Featured content

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo yaomba Tsh Bilioni 525.3 kwa  mwaka wa fedha 2026/2027
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, Mei 4, 2026 amewasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 ambapo ameomba Bunge kuidhinisha jumla ya Tsh. bilioni 525.3, ambapo kati ya fedha hizo Tsh. Bilioni 39.07 zimetengwa kwa ajili ya mishahara, Tsh. Bilioni 28.06 kwa ajili ya mengineyo na Tsh. Bilioni 458.19 kwa ajili ya miradi ya maendeleo
Waziri Kairuki: Matumizi ya Internet yameongezeka kwa 19.5%, watumiaji wafikia Milioni 58.9
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, akiwasilisha taarifa ya wizara hiyo Bungeni Aprili 30, 2026, amebainisha sekta ya mawasiliano nchini imeendelea kukua kwa kasi, ambapo idadi ya watumiaji wa Intaneti imeongezeka kwa 19.5%, kutoka milioni 49.3 (Machi 2025) hadi kufikia milioni 58.9 (Machi 2026).
Mahakama yakataa Lissu kuunganishwa kwenye kesi ya mgawanyo wa mali za CHADEMA
Aprili 30, 2026, Mahakama Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imekataa ombi la Tundu Lissu la kuunganishwa katika Shauri Namba 8323/2025 lililofunguliwa na Said Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini pamoja na Katibu Mkuu inayohusu mgawanyo wa mali za CHADEMA.
AZAKI: Tume ilitumia taarifa za Polisi ambao nao wanatuhumiwa kuua waandamanaji
Mwakilishi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Halima Sonda, wakati akiwasilisha sehemu ya tamko la asasi za kiraia (AZAKI) na watetezi wa haki za binadamu kuhusu ripoti ya matukio ya Oktoba 29, 2025 mbele ya waandishi wa habari Aprili 27, 2026, alisema kuwa Tume hiyo ilitumia vyanzo rasmi kama Polisi na vituo vya afya, ambavyo pia vinalalamikiwa kuwa wahusika wakuu wa ukiukaji wa haki, ikiwemo kuua na kutesa raia.
Jaji Juma: Baada ya Ripoti Kutoka, tumepokea simu za matusi zaidi ya 300
Tume ya kuchunguza matukio ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu 2025, imezungumza na vyombo vya habari Aprili 28, 2026 ikiwa ni baada ya siku tano ilipowasilisha na kukabidhi Ripoti yake kwa Rais Samia Aprili 23, 2026. Jaji Mkuu Mstaafu Ibrahim Juma, ambaye ni mmoja wa Wajumbe wa Tume hiyo amesema kwamba kuwa kuna watu hawataki maoni ya watu wengine yasikike na kwamba baada ya kutoa ripoti wamepokea simu za matusi zaidi ya 300.
Maswali 10 Muhimu Kuhusu Ripoti ya Tume ya Jaji Chande
Hatimaye Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imetoa ripoti yake baada ya kufanya uchunguzi kwa siku 153. Tume hiyo iliyoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande Othman, ilikuwa na wajumbe wanane ambao ni: Dkt. Stergomena Tax, Jaji Mkuu mstaafu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Balozi Ombeni Yohana Sefue, Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu Said Ally Mwema, Balozi Paul Meela, Balozi David Kapya, Balozi George Madafa, na Balozi...
Jaji Chande: Tume imepokea ushahidi toka kwa Watu 63,603
Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025, Jaji Mohamed Chande Othman, amesema Tume hiyo imepokea ushahidi kutoka kwa Watanzania 63,603 kwa njia mbalimbali. Amesema ushahidi huo umepatikana kupitia mahojiano ya ana kwa ana na mashahidi 1,323, mashahidi wa viapo 553, na madodoso 4,891 yaliyokuwa na maswali bila majina ya wahusika.
Msigwa: Deni la Taifa linakua siyo kwa sababu tunatumia vibaya fedha
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa ongezeko la deni la taifa halitokani na matumizi mabaya ya fedha, bali ni matokeo ya uwekezaji mkubwa katika miradi ya kimkakati ya maendeleo inayolenga kuleta mapinduzi ya kiuchumi. Msigwa amefafanua kuwa fedha hizo zimeelekezwa katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa kama reli ya mwendokasi (SGR), upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam, uimarishaji wa shirika la ndege (ATCL), pamoja na kuboresha huduma za kijamii ikiwemo kusambaza umeme vijiji
Rais Samia: Mmeshuhudia siku tatu zile, hakukuwa na harusi wala mabaa, zilikuwa siku nzito
Rais Samia Suluhu amesema amani ni hazina ya shughuli zetu za kiuchumi na kijamii akisisitiza kwamba bila amani hakuna kujenga uchumi, hakuna shughuli za kijamii. Ameongeza kuwa, mmeshuhudia siku tatu zile (Oktoba 29) ambapo hakukuwa na shughuli za burudani, harusi, kitchen party, mikusanyiko ya kijamii, wala michezo yoyote. Amesema zilikuwa siku tatu nzito.
Msanii A.Y: Niwe mkweli suala la kutengeneza Mdundo wa Taifa, haliwezekani
Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya (AY), ameweka wazi msimamo wake kuhusu mjadala wa “mdundo wa taifa,” akisisitiza kuwa utambulisho wa muziki hauwezi kulazimishwa kupitia mipango ya mezani bali hujitengeneza wenyewe kadri muda unavyokwenda. Amesema muziki wa Bongo Fleva tayari una ladha yake inayotambulika kimataifa, akitoa mfano kuwa hata nchi kama Nigeria zilipitia hatua za kuiga kabla ya kufikia utambulisho wao wa sasa, hivyo wasanii wanapaswa kuthamini muziki wa nyumbani.
