijajua umezitofautishaje.

Hata hivyo nakubaliana na wewe kuwa kuna haja ya kuwekeza eneo linalomgusa mwananchi wa kawaida moja kwa moja.

Nimeyapenda maoni yako na unavyofikiri. Unatoa ushauri gani kwa Tanzania. Tuchague dira gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
:rolleyes:Vituo vya afya na life expectancy...itaongezekaje? wanajamii embu nifafanulieni...
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nas

Nashukuru kwa kujibu kwa hoja.

Hivi kweli uwepo wa umeme wa uhakika katika maelfu ya vijiji tz sio kiashiria Cha maisha Bora? Imagine wakazi wa makere kule kigoma ndani kabisa wanaumeme tafsiri yake tayari Wana uchumi mkubwa.

Watafungua saloon maduka ya kuuza vyakula barafu mabaa kumbi za starehe nk.
Umeme ndio maendeleo hebu niambie Kijiji alichokiacha mkapa chenye shule ya msingi Leo hii kina

Smsingi
Sekondari
Zahanati
Umeme
Maji
Umeme
Mabaa
Saluni ke na me

Hapa utapaita kijijini Tena?

Hii itafanya vijana wasione umuhimu wa kwenda darisalama teeeenaaa.
Kwasababu pamoja na kupata mahitaji yote hayo bado ana aridhi kubwa Sana. Kwahiyo kifupi magufuli anawafanya watanzania wadharau kwenda mijini kunyanyasika.
1.Huo umeme wa REA ni mradi unaofadhiliwa na mashirika ya nje sio purely our internal funds.

2. Ulianzishwa kipindi cha kikwete hivyo kwa kipindi hiki ndo upo katika peak.

3. umeulizwa kutoa data kutokana na wewe kusomea uchumi kama ulivyosema. Mfano hospitali ngapi zilikuwepo na ngapi zimejengwa au zinazotarajiwa, Kilometres ngapi za rami zimeongezwa, reli na umeme vile vile. Pili ufanye projections ukilinganisha na facilities zilizopo sasa kwa upande wa ufanisi na matokeo yake. Just be a bit proffessional kama ulivyosema maana unachofanya hakina tofauti na story za layman yoyote mtaani
 
Nas

Nashukuru kwa kujibu kwa hoja.

Hivi kweli uwepo wa umeme wa uhakika katika maelfu ya vijiji tz sio kiashiria Cha maisha Bora? Imagine wakazi wa makere kule kigoma ndani kabisa wanaumeme tafsiri yake tayari Wana uchumi mkubwa.

Watafungua saloon maduka ya kuuza vyakula barafu mabaa kumbi za starehe nk.
Umeme ndio maendeleo hebu niambie Kijiji alichokiacha mkapa chenye shule ya msingi Leo hii kina

Smsingi
Sekondari
Zahanati
Umeme
Maji
Umeme
Mabaa
Saluni ke na me

Hapa utapaita kijijini Tena?

Hii itafanya vijana wasione umuhimu wa kwenda darisalama teeeenaaa.
Kwasababu pamoja na kupata mahitaji yote hayo bado ana aridhi kubwa Sana. Kwahiyo kifupi magufuli anawafanya watanzania wadharau kwenda mijini kunyanyasika.
Naomba takwimu za maisha bora ya watu wa Afrika Kusini na Ureno ndiyo ntaona hoja yako ina uzito.
 
Mimi kidogo nimesoma uchumi.Hivyo nitatoa short analysis ya kiuchumi.

Miaka kumi ijayo Tanzania itakuwa Kama afrika ya kusini au ureno.

Hebu fikiria yafuatayo.

Umeme mkubwa wa stiglaz gorge ambao utailuminate nchi yote na bado tukabakiwa na ziada.

Mradi wa REA ambao umeiluminate vijiji vingi Tanzania na kama ujuavyo palipo na umeme sio bushi Tena.

Imagine vituo vya afya vilivyozagaa mpaka maporini maana yake ni kwamba life expectancy ya watanzania itapanda pia.

Viwanda vikubwa vitajengwa kwasababu uhakika wa umeme upo 24/7/365 hivyo itachochea ajira nyingi Sana.

Sasa ona.

Una usafiri wa uhakika wa
Lami
Tren
Ndege

Una uhakika wa matibabu

Hospital
Vituo vya afya
Zahanati

Una nishati ya kutosha

Umeme
Gesi

Shule
Usalama
Nk

Hivi ndio vitu vitakavyotokea wafanya watanzania waishi maisha mazuri muongo mmoja ujao hii ni hakika.

Baniani mbaya kiatu chake dawa.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Ni kweli Magu anatengeneza msingi mzuri sana. Ila mimi kama mchumi mwenzako nadhani kuwa miaka 10 ijayo bado tutakuwa hatujaifikia SA achilia mbali nchi kama Ureno.

