JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Kuna tafiti za hivi karibuni zimethibitisha kwamba hata wanaume hupata hedhi, ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika. Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi, mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.
Mdau mmoja wa Jamiiforums ameonesha wasiwasi wake baada ya kwenda hospitalini kupima VVU ambapo tofauti na namna alivyotarajia, daktari wake alimpima kwa kutumia mate yaliyotolewa kwenye fizi ya juu na chini. Jambo hili limemfanya atoe ushauri kwa watu kuwa makini wanapokuwa wanabusiana kwa kuwa tendo hilo linaweza kusababisha maambukizi ya VVU kupitia mate. Ukweli wa jambo hili upoje?
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…