Zuku tv kiboko

Ddtv kwanini wanatoza kwa $ hivi ile cable network ilikufa?
 
kwa mtu anayejua content gani aangalie hawezi hata siku moja kuisifia startimes,ting au easy tv,hata hao wapenzi wa mpira huwezi kuangalia mpira kila siku kwanza live match zipo weekend tu na mara chache sana katikati ya wiki?hebu niambie baada ya kuangalia ligi ya italia utaangalia nini?mgm?hakuna channel yoyote ya maana katika startimes au ting,kama mpira unaweza kuangalia pub.asikudanganye mtu zuku ni mbadala wa dstv kama huwezi dstv nenda zuku lkn startimes unapoteza muda,kwa mfano zuku wana channel za movies za kutosha more than 5,music channel kama kerrang!,q au smash hit ambazo zinapiga miziki mikali...na kama ulizoea kuangalia ting au startimes siku ukifunga dstv au zuku hutalala na kazini hutaenda na utaacha misele...content zilizopo zuku na dstv ni zile zile tofauti ni majina tu ya channel,mfano kinachoonyeshwa kwenye crime and investigation network channel ya dstv utakipata kwenye viacrime channel ya zuku....mi naungana na jamaa aliyeisifia zuku kusema ukweli hawa jamaa wamejitahidi na huko mbele wata tender tu epl...tuwe wa kweli hiv unaweza kukaa nyumbani kwako ukaangalia startimes nusu saa bila kuhamisha channel na mwishowe kuzima kabisa tv?alfu 40 ni afadhari kuliko laki na 30 ya dstv kama mpira utaenda pub kuangalia.....
Kwa maelezo hayo bila kuongeza neno, Zoku ni janga lingine la kitaifa!
Mtazania anaelemewa na tsh 7000 ya Startimes leo useme unamsaidia kwa 40000??

DSTV wataendelea kuwajuu kwakuwa wanachaneli za mpira!
 
Wewe kweli huelewi dstv nini. Huwezi hata cku moja kulinganisha dstv na hawa wapuuzi wengine wa kibongo, wanaochoma mahindi tu. Dstv inakubalika Africa nzima+Ulaya coz huduma na station zao ni world class. Na tena, bei wanazoweka ni cheap sana. $78 unapata chaneli 180+, kutoka kila kona ya dunia, marekani, ulaya, afrika, asia, u name it! So for nw, dstv haina mpinzani, sio bongo tu, bali afrika nzima!
 
Hapa naona wote wanaosifia ni maagent tu wa hivi ving'amuzi sijui hadi sasa mkweli ni yupi kama unasema $78 ni cheap, lazima uwe fisadi tu. Samahani napita tu nikaona ngoja nipige chabo
 
wewe ndio hujui kabisa dstv ina channel ngapi unazoweza kuangalia kwa premium boequet,nenda kwa jirani yako unakoangalia kahesabie upya uone kama zinafika 180,kwa taarifa yako si channel zote uzionazo kwenye decoder ya dtv zinafunguka hapa kwetu na channel kama 107 hv ukijumrisha na free to air,watu wengi mnapoona namba zinaanzia mia mpaka mpaka mia saba basi unajua channel zote utaziona mfano mnet kuna east na west ile west [dstv 103]huku kwetu haifunguki ni kwa ajiri ya west tu.au channel kama fox,fx nazingine huku kwetu hazifunguki hata ulipie premium,na unaposema dstv inakubariki ulaya huo ni uongo mkubwa kwani beam za dstv ni kwa africa tu na itakubariki vp ulaya wakati kule kuna sky ambayo channel karibu zote unazoziona kwenye dstv zinatoka huko?hata channel zinazotoka usa dstv hapati moja kwa moja zinapitia ulaya na tunaangalia uk version na si usa version na ndio maana utakuta channel ni ile ile lkn program ni tofauti unayoaangalia wewe na ya marekani.kwa wapenzi wa movies na music zuku wapo juu tofauti na dstv ambao movies zao wanarudi rudia
 