Pamoja na kuwa Magu anafanya vema kwenye kutengeneza mazingira wezeshi, na kwenye utoaji wa huduma za umma, bado kasi ya maendeleo halisi si kubwa kiasi cha kutosha.

Sababu kubwa ni kuwa serikari ya bro Magu haijaweza kuzifungamanisha vema sekta kuu za uzalishaji (kilimo & viwanda) na hayo mazingira wezeshi inayojenga, hususan miundombinu.

Baada ya JNHPP na miradi mingine iliyopo kwenye mipango ya serikali yetu (rejea bajeti ya nishati mwaka huu) ambayo yote inaisha by 2023, tutakuwa na installed capacity ya 10,000 MW. Kumbuka SA ni 50,000MW!

Ili tufike huko sharti serikali itujengee hata skimu za kilimo moja kwa kila kanda kila mwaka (miundombinu ya kilimo) ila tija iongezeke kwenye kilimo. Pia awamu ijayo Magu aje na waziri serious kwenye viwanda na biashara. Awe mwenye maono, mbunifu, mtendaji, nk. Nazungumzia watu kama Jafo, Liana Sipora, Bashe, Mpango, et al.

Pia ili tufike huko, serikali yenyewe au kwa ushirikiano na sekta binafsi ifanye uwekezaji kwenye maeneo ya msingi: Kuchakata chuma (liganga), kusafisha mafuta, kuchakata gesi, kutengeneza magari, nk

Pia izibe maskio ifufue viwanda ambavyo ni labour intensive kama nguo, ngozi, pamba, korosho, na ilitoe boriti la bidhaa za mtumba ambalo kiukweli limetuganda machoni.

haya yanawezekana ikiwa wizara ya viwanda, biashara na kilimo zitapata watu sahihi.

Mkuu huu mradi wetu ukikamilika tutakuwa na uwezo wa kuzalisha MW ngapi?
 
SuperBug

Maendeleo ya kweli ni kuwekeza ktk watu maana Ujenzi wa Vitu (Maendeleo ya Vitu) kuna uwezekano mkubwa sababu mbalimbali kufanya miradi hiyo kuwa white elephant / magofu lakini ukiwekeza ktk elimu na afya hakuna hasara maana uwezekaji ktk Maendeleo ya Watu unahamishika..

CCM Mpya mpende msipende Lazima ku balance Maendeleo ya Watu viz Maendeleo ya vitu ktk uwiano wa 60: 40.
Katika kila shilingi mia tenga 60 ziende ktk Maendeleo ya Watu halafu 40 chenji iende ktk Maendeleo ya Vitu. Bila hivyo ktk muongo mmoja mtaiacha nchi na watu wake dhoofu bin masikini kuliko kipindi chochote cha awamu zote za CCM.

Mtu mwenye ujuzi na afya njema anaweza kuhama mkoa/ mji / nchi kutafuta maisha bora lakini Mataa ya barabarani, reli SGR, Bombadier ndege, viwanja vya ndege, madaraja, barabara za flyover hazihamishiki zinaweza kuwa magofu / white elephant.

Mjini wa Detroit Marekani ulikuwa maarufu wenye kila kitu cha Maendeleo ya Vitu lakini watu waliukimbia mji kama vile ulikumbwa na gonjwa hatari la corona. Lakini kwa vile serikali waliwapatia raia Maendeleo ya Watu yaani wana elimu, ujuzi na afya njema waliweza kutimka na kuliacha jiji la Detroit. Pia airport huko Spain imegeuka kuwa gofu la panya na ndege pori.

19 Dec 2018
How Detroit Went From A Booming Metropolis To A Shrinking City | NBC Nightly News

Part 1 of Reviving Detroit looks at how the city went from the richest in the U.S. to the most poverty stricken. Detroit’s population is at nearly a quarter of what it was at its peak, and despite a recent wave of gentrification, the city is still struggling with rampant crime, a failing school system and swaths of vacant land.
Source : NBC

Abandoned Airport in Spain

Mimi kidogo nimesoma uchumi.Hivyo nitatoa short analysis ya kiuchumi.

Miaka kumi ijayo Tanzania itakuwa Kama afrika ya kusini au ureno.

Hebu fikiria yafuatayo.

Umeme mkubwa wa stiglaz gorge ambao utailuminate nchi yote na bado tukabakiwa na ziada.

Mradi wa REA ambao umeiluminate vijiji vingi Tanzania na kama ujuavyo palipo na umeme sio bushi Tena.

Imagine vituo vya afya vilivyozagaa mpaka maporini maana yake ni kwamba life expectancy ya watanzania itapanda pia.

