JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Leo nimesoma mtandaoni kuwa Vidonda vya tumbo(Ulcers) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Naomba kujua kama ni kweli maana siku zote mie najua vidonda vya tumbo huvipata mtu kutokana na mtindo wake wa maisha(kutokula) au kwa kutumia baadhi ya dawa ambazo zinaweza kuchubua utumbo. Sasa hii ya kuambukiza kwangu imekuwa mpya sana, tena mwandishi alifafanua zaidi kuwa eti iwapo mwenza wako ana ulcers basi uwezekano wa wewe kuupata ni mkubwa maana anaweza kukuambukiza.
Kumekuwepo na barua inayiosambaa Mtandaoni ikionesha kuandikwa na Mfalme Mswati III ametoa tangazo linalodai kuwa kutokana na uhaba wa Wanaume kwenye nchi yake, amewaomba wananchi wanaoishi Kusini mwa Jangwa la Sahara kuomba uraia kwenye nchi yake, na kila mwanaume atayeoa walau wanakwake 5 atamlipia gharama za harusi zao pamoja na kuwanunulia nyumba. Ukweli wa taarifa hii upoje?
Katika pitapita mitandaoni nimekutana na huyu chawa wa Mtoto wa Rais Museveni, Kainerugaba Muhoozi akimtuhumu Kakwenza Rukira kuingia makubaliano ya siri na umoja wa Ulaya nchini Uganda katika kuhamasisha ushoga nchini humo. Nakumbuka Uganda imezuia mahusiano ya jinsia moja na Rais Museveni amebana kweli kweli wazungu hawana pa kupumulia, naona wameamua kupitia njia za panya kuleta ushenzi wao.
TinEye ni nyenzo nzuri ya kutafuta picha kwenye wavuti ambayo inaweza kutumiwa kufanya uhakiki wa Picha. JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. 1. Fungua Kivinjari Chako Anza kwa kufungua kivinjari chako kwenye kifaa chako cha mkononi au kompyuta. 2. Tembelea Tovuti ya TinEye Ingiza 'TinEye' kwenye sanduku la utaftaji la kivinjari chako na bonyeza kwenye matokeo yanayofanana na tovuti rasmi ya TinEye. 3. Pakia Picha Kuna njia mbili za kupakia picha kwenye tovuti ya TinEye Bofya kwenye kitufe cha 'Pakia Picha' au "Upload' kisha pakia picha unayotaka kufanya uhakiki. Ikiwa picha tayari iko kwenye wavuti, unaweza kunakili URL (Link) ya picha hiyo na kuibandika...
Yandex ni njia nyingine ya utafutaji inayotumika sana kufanya uhakiki wa picha. JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. 1. Fungua Kivinjari Chako Anza kwa kufungua kivinjari chako kwenye kifaa chako cha mkononi au kompyuta. 2. Tembelea Tovuti ya Yandex Ingiza 'Yandex' kwenye sanduku la utafutaji la kivinjari chako na bonyeza kwenye matokeo yanayofanana na tovuti rasmi ya Yandex. 3. Pakia Picha Kuna njia mbili za kupakia picha kwenye tovuti ya Yandex Bofya kwenye alama ya kamera iliyo kwenye sanduku la utaftaji la Yandex na chagua 'Pakia Picha' au 'Upload' kisha upakie picha unayotaka kufanya uhakiki. Ikiwa picha tayari iko kwenye wavuti, unaweza kunakili URL...
Habari wakuu, Nimeona taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki imetambulisha noti yake itakayotumika katika nchi wanachama, iliyopewa jina la SHEAFRA (SHF). Wengi wameinukuu akaunti kutoka mtandao wa X (zamani Twitter) inayojulikana Government of East Africa Moja ya chombo kikubwa kilichoinukuu akaunti hiyo ni pamoja na ITV , binafsi bado nina mashaka na hii taarifa kutokana na kwamba akaunti maalum ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ninayoifahamu siyo hii. Ukweli ni upi?
