Kumekuwepo na chapisho ambalo limechapishwa na chombo cha habari cha Azam tv tanzania kikiwa nukuu ya kuwa uking’atwa na nyoka huruhusiwi kufunga kamba juu ya kidonda, kuchanja wala kunyonya sumu kwa mdomo. Unachopaswa kufanya ni kutulia kwanza ili kupunguza msukumo wa damu.
Dai hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu na Uhamasishaji Uhifadhi wa Nyoka Tanzania (TASCEA), Aldo Charles, wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Morning trumpet
Je ni upi uhalisia wa dai hilo?