Zuhura Yunus wa BBC Swahili, amesema maisha ya London Magumu huwezi hata kusevu

Hapo naona ameamua kuficha ukweli kuhusu maisha akiogopa ndugu watampiga vizinga

Maisha popote ni jinsi unavyojiwekea matumizi yako tu kama unataka kuweka hela na mshahara wa kawaida kama £30,000 kwa mwaka hapo ukipanga bajeti vizuri unaweza kujiwekea 2m mpaka 2.5m ya kibongo kwa mwezi

Kuhusu public transport ni punguzo pia kuliko mwenye gari ila unaweza kuwa na gari na ukabaki na savings pia

Kama utakuwa mtu wa matanuzi huwezi kutoboa hapa
 
Hili ndilo lingekata mzizi wa fitina. Ndio, waweza kutumia $3,000 kwenye bili kwa mwezi lakini unasevu $8,000 kila mwezi. Sasa hapo kuna tatizo gani? Hapa Bongo waweza kutumia Tsh milioni 1 kwenye bili kwa mwezi lakini unasevu milioni 1 kwa mwezi. Gharama za maisha ni juu London na mishahara nayo iko juu. Hapo BBC kuna watu wanalipwa mpaka Pound 200,000 kwa mwaka.
Huyo Salama hakumuuliza kuhusu mshahara anapokea sh, ngapi? ili tupime ugumu wa jiji la malkia?
 
Hapa ndo nimekumbuka ile concept ya CONSUMER PRICE INDEX (CPI). Yaan Tanzania Shilling ina thaman kuliko Sterling pound kwa kiasi kikubwa sana.
 
Inawezeka yapo juu Ila mshahara Ni mkubwa pia mwalimu wangu alisoma kule masters alisema kikombe Cha kahawa mjini London Ni sawa na elf 80,000 za kitanzania ...
Mwambie mwalimu wako aache urongo.80elfu labda kama ni kawaha ya dhahabu.
 
Screenshot_20210613-124849.png
 
Sio ajabu,hata kama maisha yapo juu,lakini na pesa inapatikana.Hapa bongo,Miji ya Arusha,Dodoma,ni mojawapo ya miji yenye maisha yenye gharama sana,
Ukiwa Kahama,chumba kimoja Cha kisasa Cha kupanga ni Tsh 40000,chumba Cha aina hiyo Dodoma,ni Tsh 100000,sasa jiulize kwanini vijana wa boda boda waliopo Dodoma hawa hami Dodoma na kwenda kuishi Kahama,?sababu ni moja tu,Richa ya maisha kuwa juu Dodoma,pesa inapatikana,shughuri za kupata pesa kwa urahisi zipo kuriko Kahama.
Point.
 
London maisha ni magumu sana sana hata wazungu wanapaogooa !!! Niliwahi kwenda UK nikaishi Hereford and Reading(spelling) kidogo maisha yapo chini!!! Nilimuuza mwenyeji wangu ambaye ni mwalimu akaniambia kipato chake kwa mwezi !!!!!! Kwetu ni kiimua mgongo!!!
kiinua mgongo?
 
Back
Top Bottom