Viwanda vikubwa vitajengwa kwasababu uhakika wa umeme upo 24/7/365 hivyo itachochea ajira nyingi Sana.

Sasa ona.

Una usafiri wa uhakika wa
Lami
Tren
Ndege

Una uhakika wa matibabu

Hospital
Vituo vya afya
Zahanati

Una nishati ya kutosha

Umeme
Gesi

Shule
Usalama
Nk

Hivi ndio vitu vitakavyotokea wafanya watanzania waishi maisha mazuri muongo mmoja ujao hii ni hakika.

Baniani mbaya kiatu chake dawa.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Naam, ni mambo mema lkn pia naamini tunaweza kuwa na vitu hivyo pasipo kutekana au kufanyia dhulma wale tunao tofautiana nao kimtazamo.
 
Kama kweli umesoma uchumi na ulichoandika ni mtunda ya hiyo elimu yako, basi ulitoka na ziro au upo kisiasa zaidi. Maana kwanza huo umeme siyo wa miaka mitano ijayo ni zaidi ya hiyo, pili , vituo vya afya vipo, je kuna madaktari? Kuna vifaa na madawa? Huduma je, zipo? Hala acha kuhusinisha life expectancy na vituo vya afya.
Mimi kidogo nimesoma uchumi.Hivyo nitatoa short analysis ya kiuchumi.

Miaka kumi ijayo Tanzania itakuwa Kama afrika ya kusini au ureno.

Hebu fikiria yafuatayo.

Umeme mkubwa wa stiglaz gorge ambao utailuminate nchi yote na bado tukabakiwa na ziada.

Mradi wa REA ambao umeiluminate vijiji vingi Tanzania na kama ujuavyo palipo na umeme sio bushi Tena.

Imagine vituo vya afya vilivyozagaa mpaka maporini maana yake ni kwamba life expectancy ya watanzania itapanda pia.

Viwanda vikubwa vitajengwa kwasababu uhakika wa umeme upo 24/7/365 hivyo itachochea ajira nyingi Sana.

Sasa ona.

Una usafiri wa uhakika wa
Lami
Tren
Ndege

Una uhakika wa matibabu

Hospital
Vituo vya afya
Zahanati

Una nishati ya kutosha

Umeme
Gesi

Shule
Usalama
Nk

Hivi ndio vitu vitakavyotokea wafanya watanzania waishi maisha mazuri muongo mmoja ujao hii ni hakika.

Baniani mbaya kiatu chake dawa.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SuperBug

Maendeleo ya kweli ni kuwekeza ktk watu maana Ujenzi wa Vitu (Maendeleo ya Vitu) kuna uwezekano mkubwa sababu mbalimbali kufanya miradi hiyo kuwa white elephant / magofu lakini ukiwekeza ktk elimu na afya hakuna hasara maana uwezekaji ktk Maendeleo ya Watu unahamishika..

CCM Mpya mpende msipende Lazima ku balance Maendeleo ya Watu viz Maendeleo ya vitu ktk uwiano wa 60: 40.
Katika kila shilingi mia tenga 60 ziende ktk Maendeleo ya Watu halafu 40 chenji iende ktk Maendeleo ya Vitu. Bila hivyo ktk muongo mmoja mtaiacha nchi na watu wake dhoofu bin masikini kuliko kipindi chochote cha awamu zote za CCM.

Mtu mwenye ujuzi na afya njema anaweza kuhama mkoa/ mji / nchi kutafuta maisha bora lakini Mataa ya barabarani, reli SGR, Bombadier ndege, viwanja vya ndege, madaraja, barabara za flyover hazihamishiki zinaweza kuwa magofu / white elephant.

Mjini wa Detroit Marekani ulikuwa maarufu wenye kila kitu cha Maendeleo ya Vitu lakini watu waliukimbia mji kama vile ulikumbwa na gonjwa hatari la corona. Lakini kwa vile serikali waliwapatia raia Maendeleo ya Watu yaani wana elimu, ujuzi na afya njema waliweza kutimka na kuliacha jiji la Detroit. Pia airport huko Spain imegeuka kuwa gofu la panya na ndege pori.

19 Dec 2018
How Detroit Went From A Booming Metropolis To A Shrinking City | NBC Nightly News

Part 1 of Reviving Detroit looks at how the city went from the richest in the U.S. to the most poverty stricken. Detroit’s population is at nearly a quarter of what it was at its peak, and despite a recent wave of gentrification, the city is still struggling with rampant crime, a failing school system and swaths of vacant land.
Source : NBC

Abandoned Airport in Spain

Safi.

Tanzania tuwe na majority ya watu wanaoelewa haya ndio tutaendelea.
 
Wewe ni kilaza haswa,unafikiria maendeleo kwa watu kufungua Saloon,Bar na kuuza barafu!

Back
Top Bottom