KWELI Hiki ni Kimbunga cha Maji

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Nmeona mtu ametuma picha zikionesha kama moshi mrefu juu ya maji huku akiyaita ni maajabu lakini watu wamekuwa wakisema hiyo ni hali ya kawaida kwa kuwa hiko ni kimbuga cha maji, Je uhalisia upoje?
Screenshot 2024-11-20 092525.png
 
Tunachokijua
Kimbunga kinachotokea majini kwa kiingereza hujulikana kama waterspout, Kwa mujibu wa tovuti ya huduma za bahari nchini Marekani (NOAA) kimbunga cha majini kimegawanyika katika aina mbili aina ya kwanza ni kimbunga kinachotokea kama upepo mwepesi ama wingu kwenda na aina ya pili ni kimbunga kinachofanana kama kile cha ardhini.

Aina ya kwanza ya kimbunga hutokea juu ya maji ikiwa katika muonekano wa upepo mwepesi ambao husogea taratibu kutoka sehemu moja kwenda nyingine na haiambatani na ngurumo za radi. Aina hii hutokea juu ya maji wakati aina ya kimbunga kinachofanana na kimbunga cha ardhini hutokea hutokea kwenda chini.

Aina ya kimbunga inayofanana na kimbunga cha ardhini aina hii hutokea juu ya maji ama wakati mwingine huwa kinahama kutoka nchi kavu hadi majini, aina hii huwa na sifa zote za kimbunga cha nchi kavu. Aina hii huambatana na ngurumo kali za radi, upepo mkali, mvua ya mawe na mwanga mkali.

kimbunga kinachofanana na upepo mwepesi ndicho hutokea mara nyingi zaidi kuliko kimbunga kinachofanana na cha ardhini.

Britanica wanaeleza kuwa sio rahisi kujua idadi ya utokeaji wa waterspout kwa sababu vingi hutokea baharini na uonekanaji wake ni wa nadra sana kwani mpaka uione unapaswa kuwa kwenye pwani, kwenye meli, ama ukiwa kwenye ndege. Vimbunga hivi hutokea maeneo mbalimbali ikiwemo Afrika, mara nyingi kwenye maeneo ya kitropiki msimu wa joto.

Mwendokasi wa kimbunga cha majini unakadiriwa kuwa ni wa kawaida lakini wa juu zaidi unakadiriwa kuwa kati ya kilomita 64 hadi 80. Uchunguzi wa kisayansi wa kisasa kuhusu kimbunga cha majini ulianza mwaka Agosti 19, 1896 mara baada ya kutokea kimbunga kikubwa cha majini katika pwani ya Massachusetts, Marekani kilichodumu kwa takribani dakika 35.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom