- Source #1
- View Source #1
Salaam wanajamvi, heri ya siku ya uhuru watanzania wenzangu!!
Kuna hii taarifa nimekutana nayo kwamba Gamondi amesema, "Sasa Mmejua kwamba Sikuwa Tatizo pale Yanga SC, Kama mkiendelea kucheza kama Juzi hamfiki Robo Fainali Msimu Huu" hivi kweli huyu mzee anaweza kusema hivi?
Kuna hii taarifa nimekutana nayo kwamba Gamondi amesema, "Sasa Mmejua kwamba Sikuwa Tatizo pale Yanga SC, Kama mkiendelea kucheza kama Juzi hamfiki Robo Fainali Msimu Huu" hivi kweli huyu mzee anaweza kusema hivi?
- Tunachokijua
- Miguel Ángel Gamondi ni kocha (mwalimu) wa mchezo wa mpira wa miguu kutoka Argentina ambaye aliwahi kuitumikia nafasi ya kocha mkuu katika timu ya Yanga SC kabla ya mkataba wake kukoma kwa makubaliano ya pande zote mbili mnamo mwezi Novemba, 2024. Kadhalika aliwahi kufanya kazi na Wydad AC, Ittihad Tanger, CR Belouizdad na nyinginezo.
Akiwa kocha wa Yanga Gamondi aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2023/24, Kombe la shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup)
Tangu kuondoka kwa kocha huyo, timu hiyo imepoteza jumla ya michezo minne, miwili ikiwa ikiwa ni ligi kuu Tanzania bara, na miwili michuano ya klabu bingwa barani Afrika, matokeo ambayo yamewafanya mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuulaumu uongozi kwa kusitisha mkataba na Kocha huyo licha ya kuwa na kocha mpya ambaye tayari amekabidhiwa majukumu ya kocha mkuu.
Hata hivyo kuondoka kwake kumesababisha kuibuka kwa taarifa zisizo za kweli huku akidaiwa kutoa kauli mbalimbali kabla na baada ya mechi za Yanga.
Hivi karibuni kumekuwapo na taarifa kuwa Gamondi amesema yeye hakuwa Tatizo pale Yanga SC, akiongeza kuwa Kama timu hiyo ikiendelea kucheza kama mchezo uliopita haitofika Robo Fainali Msimu Huu.
Je ni upi uhalisia wa kauli hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa kauli hiyo haijawahi kutolewa na Gamondi wala kuchapishwa na kocha huyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, mtandaao ambao amekuwa akiutumia mara nyingi zaidi, ujumbe uliohusishwa na kocha huyo ulinukuliwa na 7MEDIA kutoka ukurasa usio rasmi ukidaiwa kuwa wa Gamondi.
Vilevile picha iliyotumika kuambatanisha ujumbe huo usio wa Gamondi, kocha huyo aliichapisha mnamo tarehe 15, mwezi agosti 2024 katika mtandao wa instagram huku akiweka ujumbe unaosema "Akili zetu zina uwezo wa kuvuka mipaka tuliyojiwekea. Zaidi ya pande mbili zinazopingana ambazo ulimwengu unazijumuisha, maarifa mapya na mawazo mapya huanza."
Ukurasa huo umekuwa ukitumia utambulisho wa kocha Gamondi huku ukichapisha kauli mbalimbali zikidaiwa kutolewa na Gamondi, rejea hapa. Aidha maudhui yake hayawiani na maudhui ambayo yamekuwa yakichapishwa na Gamondi mara nyingi kupitia mtandao wa Instagram ambao pia hauna ujumbe huo, rejea kurasa rasmi za kocha huyo za mtandao wa Instagram na Facebook.
Gamondi amekuwa na mtazamo chanya hata baada ya kuondoka Yanga tofauti na kauli zinazowekwa katika ukurasa huo. Kauli yake ya mwisho kuhusu Yanga kupitia mtandao wa Instagram Gamondi alisema "Asante sana Wananchi, Wachezaji wangu, na kila mtu… Ninashukuru sana na najivunia kuwa sehemu ya Yanga katika wakati wangu. Mtaendelea kuwa moyoni mwangu daima. Upendo mkubwa kwenu."