SI KWELI Video watoto wakicheza kwenye kimbunga

SI KWELI Video watoto wakicheza kwenye kimbunga

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Screenshot 2026-04-14 140221.png
 
Tunachokijua
Wadau wa JamiiCheck kupitia mitandao ya kijamii na jukwaa la JamiiCheck.com wamebainisha uhalisia wa video inayowaonesha watoto wakicheza na kimbunga. Wengi wameeleza kuwa video hiyo ina viashiria kuwa si video halisi bali imetengenezwa kwa kutumia Teknolojia ya Akili Unde (AI).

Baadhi ya Majibu ya wadau

my_country254 (Mdau wa JamiiCheck Instagram)
Hiyo ni AI, angalia huyo mtoto mwenye begi jeusi amerushwa mara mbili
Dotto Shaaban (Mdau wa JamiiCheck Facebook)
AI, maana huyo dogo wa mwisho inaonekana begi lake limerushwa lakini yeye akatoka tena na begi! Wakati wote wana mabegi yao, je lile lililorushwa nje ni la nani!?
chama_dulla_feb20 (Mdau wa JamiiCheck Instagram)
Kuna huyo mwenye suruali nyekundu kaingia kwenye upepo katoka ana suruali ya jeans

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa video hiyo inayosambaa kupitia mitandao ya kijamii na kudaiwa kuwa ni ya tukio kutoka nchini India, imetengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde (AI). Kwa kutumia nyenzo ya kidigitali ya kubaini maudhui ya AI ya Hive Moderation imetengenezwa kwa teknolojia hiyo kwa zaidi ya 99.4%.

1776418945925-png.3574256

Similar Discussions

Back
Top Bottom