JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Hapa kijijini mjadala umekuwa ukiendelea kuhusu wanyama jamii ya Punda namna ya ulaji wa mimea, mfano "mhindi" ambao umeng'atwa na punda huwa hauoti tena, tofauti na unapong'atwa na wanyama wengine kama ng'ombe, kondoo au mbuzi, na wanakijiji wamefika mbali zaidi na kusema labda wanyama aina ya punda yamkini watakuwa na sumu, hivyo endapo watang'ata mmea huo basi huathirika na sumu, hivyo kutokuendelea kuchipua tena.
Nyota wa zamani wa Real Madrid, Roberto Carlos anadaiwa kuingia kwenye mgogoro na mkewe hali iliyopelea atumia majengo ya uwanja wa mazoezi wa Real Madrid kama makazi wakati akishughulikia suala lake la talaka na mkewe waliodumu kwa miaka 15 Wenzi hao, waliofunga ndoa mwaka 2009, sasa wanakabiliwa na vita vya kisheria kuhusu utajiri mkubwa wa Carlos, unaoripotiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 133 (Tsh410,091,550,000)
Binamu wa rais wa zamani wa Syria, Bashar al-Assad aliukiwa kwa kunyongwa na baada ya kupandishwa juu na crane. "Baada yakuwasili kwa vikosi vya waasi wa Syria katika mji wa Latakia, ilitangazwa kuwa Suleiman al-Assad, ambaye alikuwa kiongozi wa Vikosi vya Ulinzi wa Kitaifa, aliuawa. Kwa mujibu wa gazeti hilo, Suleiman al-Assad alinyongwa kwa kutumia kreni katika uwanja mmoja huko Latakia. Sababu ya kuuawa kwake ilikuwa uhusiano wake wa damu na rais wa zamani, pamoja na "uhalifu dhidi ya wale waliopinga utawala huo."
Inadaiwa huyu jamaa bhana enzi za utumwa, alitumika na masta wake kama mbegu ya kuzalisha watumwa wenye nguvu. Inadaiwa kutokana na kuwa na nguvu, umbo maridadi na urefu wa futi 7 hivyo masta wake alimpa upendeleo wa kipekee wa kumpunguzia majukumu mengi huku kazi yake kubwa ilikiwa ni kulala na kuwapa mimba wanawake mbalimbali ili waweze kumzalia masta wao watoto wenye nguvu ambao wangetumika katika shughuli za kitumwa. Roque Jose Florêncio aliacha idadi kubwa sana ya watoto.
Back
Top Bottom