Mkuu pamoja na juhudi kubwa ya kujaribu kuipamba Zuku lakini nataka nikwambie kuwa kama wewe usivyoweza kuilinganisha Zuku na akina Startime na ting ndio hivyo hivyo huwezi kulinganisha DSTV na Zuku
Kifupi kwa mazingira ya kibongo bongo Zuku wapo vizuri zaidi kuliko akina Startimes na wenzake lakini kwa bei ya sh 40,000 bado ni kubwa hasa ukizingatia kikubwa zaidi kilichozidi kwenye Zuku ni Movies
Kwangu mimi tatizo sio wingi tu wa channel lakini ubora na mvuto wa channel kwa watu husika una matter sana
Binafsi kama ni sh 40,000 bora nijipinde na DSTV au nikomae na akina sh 9,000

Labda hii zuku ina packege zake nivizuri ukitujuza na bei au bei ni moja tu 40,000?
 
si kwamba naipamba zuku ninachoelezea nikuwa ili kupunguza gharama za kuumia na laki na 30 kwa mwezi[tena leo wametangaza kuanzia april moja ada itaongezeka kwa package zote] kwa premium bouquet ya dstv unaweza ukawa na zuku ambayo nipungufu ya gharama na mpira ukaangalia pub,channel zingine zote content zake hazina tofauti kati ya dstv na zuku tofauti ni majina tu.kusema ukweli dstv wapo juu hasa kwa sports na series wanapata the best series na sports unaangalia kila kitu tatizo ni kwenye movies wanarudia sana.kama fungu lipo la kulipia premium nenda dstv lkn kama halipo nenda zuku....ukilipia compact bouquet channel za movies ni mbili mnet action na universal studio na unalipia elfu 50,music ni channel o na trace,sports ni espn,ss9 haina ligi yoyote ya ulaya,sasa hapo angalia wewe bora dstv compact kwa alfu 50 au zuku kwa 40..dstv wananyonya sana ndio maana nina hasira nao na toka zuku wameingia decoder yao nimeweka kabatini,sitatumia tena.
 
Kukiwa na ushindani DSTV watashusha tuu bse in Kenya its cheaper than in Tz.
Ila nao wacheki namna ya kuinclude mpira wale nyomi!
 
unatakiwa kuhamia dar tu mkuu

hutakiwi kuhamia huko.unatakiwa kununua seti ya zuku(ungo wa ft2 na decoder yao) kwa tsh 112000/= wana package 3, ya sh 20000, 40000 na 60000.
 

mi con hata sababu ya ku2mia hata cent 1 kupata tv chanels.kama mpira kuna tv kibao zinarusha mechi bure,movies ndio kabisaaa.cdhani kama kuna m2 anaweza kuangalia mpira kati ya ssea na wolves.nilishawahi kusema humu ndani kuhusu king'amuzi cha ting aal-03 nilionekana kama wakala vile.tangu nimepata king'amuzi hicho cjawahi hata cku moja kulipia hata cent,co nawaibia lah ila kinanipa uwezo wa kupata tv za bure
 

Boss, nilidhani umechange ID, kumbe bado upo. Au ulikuwa shimoni?
Tabia mbaya hii ya kuhama bila kuaga majirani! Tulikumiss sana hasa katika mambo haya.
 
Boss, nilidhani umechange ID, kumbe bado upo. Au ulikuwa shimoni?
Tabia mbaya hii ya kuhama bila kuaga majirani! Tulikumiss sana hasa katika mambo haya.

poleni sn kwa kunikosa kwa muda mrefu.ni kweli nilihama kutoka kahama to mzumbe.kwa ss niko likizo na nafikiria kufungua thread ya fta installation cku za usoni ili wa2 waco wavivu km wewe mset tv chnls zenu wenyewe ili muwe huru ku2mia anga.
 
wana local stations ngapi? nimeona mbili...analogue inavyoaga, vin'gamuzi vyote inabidi viwe na local channels zetu zote, coz tulikua tunazipata for free...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…