Waziri Nanauka: Serikali kuanzisha Benki ya Vijana
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amesema serikali inaendelea na utafiti wa kuanzisha Benki ya Vijana nchini ili kuondoa vikwazo vya mitaji na kutoa huduma za kifedha zinazoendana na mahitaji ya vijana wanaoanza shughuli za kiuchumi. Akiwasilishaji wa makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27, Nanauka amesema benki hiyo itakuwa chombo cha kimkakati cha kuchochea ubunifu, kuongeza ajira, na kuimarisha mchango wa vijana katika kukuza uchumi
Uchambuzi wa Hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu 2026/2027: Tusome katikati ya mistari
"Kama baba wa familia anasema 'tutajenga nyumba kubwa mwaka huu', unauliza maswali ya msingi: Bajeti iko wapi? Fundi ni nani? Nyenzo zimenunuliwa? Tutamaliza lini?" Vivyo hivyo, tunapaswa kuihoji Serikali. Zingatia: Tarehe mosi Aprili 2026, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb.) aliwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2026/2027. Hotuba ina kurasa 131. Watanzania wengi hawatapata muda wa kuisoma yote. Ipo hapa Muhimu...
Iran yafungua lango la Hormuz kupisha mazungumzo ya Israel na Lebanon
Serikali ya Iran, kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje Seyed Abbas Araghchi, imetangaza rasmi kufunguliwa kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz kwa meli zote za kibiashara kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku 10 kati ya Israel na Lebanon yaliyoanza Aprili 16, 2026.
Maelekezo ya Lissu "Futeni kesi zangu na za chama, nikiwa huru ndiyo tuzungumze"
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameeleza utayari wake wa kushiriki mazungumzo ikiwa tu atakuwa huru baada ya kufutwa kwa kesi zote zinazomkabili yeye pamoja na chama chake. Kupitia taarifa iliyotolewa Aprili 16, 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, imeeleza kuwa Lissu amesema kesi ya Uhaini inayomkabili inatokana na msimamo wake wa No Reforms, No Election.
Arusha: Watu 6 wakamatwa wakituhumiwa kumuua Askari kwa kudhani ni Mwizi
Jeshi la Polisi linawashikilia Watu 6 kwa kudaiwa kumuua Askari Polisi, Roland Mollel baada ya kumshambulia, tukio lililotokea katika Mtaa wa Mlimani, Kata ya Muriet, jana Aprili 15, 2026. Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Justine Masejo amesema Roland alikuwa katika shughuli zake binafsi baada ya kazi, kulitokea taharuki iliyotokana na kusambaa maneno ya kundi la Watu wakidai eneo lao kuna wezi, marehemu akapita akiwa amebebwa katika bodaboda, kundi la Watu likawashambulia huku wakiwakimbiza.
Rais wa FIFA: Nimeonana na Iran, itashiriki Kombe la Dunia 2026 Marekani
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino amewahakikishia mashabiki wa Soka Duniani kuwa timu ya taifa ya Iran itashiriki Kombe la Dunia 2026, licha ya mashaka yaliyotanda tangu Marekani na Israel zilipoingia katika vita na Iran. Amesema Iran imefuzu kihalali kushiriki Kombe la Dunia na wachezaji wake wana haki ya kucheza na kuiwakilisha nchi yao.
Mwigulu: Elimu ya msingi ya lazima kuwa miaka 10
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba ametangaza kuanza kwa utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu utakaofanya elimu ya msingi kuwa ya lazima kwa kipindi cha miaka kumi, akisema ni sehemu ya mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu. Akihitimisha hotuba ya bajeti bungeni, ameeleza kuwa mabadiliko hayo ni makubwa zaidi tangu yale ya mwaka 1967 yaliyoongeza elimu ya lazima kufikia darasa la saba.
Afrika Kusini: Kiongozi wa Upinzani Julius Malema ahukumiwa miaka 5 jela
Kiongozi wa Chama cha Upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF), Julius Malema amehukumiwa kifungo cha Miaka Mitano jela na kulipa faini baada ya kupatikana na hatia ya makosa matano ikiwemo kumiliki silaha kinyume cha Sheria na kuifyatua hadharani hali iliyohatarisha maisha ya Watu. Mwanasheria wake amesema watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo ili kuzuia kiongozi huyo kupelekwa gerezani.
Mahakama ya Rufani yairuhusu CHADEMA kuendelea na shughuli za Kisiasa nchini
Mahakama ya Rufani Kanda ya Dodoma, leo Aprili 15, 2026 imetengua maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyokizua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya shughuli za Siasa nchini, kufuatia kesi iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar), Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya chama hicho.
Korea Kusini: Raia kuanza kupewa Intaneti ya bure kama haki ya msingi sawa na maji na umeme
Korea Kusini imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza mpango wa kuwapatia wananchi Intaneti bure hata baada ya vifurushi kuisha, kwa kasi ya takriban 400 Kbps. Hatua hii inalenga kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu mtandaoni kama sehemu ya mkakati wa kuifanya Intaneti kuwa haki ya msingi, tofauti na nchi kama Ufilipino, Estonia na Costa Rica ambazo hutoa Wi-Fi ya bure katika maeneo ya umma.
Back
Top Bottom