Habari Wadau, Nimekutana na tangazo la kazi likionesha kuwa Kampuni ya usafirishaji ya Tilisho inahitaji Wafanyakazi kwa nafasi ya Wakatisha Tiketi na wahudumu wa ndani ya Mabasi. Nimepata mashaka baada ya kuona ukilifuata tangazo hili ndani yake linahitaji usambaze link kwenye magroup ya WhatsApp na Facebook ili kuendelea hatua inayofuata. Je, kuna ukweli juu ya Tangazo hili?
Kuna dada zetu wanapenda sana urembo hivyo kujiongezea baadhi ya vitu kama matako, kope, lenzi kwenye macho, matiti vimekuwa vitu vya kawaida sana kwao. Ukweli hayo yote wanayojiongea yanakuwa na madhara. Mimi nipende tu kutoa hadhari kuwa kope na lenzi bandia mnavyojiongezea ni hatari kwa afya ya macho yenu. Chonde chonde ridhikeni na mlivyoumbwa navyo. Khadija Omary ni mmoja wa wahanga wa kupofuka baada ya kuwekewa kope bandia. Ni hayo tu.
Salaam wakuu, Wakati mikoa mingi nchini ikiendelea kupata mvua ya kutosha, kwa wengine imekuwa neema kwao kwani sasa wanaweza kuvuna maji ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, mifugo na hata mazao. Sasa kwa matumizi ya nyumbani ni pamoja na kuyatumia kwa kunywa bila kuyafanyia treatment yoyote. Tokea nakua kumekuwa na kasumba na kuaminishana kuwa maji ya mvua ni bora kwa kunywa. Mvua ikinyesha tumekuwa tukiyakinga na kunywa moja kwa moja bila kujua madhara yake Pamoja na kubeba vimelea vingi na kila aina ya takataka, pia kuna aina ya madini maji hayo hukosa kwa ajili ya afya ya binadamu. Pia kuna jamii zinaamini kuwa maji ya mvua yanatibu magonjwa mbalimbali. Maji ya mvua yanaweza kuwa safi lakini siyo salama.
Haya mambo yasikie tu, watoto wetu siku za shule huwa wanalazimishwa kulala tu punde wamalizapo kula. Hii ni hatari kwa mujibu wa tafiti za afya. Uelewa mdogo na kutojali kwa wazazi kunaweza kupelekea watoto wetu kupata madhara hapo mbeleni. Kulala mara baada ya kula ni kitendo ambacho hupendelewa kufanywa na mamilioni ya watu japokuwa tabia hii si nzuri kiafya, kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wansayansi wa chuo kikuu cha Loannina Medical watu wanaosubiri kulala kwa muda kidogo mara baada ya kula wana nafasi ndogo ya kupata ugonjwa wa mshtuko na hii ndio sababu inashauriwa kukaa masaa mawili mara baada ya kula ndipo kulala.
Wote mnaweza kufikiria ni namna gani mtu asiye mkazi au mfanyakazi au mwenye appointment kwenye makazi rasmi ya Malkia wa Uingereza angeweza kupenya bila kuonekana, akafanikiwa kuingia ndani ya jumba hilo, akapiga misele kidogo, akaingia ofisi ya Malkia Elizabeth kufyonza mvinyo maalum wa Malkia, na mwisho wa siku akazama ndichi kwenye hiyo room ya Malkia na kumkuta Malkia akiwa katikati ya njozi tamu, akaketi pembeni yake na kumsubiri Malkia aamke ili wayajenge/wapeane maelekezo. Basi kunaye dogo mmoja alileta makwaru na kufankiwa mpaka Malkia mwenye alipomsanukisha. Inadaiwa tukio hilo lilisababisha ulinzi zaidi uimarishwe na baadhi ya walinzi walifukuzwa.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…